Siku hizi, kuna ugumu wakati
mwingine, kujua kama mtu ni mwanamke au ni mwanaume. Vijana na hata watu wazima
wengi wanaume hujipamba sana kwa kutumia vipodozi, ambavyo kwa kawaida,
vimekuwa vikitumiwa na wanawake.
Kuna wanaume wanaopaka nyuso zao dawa za kung’arisha na kupambana
kabisa na ndevu. Hawa ukiwatazama nyuso zao ni kama za wanawake, kwani mwanaume mwenye uso mororo sana huonekana kama mwanamke kwa kiasi cha kutosha.
kabisa na ndevu. Hawa ukiwatazama nyuso zao ni kama za wanawake, kwani mwanaume mwenye uso mororo sana huonekana kama mwanamke kwa kiasi cha kutosha.
Kuna wanaume wanaovaa hereni, bila hata
kujua wazivae kwa namna gani. Uvaaji wa hereni kwa wanaume, ambapo inasemekana
ulianzia kule Marekani, ulikuwa ukifanywa kwa sababu maalum na kwa namna
maalum. Kwa mfano kuna waliokuwa, au wanaovaa ili kuonesha upendeleo wao
kimapenzi (kwa mfano ushoga) na wengine kwa sababu mbalimbali.
Kwa kawaida mwanaume anapotoga sikio
moja tu, hasa la upande wa kulia na kulivisha hereni, inamaanisha kwamba,
mwanaume huyo ni shoga! Kwabahati mbaya hapa kwetu kuna vijana ambao hutoga
sikio moja la kulia na bado wanaamini kwamba, wako salama. Ukweli ni kwamba
siku akikutana na raia wa Marekani wanaotafuta mashoga, hawatasita kumwita na
kumtongoza. Ndio maana yake, kwani nyie mlidhani vipi?
Kwa kawaida wanaume wamekuwa
wakikataa kuvaa mapambo na kujipodoa kama wanawake katika kuonesha kwamba,
mwili wao hauhitaji vitu hivyo kwani ni mwili wa kazi hususan za nguvu na hivyo
mapambo hayawezi kuwa na maana kwao.
Ndio maana najiuliza kujipodoa na
kujipamba huku kwa wanaume na kuvaa hereni na makorokoro mengine yanaashiria jambo
gani?
Je? hii pia ni kwa wanawake wakivaa kikuu inaadhiria nini?
ReplyDelete