0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

May 19, 2011

KUMBE HAKUWA MWENDAWAZIMU! SEHEMU YA MWISHO

ILIPOISHIA.............

Kwa maneno yake mwenyewe mzee Martin alisema “Hivi inawezekana kweli mtuhumiwa awe anaumwa uwendawazimu na awe na uwezo wa kukumbuka kwamba, kwa kuwa mzee Makende aliwahi kumwambia kuwa atamloga, kwa hiyo ndiye aliyemloga na hivyo aamue kwenda kumuuwa? Zaidi ya hapo mtuhumiwa pia anajua kwa usahihi kabisa kwamba alimpiga mzee Makende na mchi mara ngapi kichwani kitu ambacho hakiwezekani kufanywa na mtu mwenye wendawazimu”SASA ENDELEA……

Katika hukumu yake katika kesi hii Jaji Bahati alikubaliana na maelezo yaliyotolewa na wazee wote wawili wa baraza.Katika majumuisho yake kwa maneno yake mwenyewe Jaji Bahati alianza kwa kusema “Swali la kujiuliza hapa ni Je mtuhumiwa alikuwa na uwendawazimu wakati anauwa au la?”Jaji Bahati aliendelea kusema kwamba, kwa mujibu wa kanuni ya sheria kifungu cha 12 na 13 kama vilivyotumika katika kesi ya M’naghten aliyeshitakiwa kwa kosa la kuuwa kwa kukusudia vimeelezea bayana kuhusu watuhumiwa wenye uwendawazimu.Kwa mujibu wa kifungu cha 12 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 imeeleza kwamba sheria inamchukulia mtu yeyote kuwa ni mwenye akili timamu kwa wakati wowote mpaka pale itakapoamuliwa vinginevyo.Lakini kifungu cha 13 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 imesema waziwazi kuwa mtu yeyote hawezi kuchukuliwa kuwa ametenda kosa kama kutenda kwake au kutokutenda kwake na katika muda wa kutenda au kutokutenda alikuwa anasumbuliwa naugonjwa na akili na hivyo kumfanya kutokutambua alichokuwa anakifanya.(Tafsiri ya vifungu hivi ni ya muandishi)Baada ya kunukuu vifungu hivyo Jaji Bahati aliendelea kubainisha kwamba kwa mujibu wa vifungu hivyo jukumu la kuthibitisha kuwa mtuhumiwa alikuwa na uwendawazimu liko kwa mtuhumiwa mwenyewe kwa sababu kwa mujibu sheria inaaminika kwamba kila mtu ana akili timamu, vinginevyo labda mpaka ithibitishwe kitaalamu.Hata hivyo jaji Bahati alikubaliana na Bi Humplick kuwa tatizo la uwendawazimu mtuhumiwa alilodai kuwa nalo halikuthibitishwa kitaalamu, lakini ili kuleta uwiano Jaji huyo alinukuu kesi kati ya Mbekule na Jamhuri ya mwaka 1971 EA 481.Lakini hata hivyo Jaji Bahati alizidi kusisitiza kwamba, pamoja na yote hayo bado kunahitajika ushahidi wa kitaalamu ili kuthbitisha kwamba mtuhumiwa alikuwa na uwendawazimu wakati anauwa?Swala la uwendawazimu limeelezwa vizuri katika kanuni ya sheria kifungu cha 13, kwa mfano kesi kati ya Muswi Musola na Jamhuri kama ilivyonikuliwa hapo juu inawiana na kesi hii.Katika kesi hiyo mtuhumiwa alimuuwa mkewe kwa sababu aliamini kuwa mkewe alikuwa akimloga.Mtuhumiwa aliieleza mahakama kwamba hakuwa anajua ni nini alichokuwa anakifanya wakati anamuuwa mkewe, lakini kulikuwa na ushahidi kutoka kwa Daktari aliyemchunguza mtuhumiwa na kuthibitisha kuwa alikuwa na na akili zake timamu na alikuwa anajua ni nini alichokuwa anakifanya wakati anamuuwa mkewe.Kwa hiyo kwa kusingizia kwake kuwa alikuwa na uwendawazimu mtuhumiwa alidhani kwamba angehalalisha alichokifanya ingawa alikuwa anaweza kutofautisha baya na zuri.Baadae katika mahakama ya rufaa ilikuja kugundulika kuwa ushahidi ulikuwa ni finyu sana katika kuthibitisha hata uwezekano wa kuwa mtuhumiwa alishambuliwa na maradhi yaliyoathiri akili yake hivyo kutojua ni nini alichokuwa anakifanya.Hata hivyo Jaji Bahati aliendelea kubainisha kwamba, kwa kuangalia ukweli juu ya kanuni ya sheria kifungu cha 12 na 13 alikiri kutokuona ugumu kutupilia mbali utetezi wa mtuhumiwa Nestory Hussein Chigawa kuwa alikuwa na uwendawazimu wakati anamuuwa mzee Makende.Jaji Bahati aliendelea kubainisha kuwa iwavyo vyovyote vile kama mtuhumiwa alikuwa hajui ni nini anachokifanya wakati anatekeleza mauaji, basi asingeweza kuonyesha tabia aliyoionyesha kabla na baada ya kutekeleza mauajiMtuhumiwa alikiri mwenyewe kukutana na shahidi wa pili katika kesi hii, mtoto wa mzee Makende aitwae Paschal Makende na alikiri pia kuwa alimpiga mzee Makende kwa mchi mara mbili kichwani, na kwa mujibu wa shahidi wa kwanza katika kesi hii binti wa mzee Makende aitwae Maria Makende akitoa ushahidi wake alikiri kumuona mtuhumiwa akikimbia mara baada ya kumuuwa baba yake mzee Makende.Pia mtuhumiwa huyo huyo alikimbilia kwa shahidi wa tatu katika kesi hii Eduard Chigawa na kumueleza kuwa amemuuwa adui yake mzee Makende kwa hiyo ampeleke kwa mwenyekiti wa kijiji.Jaji Bahati alikiri kuwa hayo sio matendo yanayoweza kufanywa na mtu mwenye uwendawazimu ambaye hajui ni nini anachokifanya.Jaji Bahati aliendelea kusema kwamba hakuna kitu kigeni kwa mtuhumiwa kutweta na kupumua kwa nguvu mara baada ya kumuuwa mzee Makende, kwani mtuhumiwa huyo alikuwa akimkimbiza mzee Makende , na mara baada ya kumuuwa alikimbia kutoka katika eneo la tukio na kwenda kwa shahidi wa tatu ambaye ni mjomba wake Eduard Chigawa. Licha ya hivyo katika kipindi chote wakati kesi hiyo inaendeshwa mtuhumiwa alionekana kuwa katika hali ya kawaida kabisa .Kwa maneno yake mwenyewe Jaji Bahati alisema “Sikuwahi kuona hali yoyote isiyo ya kawaida kutoka kwa mtuhumiwa wakati naendesha kesi hii, hivyo nakubaliana na wazee wa baraza kuwa mtuhumiwa alikuwa anjua ni nini alichokuwa anakifanya na nimeona kuwa utetezi wa mtuhumiwa kuwa na uwendawazimu wakati akitekeleza mauaji haukuthibitishwa kabisa, kwa hiyo kama wazee wa baraza, na mimi naungana nao kuwa tuhuma za mauaji ya kukusudia kama ilivyoainishwa na kanuni ya sheria kifungu cha 196 zimethibitishwa bila shaka yoyote, kwa hiyo basi mtuhumiwa amepatikana na hatia ya kuuwa kwa kukusudia na ninamhukumu kama ifuatavyo;Kwa mujibu wa sheria kuna hukumu moja tu kwa makosa ya kuuwa kwa kukusudia , nayo ni adhabu ya kifo, kwa hiyo basi, nakuhukumu wewe Nestory Hussein Chigawa adhabu ya kifo kwa kunyongwa na haki ya mtuhumiwa kukata rufaa iko wazi”**************MWISHO**************2 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Mkuu zinga la kisa ...duuuh, ngoja nitaipitia tena baadaye maana muda wa ofisi umekwisha

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi