0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Apr 9, 2011

KITUO CHETU CHA FAJI KUKUMBWA NA BOMO BOMOA

Alama ya X katika kituo cha FAJI Bomoa ni andiko ukutani Mwenyekiti Mzee Mbeyela
Mwenyekiti Mbeyela na Katibu Tafsiana


Wanachama wakitoa michango yao


Wanachama baada ya Kikao


Wanachama picha ya pamoja

Huu utakuwa ni msiba mkubwa kwa wanafamilia ya Jitambue, baada ya serikali kuweka alama ya X kwenye nyumba ambayo ndipo kilipo kitivo chetu kikuu cha kukutana na kuelimishana juu ya Utambuzi na Kujitambua.



Kituo hicho ambacho kilianzishwa na Mwasisi wa madarasa haya ya Utambuzi Hayati Munga Tehenan ambaye alifariki hapo mnamo tarehe 5 Mei 2008, kimekuwa ni chachu ya mabadiliko ya kitabia na mienendo kwa wanachama wake na wapenzi waliokuwa wakihudhuria madarasa hayo na wale waliokuwa wakisoma vitabu na magazeti ya Jitambue.



Baada ya kifo cha mwasisi huyo, ni madarasa pekee ndiyo yaliyokuwa yamebaki pamoja na blog hii yaliyokuwa yakiendelea kuelimisha juu ya maarifa haya ya utambuzi.



SIku ya Alhamisi ya tarehe 7 April 2011, tulikutana katika kituo hicho ili kujadili mustakabali wa umoja wetu na kuweka mikakati ya kuboresha uendeshaji wa kituo chetu ikiwa ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuhama katika jengo hilo kabla ya utekelezaji wa bomoa bomoa.



Katika mjadala huo Katibu wa kikundi Dada Tafsiana alieleza changamoto kubwa mbili zinazoikabili familia yetu ya Jitambue.



Kwanza alizungumzia juu ya wanachama wengi kutojihusisha katika shughuli mbalimbali za umoja wetu, inawezekana wakawa aidha wamejitoa, au wameamua tu kukaa pembeni kwa sababu zao wanazozijua. Alibainisha pia kuwa mahudhurio kwa wanachama katika vikao muhimu vya maamuzi ni hafifu mno kiasi kwamba viongozi wanashindwa kupitisha maamuzi mbali mbali kwa kuhofia kuonekana kuungwa mkono na idaidi ndogo ya wanachama. Akitoa mfano alisema kuwa kati ya wanachama 70 aliowatumia ujumbe wa simu ya kiganjani kuwaalika katika kikao hicho ni wanachama 9 tu ambao tulihudhuria.



Pili alizungumzia juu ya kukwama kwa miradi mbalimbali ya umoja wetu kutokana na ukosefu wa fedha, hiyo imekuwa ni changamoto kubwa kwa sababu wanachama wameshindwa kuwasilisha michango yao ambayo ndio chanzo kikuu cha mapato katika kugharamia uendeshaji wa kituo chetu.



Mwenyekiti ndugu Fred Mbeyela Aliwaomba wanachama waliohudhuria katika kikao hicho kutoa mawazo yao ya namna ya kukiendesha kituo chetu ambacho kwa kweli kinaonekana kukosa mwelekeo kwa sasa.



Wanachama tuliohudhuria tulikubaliana kwa pamoja kubadili muundo wa uendeshaji wa kituo chetu.


Kwanza tulikubaliana kwamba tutafute ofisi mahali pengine ili kupisha bomoa bomoa



Pili tulikubaliana kwamba katiba ya umoja wetu ibadilishwe na kuboreshwa zaidi na pia kuwe na masharti ya uanachama yatakayowafanya wanachama wawajibike katika umoja wetu.


Na tatu kuongeza kipengele katika katiba kitakachoruhusu shughuli za Umoja wetu zibinafsishwe kwa mtu au kikundi kitakachojitokeza kutaka kukiendesha kituo chetu.


Ili kufanikisha maamuzi hayo iliamuliwa kwamba patafutwe wataalamu watakaoipitia katiba yetu na kutoa mapendekezo ya namna ya kuiboresha kulingana na matakwa ya wanafamilia.

Waliopewa jukumu hilo ni mimi, mama Juliana Mwenda na kijana mwingine aliyejulikana kwa jina la Jafari.


Waliohudhuria kikao hicho ni:


Fredi Mbeyela – Mwenyekiti

Tasfiana P Kapufi – Katibu

Moshi Mwachura – Mweka Hazina

Dr. John Simbila – Mjumbe

Bi Juliana Mwenda – Mjumbe

Musa Utali – Mjumbe

Jaffari –Mjumbe

Ali Mkandama – Mjumbe

Shaban Kaluse- Mjumbe


Nitaendelea kuwajuza zaidi kila hatua tutakayopiga katika jitihada hizi tuliyoianzisha ya kutaka kuboresha kituo chetu cha Wanafamilia ya Jitambue


1 comment:
Andika Maoni Maoni
  1. Mimi naitwa Lucas Haule. Nimekuwa mwanachama wa FAJI kwa muda mrefu, lakini alipouacha mwili wmasisi wetu, nikawa pembeni.
    Ila nimefurahi kuwa iletiba ya akili bado inapatikana, naomba kuwa nashiriki na kushirikishwa. No yangu ni 0754805111.

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi