0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Jul 22, 2010

NIMSAIDIEJE HUYU?

Kila siku malumbano hayaishi

Ni siku ya Jumatatu jioni niko njiani, naelekea chuoni, mara ghafla simu yangu ya kiganjani ikaanza kuita, nilipokea simu ile na sauti ya kike ikapenya katika sikio langu.

Habari za saa hizi, mpiga simu alianza kwa kunijulia hali, nami bila kusita niliitikia salamu ile. Eti naongea na kaka Shabani? Mpiga simu akanitupia swali,
Ndiye mimi, nikusaidie tafadhali. Nilimjibu.

Kwa kuwa kazi ninayofanya, ninakuwa nikiwasiliana na watu wengi nisiowafahamu, simu ile haikunistaajabisha na nilijua atakuwa ni mmoja wa wateja wetu, hivyo nilitarajia mazungumzo ya kikazi zaidi, lakini tofauti na mawazo yangu, mwanamke yule alijitambulisha.

Samahani kaka Shaban, Je uko kwenye nafasi nzuri tuongeee kidogo maana mazungumzo yangu yanaweza kuwa marefu kidogo.

Nilimwambia kuwa anaweza kuongea kwani wakati huo nilikuwa nimesimama mahali pembeni ya barabara.

Mie naitwa mama K, na ninashi hapa hapa Dar es salaam, Kwa kifupi mie ni msomaji wa Blog yako ya Utambuzi na Kujitambua, na nimekuwa nikivutiwa sana na makala zako kuhusiana na maswala ya ndoa.

Sasa kaka Shabani, aliendelea kunieleza, na wakati wote nilikuwa mtulivu nikmuitikia kuashiria kuwa nafuatilia mazungumzo yake. Mie ninalo tatizo moja, ambalo limejitokeza yapata wiki ya tatu sasa.

Tatizo gani hilo? Nilimsaili.
Ni kuhusiana na ndoa yangu, ni kwamba nimejikuta nikiwa namchukia sana mume wangu, kiasi kwamba sitamani hata kumuona na kila nikimuona najisikia kisirani, nimejitahidi sana kutomwonyesha hisia zangu za chuki dhidi yake lakini nimeshindwa na sasa amejua kuwa simpendi.

Kusema kweli mume wangu nilikuwa nampenda sana na amekuwa ni mwema sana kwangu, ni mtu anayejua kutunza familia na anayewajibika hasa, lakini nashindwa kuelewa, hisia hizi za chuki zimetoka wapi?

Kwa kuwa ameshagundua kuwa simpendi amekuwa akijitahidi sana kutaka kuniridhisha na amekuwa akijitahidi kuniuliza ili kujua sababu za mie kumchukia lakini sina jibu la kumpa ingawa ni kweli namchukia, na kila anapojitahidi kuwa karibu na mimi ndivyo ninavyozidi kuwa na kisirani dhidi yake. Aliendelea kueleza kwa hisia kali mama K.

Awali alidhani mie ni mjamzito lakini baada ya kuniona nikipata siku zangu kama kawaida akashangaa, maana hata kama ni kisirani cha kupata hedhi, basi imekuwa too much, kwani, ananifahamu vizuri sana.

Je hamjawahi kugombana hivi karibuni? Nilimuuliza.

Hapana kaka Shaban. Alinijibu, kisha akaendelea.
Kwa kweli sijui hata hii imetokana na nini,na kitu kingine ni kwamba sasa hivi ninapata hisia za kutaka kuondoka kabisa na kuachana naye, lakini dhamira inanishitaki na pia namuonea huruma yeye na wanangu watatu ambao tumebahatika kuwapata katika ndoa yetu takatifu iliyodumu kwa miaka nane sasa.

Nimekuwa nikimfanyia vituko vingi lakini amekuwa akinivumilia, ila siku za hivi karibuni ameanza ku react na sasa tumeanza kuwa na ugomvi wa waziwazi mbele ya watoto kitu ambacho sio kawaida yetu.

Je kaka Shabani utanisaidiaje ili kuokoa ndoa yangu maana kuondoka nataka lakini dhamira inanishtaki na tunapoelekea ni pabaya, na sijui hata hii hali imetokana na nini?Nilishusha pumzi na kumpa pole mama K, na kutokana na kuwa nilikuwa nawahi chuoni, sikutaka kuwa na mazungumzo mengi na yeye, hivyo nilimuomba tukutane pale katika ofisi zetu za Faji ili tuweze kuongea vizuri na kwa utulivu.

Nilimhakikishai kuwa ndoa yake itakuwa imara kama awali au hata kushinda awali. Nilimwomba tuwasiliane wiki ijayo ili tuweze kupanga muda wa kukutana.

Labda nirejee kwa wasomaji wa kibaraza hiki, Je, tunawezaje kumsaidia mtu anayepatwa na tatizo kama hili, awe ni mume au mke?

Naomba mtazamo wenu

5 comments:
Andika Maoni Maoni
 1. Hi Shabani,

  In this topic they are two things involved.

  1) Tunaitaji uwazi toka kwa huyu mama, inavyoeleza habari yake,, kuna vipengele muhimu sana nahisi anaficha.

  2) Kwa wale wanaoamini nguvu za giza,,,kama kweli amekuwa muwazi basi..aanze kumpigia magoti mungu wake,,tena kwa nguvu za ajabu...ili amuokoe katika hili janga.

  Kwa kifupi Kaka Shabani kazi unayo.

  Gud luck

  Il

  ReplyDelete
 2. lakini hajasema kwa nini anamchukia mume wake kisa ni nini?

  ReplyDelete
 3. Mi nadhani anahitaji kuwa wazi zaidi ili kuweza kumsaidia bado haijaniingia akilini kuanza kumchukia mumewe bila ya kuwa na sababu, Kaluse jaribu kumdadisi vizuri ili aweze kuiokoa ndoa yake kama anavyotaka.

  ReplyDelete
 4. Tatizo kubwa kwa wanadoa wengi ni mawasiliano, hasa wale wanao-oana na bado kuna kitu aibu ndani yake.
  Wandoa wenhi wanshindwa kujua kuwa mkioana,nyie ni ktu kimoa na hapo haitakiwi kufichana, hapo kila mtuu ana uhuru na mwenzake, hapo mnatakiwa mshirikiane na kufichua yale mabaya kwa kukaribisha mema.
  Katika udhaifu wa kibinadamu, mmoja anweza akawa anapendelea kitui fulani au anakichukia lakini anaogopa kumuelezea mwenzake kwasababu kadhaa, ikiwemo kutokuwepo kwa ukarubu wa kimawazo. Matokeo yake mmoja anapata sehemu ambayo anayoyapenda anayapata kwa mwingine, unafikiri kwa udhaifu wa kibanadamu itakuwaje, chuki zinaanza.
  Ili asaidiwe inatakiwa atupe ukweli angalau kidogo, kuna kitu hakipendi kwa mwenzake, au anakipenda lakini hakipati, na je kuna mvuto mahala kwingine?

  ReplyDelete
 5. mi nafikiri ajichunguze vizuri kunakitu au vitu havipendi kwa mume wake, ambavyo vimejilundika taratibu kwa sababu ya kushindwa kuwa wawazi , na imefikia mahali sasa moyo una shindwa kuubeba . tena vinaweza vikawa vitu vidogo dogo sana ambavyo hata yeye na mtendaji wanavipuuzia lakini kumbe ndio vimepelekea hapo . katika mahusiano tumekutana ukubwani na tabia tofauti tofauti. naweza kutoa tu baaadhi ya mifano , mwenzako anaweza kuchukia labda kwa kutompa ushirikiano anapokuadisia kitu , kupuuza , anavyogomba na watoto labda makelele sana , hapendi unavyomgombeza pindi mna hitilafu ,Unavyoonyesha kujali vitu vya nyumabani visiaribike , mf mamananai hii deck unaona sijui , lawama kibao au mama nanii unamuona huyu mtoto anafanya hivi ,zote zinakuwa ni lawama kwa mama , Kama mama hawezi kusimama na kumweleza mwenzie kwamba hapendi , basi ndo vikero vinajilundika unaanza kumchukia . mwanzo nami nilipata shida lakini nilisimama , kuongea pale anakukera inasaidia sana na mtu anabadilika . Zaidi ya yote ni kumuomba Mungu kama kuna roho yoyote imepandwa ili muachane itatoka . Mungu Hapendi kuachana , hivyo mlilie mola wako aitengeneze ndoa yako atakusaidia .

  ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi