0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Jan 3, 2009

GHARAMA ZA HOFU YA KUGEUKANA!!!!!!!

Je umewahi kufikiria ni kwa nini maisha yetu ya sasa tunawategemea sana wanasheria? Kama umenunua nyumba hivi karibuni, ni lazima utakuwa umesaini nyaraka chungu mbovu mbele ya wanasheria.

Nyaraka hizi ni lazima zisainiwe na muuzaji na mnunuaji ili kama mmoja anamgeuka mwenzie, yule anaegeukwa awe salama kwa kiasi fulani.

Kila kitu huanikwa wazi katika mikataba hii ili msirukane baadae ninyi mlioingia katika mikataba hiyo. Hakuna siri tena! Wanasheria wako upenuni mwetu kila kukicha, na ili uweze kusalimika kama utashitakiwa mahakamani huna budi kuweka wakili tena!

Kama unavyojua ni kwamba sheria za nchi zinatungwa na na wabunge. Humo bungeni hawakosekani wanasheria kwa sababu ndio wenye fani; hivyo sheria hizi kwa bahati mbaya tena hutungwa na wanasheria!

Jamii ya wanasheria huweka shinikizo ili tusiweze kuishi bila kuwategemea. Kila mtu katika maisha ya siku hizi analipa gharama kubwa kwa wanasheria ili kuogopa migogoro ya baadae kati ya muuzaji na mnunuaji. Kama ndio hivyo basi tumekwisha!
Kwa mfano kuuza shirika la umma , gharama za kisheria ni nyingi mno; inakadiriwa kufikia shilingi bilioni 100! Hizi ni gharama za kutisha!

Hizi fedha zinazomwagwa kwa wanasheria zingekuwa zinaenda kwa wenye kampuni kama hisa zao na kufaidi matunda ya kazi zao, badala yake zinaenda kwa wanasheria! Kwa kazi gani hasa mpaka walipwe fedha kiasi hicho?

Inatisha sana mpaka wakati mwingine najiuliza miaka 25 au 50 ijayo gharama hizi zitapanda kwa kiasi gani? Hizi ndizo gharama za matarajio ya kugeukana!

Mpaka hapa tunaweza kusema kwamba tuko katika wakati ambapo kila kitu tukifanyacho lazima kianikwe wazi kabisa na kutolewa maelezo ili kuzuia migogoro ya baadae!

Nina matumaini, mbali ya mikataba, kila jambo hata la kawaida linalofanyika ni lazima litafanyika kwa makubaliano ya kimaandishi kwa kila mhusika. Kwa upande wa mikataba ndio hiyo mikataba niliyoisema mapema.

Mikataba ya ndoa ya wapenzi kabla hawajaoana ni jambo la kawaida siku hizi na ni kivuno kizuri tu kwa wanasheria!
Talaka nazo ni biashara nono kwa wanasheria!

Hivi ni kwa nini binadamu asijifunze kusimama kwenye ahadi na kauli zake? Kwa nini asijifunze kula kilicho chake tu? Kwa nini asiwe mnyoofu asiyehitaji kutishwa ili atimize wajibu? Ni kwa sababu amepogoka, anataka kupata anataka kushinda maana kwake maisha ni mashindano.



7 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Tanya Stephens alisema "i'm tired of life and death being sold as a pair" Sijui unalitazama hilo kwa jicho gani, lakini kama mtu unayeamini kuwa anakupenda na ndiye pekee maishani mwako anaweza kupanga kukuua nadhani unaona alilosema na unalosema kuwa tunashindwa kusimama katika ahadi zetu. Ama kama hao wanasheria ndio wanaotunga sheria na kisha wanatumika kuzipindisha kukushindisha unadhani ni nini hiyo? Ni ngumu kuwaza na kutambua ni wapi tumeanguka na ni nini kilichosababisha yote haya (nikimaanisha kugeukana na kupotezana imani) lakini ndio tunalilopa sasa. Ndio vita vya panzi (ambao ni sisi wananchi) ambavyo vyawanufaisha kunguru (ambao ndio wanasheria). Imani kupungua sasa ni kila pembe ya maisha yetu. Na ni upungufu huo unaotugharimu saana. Imeingia kwenye nyumba za ibada, kwenye familia na karibu kila sehemu. Gharama zake twaziona zinavyoathiri mamilioni ya watu. Marekani waliomwamini Osama wakati fulani kuwatimizia haja zao, ama Saddam wakati fulani sasa kugeukana kwao unaona kunakotupeleka. Huo ni mfano halisi wa gharama tunazolipa kwa kutosimama kwenye yale tusemayo na pia kuendekeza maslahi binafsi. Ni UBINAFSI unaoibua yote haya na twaweza kuona mwanzo wake, lakini dalili za mwisho wake hazifikiriki.
    Blessings

    ReplyDelete
  2. Asante kwa kibaraza chako cha leo nimefurahi sana ila umesema san
    a juu ya wanasheria na kuona kuwa ndio kila kitu hapa duniani jambo ambalo ninalipinga kwa sababu hapa duniani kila kazi inaumuhimu wake wewe hapa unahabarisha kupitia mtandao, unaumuhi sana katika jamii kwani bila habari ni sawa na giza.

    Asante na ubarikiwe.

    ReplyDelete
  3. Asante kwa kibaraza chako cha leo nimefurahi sana ila umesema san
    a juu ya wanasheria na kuona kuwa ndio kila kitu hapa duniani jambo ambalo ninalipinga kwa sababu hapa duniani kila kazi inaumuhimu wake wewe hapa unahabarisha kupitia mtandao, unaumuhi sana katika jamii kwani bila habari ni sawa na giza.

    Asante na ubarikiwe.

    ReplyDelete
  4. Ahsante sana mzee wa changamoto kwa maoni yako.
    Naomba nikiri kwamba maoni yako ndio chanzo cha kuibua hoja mbali mbali katika blog hii.

    nawe kaka Fita ahsante sana kwa maoni yako, na ningependa kukukaribisha tena na tena hapa kibarazani

    ReplyDelete
  5. Ahsante sana mzee wa changamoto kwa maoni yako.
    Naomba nikiri kwamba maoni yako ndio chanzo cha kuibua hoja mbali mbali katika blog hii.

    nawe kaka Fita ahsante sana kwa maoni yako, na ningependa kukukaribisha tena na tena hapa kibarazani

    ReplyDelete
  6. mmmm naogopa siku hizi kunua nyumba maana kwa umri huu natamani sana kuwa na nyumba yangu wakati wazee wakubw awamekosa nyumba. lakini haya mambo ya UTAMBUZI nayo matamu kweli asante Kaluse kwa somo

    ReplyDelete
  7. Hivi karibuni baba yangu kageukwa.
    hivi sasa kesi iko mahakamni na anazidi kukamuliwa fedha na hao wanoitwa wanasheria.

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi