Kwa nchini Marekani, tatizo la unene ni janga la kitaifa....
Swala la wanawake kupunguza unene sasa limefikia katika hatua ya kushtua. Hivi sasa huko nchini Marekani mtaalamu mmoja amegundua njia mbadala ya kuwawekea wanawake kiraka cha kipande kigumu mithili ya turubai chenye ukubwa wa stamp ya kwenye barua kwenye ulimi.
Kipande hicho kinashonewa na nyuzi zisizopungua sita ili kuwafanya walioshonewa kipande hicho kushindwa kula vitu vigumu na kuishia kunywa vitu vya majimaji na hivyo kupunguza kula vyakula vigumu vyenye virutubisho (Calories).
Njia hii ambayo imeonekana kupendwa na wanawake imeonyesha kuleta matokeo mazuri ambapo waliowekewa kipande hicho cha turubai wamekiri kupunguza uzito wa kilo 15 kwa mwezi.
Njia hii imeleta matumaini kwa wale wanawake ambao walikuwa wanachukia miili yao na ambao walipoteza wapenzi wao kwa kukimbiwa kutokana na kuwa na miili tipwa tipwa na kupoteza shape walizokuwa nazo awali.
Akizungumzia kuhusu ugunduzi wake mtaalamu wa ugunduzi huo Dk. Nikolas Chugay wa huko Beverly Hill nchini Marekani amedai kwamba anachofanya ni kuwapa muongozo wa vyakula wanavyotakiwa kula wale wanaowekewa viraka hivyo ambavyo ni vya majimaji na vina vitutubisho maalum ambavyo husaidia kupunguza mafuta mwilini.
Mtaalamu huyo anatoza kiasi cha dola 2,000 kwa tiba hiyo.
Hii inaonyesha ni kiasi gani wanaadamu wamekuwa wagumu kuwa na nidhamu ya kula hata pale wanapotakiwa kufanya hivyo na wataalamu wa tiba ili kupunguza uzito na ndio sababu ya mtaalamu huyo kuja na njia hii mbadala ambayo inamfanya mtu aliyewekewa kiraka hicho kuacha kula vyakula vigumu kwa lazima kutokana na kiraka hicho kilichoshonewa kwenye ulimi kumfanya ashindwe kutafuna vyakula vigumu.
Naamini bado kitambo kidogo tiba hii itaingia nchini na sitashangazwa na wimbi la wanawake watakaokimbilia tiba hii.
Kwa nini watu wasifanye mazoezi na huku wakiendelea kula kama kawaida? Na hiyo mbinu iliyogundulika hicho kiraka atakuwa nacho hapo kwanye ulimi maisha yake yote?
ReplyDelete