0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Jul 23, 2014

Saikolojia ya wanawake kuchagua mwenza inachekesha sana…!



http://blacklikemoi.com/wp-content/uploads/2013/08/14/black-women-friends-640x325.jpeg
Ukichekewa na mashosti wake kama hivi, basi ujue umelamba dume.......!

Wanasaikolojia wakiongozwa na mwanasaikolojia Benedict Jones wamegundua kwamba, mwanamke akitaka kupima uzuri wa mwanaume ambaye angependa kuwa rafiki au mpenzi wake, hupenda kujua kama hata wanawake wenzie wanampenda kama yeye anavyompenda……..

Anavyozidi kuwaona wanawake wenzie wakitabasamu au kumchekea mwanaume huyo anapopita mbele yao ndivyo atakavyojua kwamba, huyo mwanaume ni mzuri.



Hali hii inafahamika kama copycat reflex na ni matokeo ya nadharia ya Darwin ya mambo ya mabadiliko ya maumbile ya viumbe, kwa mujibu wa wataalamu hao, yaweza kutumika pale ambapo mwanamke anakumbana na wanaume wengi wanaomtaka lakini anapata matatizo ya kumchagua yupi na kumwacha yupi.

Au akiona uchaguzi wa mwanaume bora utamchukulia muda wake mwingi na nguvu zake hujirahisishia kwa kuchukua uamuzi wa kuwaangalia wanawake wenzie wanavyomwona mchumba wake mtarajiwa. 

Uchunguzi huu hufanyika bila wanawake wenzie kujua kwa hiyo mwanaume anayeonekana kuchangamkiwa sana na wanawake wenzake kwa lengo la kumvuta ili awe mpenzi wake ndiye ambaye atapata uwezekano mkubwa wa kukubaliwa na mwanamke huyo.

Watafiti hao wameripoti matokeo ya utafiti huu katika jarida la British Journal Proceedings of the Royal Society B. Katika utafiti huo, watafiti hao waliwatumia wasichana 28 waliojitolea wakiwa na wastani wa umri wa miaka 24

No comments:
Andika Maoni Maoni

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi