0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Feb 6, 2014

KUCHAGUA MWENZA: PALE MWANAMKE ANAPOJIKUTA KALAMBA GARASA...!



Kuchagua mwenza: Pale mwanamke anapojikuta anaangukia kulamba GARASA…!

Linapokuja swala la mapenzi, wanawake ndio wanaokabiliwa na changamoto nyingi katika kuchagua mwenza hususan pale wanapokuwa wametokana na wanaume kadhaa ambao wameonyesha nia. Kutoka huko hakumaanishi kukutana kimwili bali hata kule kuwa na mitoko (dates) za mara kwa mara ambapo zote zinaonekana kuzaa matunda, hapo ndipo wanawake hujikuta wakikabiliwa na mtihani mzito wa kuchagua kwamba aolewe na yupi.

Nimeshawahi kuwasikia baadhi ya wanawake ambao niko nao karibu wakidai kwamba wanajuta kwa sababu uchaguzi wa wenza waliooana nao haukuwa sahihi kwa sababu ya changamoto wanazokabiliana nazo katika ndoa zao tofauti na matarajio yao.



Je wewe ni mmoja wa wanawake wanaojutia uamuzi wa kuolewa na mwanaume uliye naye sasa?

Ukweli ni kwamba kuna idadi ya kutosha ya wanawake ambao wanajutia uamuzi wa kuolewa na wanaume walio nao leo. Wapo ambao wameshindwa na kujiondoa katika ndoa hizo, lakini wamejikuta tena wakiangukia kulamba garasa kwa maana ya kuolewa na wanaume hao hao wasio sahihi kwao mpaka wanajiuliza kama wana mkosi gani.

Lakini wapo ambao wamefaulu kujifunza kutokana na makosa na wakamudu kukubali matokeo na kubadili namna yao ya kufikiri kutoka upande wa hasi na kuweka fikra zao upande wa chanya, na hivyo kuleta mabadiliko makubwa katika uhusiano wao na kurejesha upendo. Hawa wamefanikiwa kuishi katika ndoa zao bila kujuta wala kuumiza hisia zao.

Wapo waliojitoa na kujipanga upya na kisha kwa umakini mkubwa kupata mwenzi aliye chaguo lao, wakiepuka kutorudia makosa waliyoyafanya awali, hawa mara nyingi sana huwa ni wale waliopata wasaa wa kutuliza akili na kufikiria kwa umakini na kupata jibu kwamba walikosea wapi. Wapo wanaopata msaada wa ushauri nasaha, lakini pia wapo wanaomudu kutuliza akili wakiwa peke yao na kupata suluhu muafaka.

Je mnadhani ni kwa nini linapokuja swala la kuchagua mwenza wapo baadhi ya wanawake ambao huangukia kupata mwanaume Garasa…… 

Mara nyingi wanawake wanaojikuta wakiangukia kulamba garasa ni wale wanaokabiliwa na matatizo yafuatayo:

1. Wanakuwa wamesongeka kutokana na kuvunjika moyo baada ya uhusiano wao wa awali kuvunjika katika mazingira ambayo hawakuyatarajia, hivyo hutafuta suluhu ya haraka ili kuziba pengo. Inapotokea kukutana na mwanaume mfujaji anayejua kujali hisia za wanawake mara nyingi hutokea kumuamini mwanaume huyo bila kukagua maeneo mengine ya tabia, na kwa sababu bado akili yake imefungwa hujikuta amelamba garasa bila kujijua na hata akijua inakuwa ni too late. Hapo ndipo atajiuliza maswali mengi. Je kitoka katika uhusiano huo jamii itamuaonaje? Je itamuona hajatulia? Je itamuona ni Malaya au ana matatizo ya kutomudu kulinda uhusiano? (Kumbuka uhusiano wowote ukivunjika jamii huelekeza lawama kwa mwanamke)

2. Kutojiamini na kusubiri kukamilishwa na wengine

3. Utegemezi wa kihisia

4. Kuogopa kukosea

5. Kuogopa kusikiliza machale yao (Intuition). Kwa kawaida sisi binadamu tuna machale. Kwa mfano kama mwanamke anakua na uhusiano na mwanaume ambaye siyo husband material, ipo sauti ndani mwao huwaambia kwamba watafanya makosa kuolewa na mwanaume fulani…. Lakini hutokea kudharau sauti hiyo ambayo mara nyingi hujirudia mara kwa mara. Sauti hii sisi huiita machale, na mara nyingi sisi tumekuwa hatusikilizi machale yetu, hudharau na mwisho wa siku tunajikuta tumeangukia mahali pabaya au tumeumia.

6. Malezi ya wazazi nayo huchangia kuwafanya wanawake wengi kuangukia kulamba garasa katika kuchagua mwenza. Hebu fikiria mzazi au wazazi wanaotukuza watu wenye fedha na kusifia wanawake walioolewa na wanaume wenye fedha. Kama anafanya hivyo mbele ya watoto wake wa kike,hapo somo linakuwa limetimia kwamba mwanaume wa maana ni yule mwenye fedha tu, na hapo ndipo unapoweza kumuona mwanamke anangukia kwa mwanaume mwenye fedha lakini mnyanyasaji na mzinzi kupita kiasi lakini yumo tu haoni wala hasikii…

7. Makundi, hii nayo ni shule nyingine ambayo huwakabili wanawake wengi kuangukia kulamba garasa wanapochagua mwenza, mafunzo ya makundi bila kuchanganya na zako huwaponza wanawake wengi......

No comments:
Andika Maoni Maoni

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi