0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Jan 30, 2013

KISA CHA DAVID CRESPI NA MAUAJI YA MABINTI ZAKE MAPACHA.....!







Mnamo Januari 2006 lilitokea tukio moja la kutisha nchini Marekani. Yapo matukio mengi ya kutisha yanayotokea nchini humo, lakini hili lilikuwa ni la aina yake na kwa kweli lilivuta hisia za watu wengi.

Mtu mmoja aitwae David Crespi ambaye alikuwa ni makamu wa rais wa benki moja maarufu nchini Marekani, aliwauwa watoto wake mapacha wa kike waliokuwa ana umri wa miaka mitano kwa kuwachoma kwa visu mara kadhaa mwilini na kisha kupiga simu Polisi na kutoa taarifa kuwa ameuwa.

Mkasa wenyewe ulikuwa hivi:

Siku ya tukio bwana David ambaye alikuwa na tatizo la msongeko (Depression), alikuwa nyumbani kwake katika jimbo la North Carolina na mkewe, ambapo alikuwa na mapumziko ya wiki mbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya tatizo hilo la msongeko.

Baadaye mkewe alimuaga kuwa anakwenda kutengeneza nywele na kumuacha na watoto wake wawili mapacha. Alipoondoka wale watoto walimuomba baba yao wacheze mchezo wa kujificha, na wakati wanaanza kucheza, baba yao alikwenda jikoni na kuchukua visu viwili. Alikuja navyo sebuleni na kuanza kumshambulia mtoto wa kwanza aitwae Samantha kwa kumchoma kisu mara 18 kifuani, mgongoni na kichwani.

Pacha mwenzie aitwae Tessara alipoona mwenzake anashambuliwa, akaanza kukimbia ili kujificha. Alifanikiwa kujificha ili baba yake asimwone, lakini bahati haikuwa yake, kwani baba yake alimfuata huko mafichoni na kumchoma kisu mara kumi na nne. 

Alipomaliza kuwauwa, alipiga simu polisi na kuwajulisha kuhusu mauaji aliyoyafanya kisha akabadilisha nguo kwa kuvua nguo zenye damu na kuvaa nguo nyingine kabla Polisi hawajafika. Wakati wote huo alikuwa hajarejewa na ufahamu wa kuona kama alichofanya ni kitendo cha kinyama na kikatili. Lakini baada ya Polisi kufika, ndipo aliporejewa na fahamu na kugundua kuwa ameuwa watoto wake wa kuwazaa.

David ambaye sasa anatumikia kifungo cha maisha gerezani, majirani zake pamoja na wafanyakazi wenzake wanamwelezea kama mtu muungwana sana na aliyeonekana kuwa mwenye mafanikio. Lakini hakuna aliyejua kama alikuwa na siri kubwa moyoni aliyokaa nayo kwa miaka 11 ya kutaka kuiangamiza familia yake mwenyewe ya mke na watoto wake watano.

Wakati anahojiwa na polisi alikiri kuliona tukio la kuwauwa wanaye kama jukumu lake, kwani kulikuwa na kitu kinamwambia auwe na aliona afanye hivyo. Pia aliona kumuuwa mmoja isingekuwa busara, kwani kwa kawaida malezi ya watoto mapacha hutendewa jambo wote kwa pamoja.

Alipoulizwa kwa nini asijiuwe yeye mwenyewe, badala yake akauwa wanaye, David alikiri kufanya majaribio kadhaa ya kutaka kujiuwa, lakini mkewe aitwae Kim alipozungumza naye na kumshauri kwamba asije akafanya tena jaribio la kutaka kujiuwa aliahidi kutojaribu tena kufanya hivyo.

Tatizo la msongeko (Depression) ni kubwa sana nchini Marekani. Matukio mengi ya mauaji yanayotokea nchini humo ni ushahidi tosha kwamba tatizo ni kubwa zaidi. Inakadiriwa kwamba watu wapatao milioni 19 wanasumbuliwa na msongeko na miongoni mwao wapo ambao wameuwa au kujiuwa kutokana na tatizo hili. Kwa tafsiri isiyo rasmi msongeko ni tatizo linalotokea ndani ya ubongo linalohusisha chembe chembe zilizoko ndani ya mishipa ya fahamu kushindwa kuwasiliana vizuri. 

Sababu zinazotajwa kusababisha msongeko ni nyingi lakini kubwa kabisa zinazopelekea mtu kupatwa na msongeko ni hizi zifuatazo:

1. Kupoteza ajira au kuwa na wasiwasi wa kupoteza ajira
2. Kuishi katika lindi la umasikini wa kupindukia kiasi cha kukosa matumaini ya kujikwamua.
3. Kutoridhika na hali aliyonayo mtu kiuchumi na kushindwa kukubaliana nayo kutokana na shinikizo la watu waliomzunguka hususan kwa wanandoa.
4. Migogoro ya ndoa isiyokwisha au ya kifamilia.
5. Matukio kama vile vifo vya wazazi, kutelekezwa utotoni na udhalilishwaji wa kijinsia 
6. Maradhi sugu

Dalili za mtu aliye na msongeko zinatofautiana kati ya mtu na mtu, lakini nitajaribu kutaja chache:

1. Kukosa usingizi au kuwa na usingizi mzito usio wa kawaida
2. Kukosa raha
3. Kujiona ni mwenye hatia
4. Kuwa na wasiwasi
5. Kuishiwa na nguvu kusiko kwa kawaida na kukosa hamu ya kula au kuwa na hamu ya kula kupita kiasi hivyo kupelekea kupungukiwa na uzito au kuongezeka uzito.
6. Kukosa matumaini na kuyaona maisha kama hayana maana
7. Kuwa na mawazo ya kuuwa au kujiuwa ya mara kwa mara.

Mara nyingi dalili za mtu mwenye msongeko zinaweza kudumu akilini kwa miaka mingi bila mtu kujua. Na hata kama muathirika anatamka kwamba atajiuwa au atauwa mtu, inakuwa ni kama masihara kwa mtu asiyeelewa, lakini lazima ifahamike kwamba, wanaotamka hivyo wanakuwa wamedhamiria.

Watanzania wengi wanaosumbuliwa na tatizo hili la msongeko, lakini labda kwa sababu hatuna takwimu sahihi ndiyo sababu tatizo hili limekuwa halifahamiki. Wapo watu wengi sana wameuwa au kujiuwa kutokana na tatizo hili la msongeko, lakini kwa bahati mbaya sana watu hulihusisha tatizo hili na imani za kishirikina. Kuhusisha tatizo hili na ushirikina ni kujidanganya bure, kwani hakuna ukweli wowote na matokeo yake wengi wamejiuwa au kuuwa kutokana na kutopata tiba muafaka.

1 comment:
Andika Maoni Maoni
  1. Depression inasababisha hata mtu kupoteza maisha

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi