0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Feb 3, 2013

LIJUE SHAMBA LA MIILI YA WATU LINALOTUMIKA KWA TAFITI MBALIMBALI..........!


Shamba hili lilianzishwa miaka 31 iliyopita huko nchini Marekani wakati Dk. William Bass alipokuwa akitafuta namna ya kuchunguza mwili wa mtu baada ya kufa. Mnamo mwaka 1981, Daktari huyu alimuuliza mkuu wa kitivo cha sayansi cha chuo kikuu cha Tennessee kama anaweza kutumia sehemu ndogo ya chuo hicho kuweka miili ya watu waliokufa kwa ajili ya kuifanyia utafiti na huo ndio ukawa ni mwanzo wa kuanzishwa kwa shamba hilo ambalo lilikuja kujulikana kwa jina la Anthropology Research Facility.


Kilichofanyika ni kwamba, kituo hicho kiliomba watu wajitolee kukubali miili yao kutumika na kituo hicho pale watakapokuwa wamekufa na baada ya makubaliano hayo watu hao wanapokufa miili yao huchukuliwa na kutupwa katika shamba hilo kwa namna tofauti tofauti kulingana na mahitaji ya utafiti.


Ipo miili inayotupwa kwenye maji yasiyo na kina kirefu, kutelekezwa kwenye nyumba au nyuma ya gari, kutupwa sehemu ya wazi na mingine inafukiwa kwenye kaburi fupi tu na utafiti hufanywa siku nne tangu mtu huyo afariki. Kwa kutumia sayansi ya wadudu, wataalamu hao wanaweza kugundua kwa usahihi kabisa siku mtu huyo alipofariki kutokana na aina ya funza watakaokutwa katika mwili huo.


Kwa kawaida mtu anapokufa mwili wake hushambuliwa na funza. Wale funza wa awali wanaposhambulia mwili huo pia huutayarisha kwa ujio wa funza wengine na hutofautiana kwa muda maalum, kutoka aina moja kwenda nyingine na hapo ndipo wanasayansi hao kwa kutumia aina ya funza na wadudu wengine waliowakuta katika mwili huo hujua kwa usahihi kabisa kwamba mtu huyo alikufa kipindi gani au mwili wake ulitelekezwa mahali hapo wakati gani. Pamoja na utafiti wa wadudu, pia mazingira ya eneo husika (Scene of crime) na hali ya hewa ya eneo hilo kijiografia kulingana na msimu, kwa mfano msimu wa baridi, joto nk, huzingatiwa ili kufanikisha utafiti huo.


Leo hii kupitia shamba hilo la miili ya watu, wataalamu wa kisayansi wa kutatua sababu ya vifo visivyo vya kawaida wamefanikiwa sana kufanya tafiti mbalimbali ambazo zimetumika kutatua kesi nyingi za mauaji nchini Marekani. Kupitia utafiti huo hivi sasa, bila kujali mtu amekufa lini, mwili wa mtu unaweza kutoa majibu sahihi sawa sawa na mwili wa mtu aliyekufa hivi punde. 


Mpaka sasa kuna watu 300 ambao wamejitolea miili yao ili kusaidia kituo hicho kufanya utafiti na inaelezwa kwamba zaidi ya miili 120 hupokelewa na kituo hicho kila mwaka. Kutokana na mafanikio ya kituo hicho, hivi sasa kuna vituo vingine vinne vimeanzishwa katika majimbo mengine kwa lengo hilo hilo la kutatua vifo visivyo vya kawaida na kesi za mauaji nchini humo, vituo hivyo ni:


-Texas University kilichopo San Marcos


-Western Carolina University kilichopo Cullowhee kituo hiki pia hutumika kwa ajili ya mafunzo kwa mbwa wa kunusa (Cadaver dogs).


-Sam Houston University kilichopo Huntsville


-Southwestern Pennsyvania ambacho kinatumiwa na watafiti wa Chuo kikuu cha Carolina huko Pennsylvania.

No comments:
Andika Maoni Maoni

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi