Trish Zemba
Desemba 24, 1993, siku moja kabla ya sikukuu ya Krismas, msichana Trish Zemba alipanda farasi akiwa anataka kwenda kutembea, pengine kuwaalika wenzake kwa ajili ya sikukuu ya Krismas au kwa sababu nyingine. Akiwa njiani, farasi wake alibadilika na kuanza kufanya vitimbwi, ambapo hatimaye alimwangusha chini msichana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 14 wakati huo.
Trish aliumia mguu, ingawa siyo sana. Alilazimika kurejea nyumbani akiwa na maumivu. Baada ya huduma ya kwanza, alipata nafuu kubwa na haikuonekana kama alikuwa ameumia asubuhi ya siku ile. Kwa hiyo alisherehekea Krismas yake vizuri tu. Lakini siku kumi baadaye akiwa bafuni asubuhi alipoteza fahamu na kuanguka. Kuanguka huko kulimtonesha mguu mahali alipokuwa ameumia wakati wa ajali ya farasi. Ilibidi apelekwe hospitalini ambako alilazwa.
Ni tatizo lenye kusababisha maumivu makali sana kwa mgonjwa na kuoza kwa kiungo kilichohusika. Pamoja na madaktari kutumia zile dawa kali kabisa ambazo zinakaribia kuwa kama sumu kwa ukali, bado Trish alikuwa akihisi maumivu makali. Maradhi haya yana tatizo la kumfanya mtu kuhisi maumivu makali kupita kiasi, hata kama ameumia kwa kujikwaruza tu.
Pamoja na yote hayo, wazazi wa Trish walikuwa wakisema kwamba, haitakuwa rahisi kwao kupoteza imani kwamba, mtoto wao amepona. Walisali na kuomba, na kubwa zaidi, waliamini kwamba, binti huyo mdogo angepona tu, bila kujali anaumwa kitu gani au kwa kiasi gani.
Wenyewe waliamini kwamba, mguu ukikatwa, maumivu yatakwisha na hivyo itakuwa rahisi kwao kushughulikia kidonda. Wazazi walikubali, ingawa bado walikuwa wanaamini kwamba, binti yao angepona bila kukatwa kiungo. Kwa nini walikuwa bado wakiamini vile? Ni wazi ni kutokana na imani kubwa waliyokuwa nayo kwa Mungu au chochote wanachokiamini.
Hii ilikuwa ni subuhi ya Machi 11, 1994, pale ambapo wazazi walipofika kwenye chumba cha binti yao, waliogopa sana walipomwona akiwa amesimama. Ukweli ni kwamba, kwa maumivu yake hata kukaa ilikuwa ni vigumu, achilia mbali kusimama. Ilibidi wazazi wale waamini, lakini walishikwa na hofu pia ya uwezo wa imani zao wenyewe.
No comments:
Andika Maoni Maoni