0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Jul 15, 2010

KAMA BOSI WAKO ANAZO TABIA HIZI, BASI UMEKWISHA!

Kuna wakati huwa kama vichaa!

Kuna mamilioni ya wafanyakazi duniani ambao wanafanya kazi chini ya mabosi wakorofi au mabosi ambao hawaelewani nao kutokana na ukorofi wa mabosi hao. Kwa hiyo usije ukadhani uko peke yako kama bosi wako ni miongoni mwa mabosi hao, kwani nawe ni miongoni mwa mamilioni ya wafanyakzi hao.

Kama unaelewana na wafanyakazi wenzako na pia unaipenda kazi yako lakini ukawa huelewani na bosi wako ni wazi kuna tatizo mahali na mara nyingi ni kwamba una bosi mkorofi.

Nawe kama ni bosi, ukigundua kwamba huelewani vizuri na wafanyakazi au watu walio chini yako, basi huenda ukawa na tatizo. Ni vigumu kwa Bosi kukiri kwamba yeye ndiye chanzo cha tatizo pale anaposhindwa kuelewana na wale walio chini yake.

Ni vizuri tukazitaja sifa zifuatazo ambazo ni za bosi mkorofi.

Kama wewe bosi una tabia hizi jaribu kuziacha, na kama wewe mfanyakazi, bosi wako hana tabia hizi inabidi ujue kwamba wewe ndiye mwenye mataizo.

Bosi mkorofi huwa haamini aliye chini yake. Huwa anamuona kuwa hajui vizuri na pia huwa anadhani siyo wa kuaminiwa katika mambo mengi hata yakiwemo ya hela.

Bosi mkorofi huwa haheshimu walio chini yake, anawaona kama watu wenye shida ambao hata akiwafanyaje wakaamua kuondoka, anaweza kupata wengine wakachukua nafasi zao. Kwake, walio chini yake ni watu wenye shida na wasio stahili heshima yoyote, ni kama vifaa tu na sio watu.

Bosi mkorofi huwa hawapi walio chini yake taarifa muhimu kuhusu kinachoendelea hapo kazini, naye hana haja au haoni umuhimu wa wa kujua kile ambacho kinatoka kwao kuhusu maisha yao ya kazi.

Bosi mkorofi huwa hawahusishi walio chini yake katika kujadili mabadiliko muhimu hapo kazini, bali huwashushia tu maamuzi. Pia ni mtu mwenye kiburi na aliye na roho ya kikatili, kwani huwa hataki kusikia mfanyakazi ana tatizo au shida, hana huruma wala kufikiri mara mbili kabla hajaamua kuhusu adhabu kwa aliye chini yake.

Bosi mbaya huwa hafikirii au kujua kwamba kuna uhusiano kati ya kazi na familia, huwatazama walio chini yake kama wasio na familia kwa jinsi anavyowatendea. Anaweza pia akawa anatoa kazi kubwa au malengo makubwa katika muda mdogo sana, hajali kama walio chini yake wanahitaji pia muda wa kupumzika.

Anachotaka yeye kuona kazi imefanywa na sio imefanywaje, walio chini yake ni kama watumwa wake.

No comments:
Andika Maoni Maoni

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi