Muuaji Andrew Cunanan katika muonekano tofauti tofauti
ILIPOISHIA.........................
Siku mbili baadae Polisi waligundua mwili wa Jeff Trail ukiwa umeviringishwa na zulia nyumbani kwa Madson na ilionesha kwamba Jef Trail aliuawa kwa kupigwa na nyundo kichwani na uso wake ulikuwa umepondwa pondwa kwa nyundo.
ENDELEA KUSOMA HAPA........................
Polisi waliamini kwamba Madson hakuwepo nyumbani wakati mauaji yanapotokea, na aliporudi alishikiliwa na ndani ya nyumba yake kama mateka kwa siku mbili huku mwili wa Trail ukiendelea kuaribikapale ndani.
Baadaye Cunanan alimchukua Madson na kumpakia ndani ya gari aina ya Cherokee Jeep, linalo milikiwa na Madson mwenyewe, kisha aliednesha gari hilo umbali wa kilometa 48, Magharibi mwa jiji la Minnesota, ambapo alimpiga risasi mbili kichwani na kuutupa mwili wake ndani ya ziwa na kutoroka na gari la Madson.
Baadaye mwili wa Madson ulikutwa na wavuvi, ambao waliwajulisha polisi.Kupatikana kwa mwili wa Madson kulipelekea polisi kwenda nyumbani kwake ambapo waliukuta mwili wa Trail na mkoba wa Nailoni wenye jina la Cunanan.Walipokwenda kuchunguza nyumbani kwa Trail walikuta ujumbe kwenye mashine maalumu ya simu za mezani inayotumika kuacha ujumbe kama muhusika hayupo, ujumbe ambao uliachwa na Cunnan, ukimualika Trail nyumbani kwa Madson.
Hiyo ilidhihirisha kwamba Cunanan hakuchukua tahadhari kuficha uhusika katika mauaji yale. Mnamo Mei 4,1997,siku tano baada ya kutokea mauaji ya Trail, mtu mwingine aliye julikana kwa jina la Lee Miglin aliye kuwa na umri wa miaka 72, milionea mmiliki wa majumba, alikutwa na mke wake akiwa ameuwawa ndani ya gereji ya gari, katika mtaa wanaoishi matajiri huko Chicago.
Mwili wake ulikutwa umeviringiswa ndani ya plastiki huku ukiwa umekatwa shingoni na kitu chenye ncha kali na mdomo ulifungwa kwa plasta.Inawezekana ni ili asipige kelele.Pia macho yake yalikuwa yameng'olewa na alikuwa na majeraha ya kuchomwa sana na kitu chenye ncha kali.
Hiyo, iliwadhihirishia polisi kwamba kabla ya kuuwawa kwake Miglin alikuwa amteswa sana. Walipochunguza zaidi ndani ya nyumba waligundua kuwa muuaji alijitengenezea mkate wa nyama na kunyowa ndevu zake, na kabla ya kuiba mavazi ya thamani ya Miglin na feza zipatazo dola 2,000 na kutoweka na gari la Miglin aina ya Lexus.
Gari la Madson aina ya Cherocee Jeep lilikutwa likiwa limetekelezwa nje ya eneo la tukio, kwa mara nyingine tena, Cunanan hakuficha kuhusika kwake na mauaji yale.
Mke wa Miglin, mama Margareth ambaye hakuwepowakati mauwaji ya mumewe yanatokea, alikanusha kwamba mumewe alikuwa shoga na kuwa alikuwa akifahamiana na Cunanan.
Siku tano baadaye Cunanan aliibukia Pennsville, New Jersey. Mnamo mei 9,1997, mwili wa mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la William Reese aliyekuwa na umri wa miaka 45, mtunza makaburi katika eneo la Finn's Point, ulikutwa katika eneo hilo ukiwa na majeraha ya risasi kichwani, na aina ya silaha ikiwa ni ileile iliotumika katika matukio ya mauaji ya Madson.
K wa mara nyingine tena makosa ya awali ya muuaji yalijirudia ya kuacha ushahidi wa dhahiri. Gari la Miglin aina ya Lexus liliachwa katika eneo la tukio na gari la Reese aina ya Chevrolet lilikuwa halipo, na h1yo ilionesha kwamba Cunanan alihusika na mauaji yale.
Wakati mwili wa Reese ukigunduliwa, Cunanan alielekea Miami akitumia gari la Reese. Pamoja na kwamba alikuwa anatafutwa na FBI, na alikuwa kwenye orodha ya watu muhimu wanaotafutwa lakini alikuwa hafichi mwonekano wake.
Alipofika Miami alifikia kwenye Hoteli ijulikanayo kama Normandy Plaza ambapo alikaa kwa miezi miwilihuku akijichanganya kwenye klabu za mashoga na kujitambulisha katika jamii ya mashoga wa Miami.
Mnamo Julai 6, 1997, siku tisa kabla ya Cunanan hajamuua Giani Versace, alitumia sarafu adimu ya dhahabu aliyoiiba nyumbani kwa Miglin na kuiweka rehani kwenye maduka maalum ya kuwekesha rehani, ambao aliandikisha jina lake kamili na anuani ya hoteli aliyofikia. Kwa kawaida Wamarekani hutumia sarafu maalum za dhahabu kukopea fedha kwenye maduka maalum ya kuweka rehani {Pown Shop}
Kwa mujibu wa sheria ya jimbo la Florida, taarifa za muweka rehani hutakiwa kupelekwa polisi ndani ya masaa 24 tangu meka rehani kuchukuwa fedha, lakini pamoja na taarifa hizo kufikishw polisi, hazikufanyika juhudi zozote kuchunguza taarifa za mmiliki wa sarafu ile.
Ilipofika julai 15, 1997 ndipo Cunanan alipoitikisa jamii ya wafanyabiashara wa mitindo ya mavazi kwa kumuua Giani Versace.
Ndani ya wiki moja tangu Giani Versace kuuawa FBI wakishirikiana na polisi walianza msako mkali wa kumtafuta muuajina ndipo Julai 23, 1997 saa kumi jioni, polisi walipopigiwa na mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina Fernando Curreira.
Mlinzi wa boti za starehe zilizopo pembezoni mwa bahari, akiwajulisha kwamba amemwona mtu mmoja anayefanana na Cunanan akiingia kwenye boti moja inayotumika kama makazi, na alipojaribu kumsimamisha alimrushia risasi na kuingia ndani ya boti hiyo.
Baadaye polisi walifika wakiwa na kikosi maalum maarufu kama SWAT, wakiwa na mbwa na kuizingira boti hiyo hukukukiwa na helikopta inayoranda angani.
Polisi walikuwa wakitoa matangazo kupitia kwenye spika zao wakimtaka mtuhumiwa ajisalimishe, lakini Cunanan hakufanya hivyo na aliendelea kubaki kimya ndani ya boti.
Ilipofika saa 2 usiku, polisi walisikia mlio wa risasi kutoka ndani ya boti hiyo na kufuatiwa na ukimya. Baadaye polisi walitumia gesi ya kutoa machozi na kuvamia boti hiyo ambapo wakakuta mwili wa mtu akiwa amejipiga risasi kupitia mdomoni mwake na kuharibu uso wake wote kiasi cha kutotambuliwa, pembeni mwa mwiliule ilikutwa bastola ambayo ilitumika katika mauaji ya David Madson na William Reese.
Mwili ule ulikuja kujulikana kwamba niwa Andrew Cunanan baada ya alama zake za dole gumba kufuanana kabisa na alama alizoacha katika duka la kuweka rehani.
Msemaji wa polisi, Baretto alisema, sura yake iliharibika vibaya baada ya kujipiga risasi kiasi cha kutotambulika, lakini baada ya uchunguzi wa alama za vidole, imekuja kujulikana kwamba mwiliule ulikuwa wa Andrew Cunanan.'
Baretto aliendelea kusema kwamba ingawa yapo maswali mengi ambayo hayajapata majibu juu ya mauaji aliyokuwa akiyaendesha Cunanan, lakini, wakati umefika wa watu kupumua baada ya jinamizi lile kuondoka.
Alipoulizwa kwamba, haoni kama polisi walichelewa kumkamata mtuhumiwa wakati alikuwa akijibainisha dhahiri kila anapofanya mauaji.
Baretto alisema, 'sidhani kama polisi walizembea, kwani walichukua hatua madhubuti katika kumsaka mtuhumiwa, naamini hawapaswi kulaumiwa kwani walifanya kazi nzuri.
Mtu mmoja alijitambulisha kwa jina la Nicole-Murray mwandishi wa makala za jamii katika magazeti na rafiki wa zamani wa Cunanan alisema kwamba polisi waliichukulia kesi ya Cunanan kwa wepesi mno, mpaka alipouwawa mtu aliyegusa jamii ya watu maarufu duniani katika biashara ya ubunifu wa mavazi ndipo ndipowakashtuka nakuchukua hatua zinaostahili, kwa wao polisi ilikuwa kama,'Eh” Nguruwe mwingine ameuwawa huko, lakini alipouwawa Gianni Versace ndiyo wakashtuka kwamba yupo mtu anayeendesha mauaji.
******************MWISHO*******************

ni simulizi ya kusisimua
ReplyDelete