0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Feb 13, 2010

MUUAJI SHOGA ALIYEPUKUTISHA WENZIE. SEHEMU YA PILI

Princess Diana na Elton John walimlilia Gianni Versace

Gianni Versace akiwa na Naomi Campbell na Cindy Crowford

Gianni Versace akiwa na wanamitindo wake

Mojawapo ya bidhaa zake


ILIPOISHIA..........

Polisi walivamia katika jumba hilo na kukuta mwili wa mtu aliyekuja kujulikana kama Silvio Alfonso aliyekuwa na umri wa miaka 44, daktari mhamiaji kutoka nchini Cuba, Mwili wake ulikutwa ukiwa nusu uchi sakafuni………..

ENDELEA KUSOMA HAPA.......

Kama ilivyotokea kwa Versace ambaye na yeye alikuwa ni shoga wa waziwazi aliuawa kwa kupigwa risasi mbili kisogoni. Wapelelezi waliamini kwamba kuna uwezekano mkubwa Dk. Alfonso alimchukua Cunanan katika baa moja ya mashoga iliyopo katika viunga vya Miami na kwenda naye kwake kwa nia ya kufanya naye mapenzi na hivyo kuuawa baada ya kuwa wameshafanya mapenzi.

Labda nikujulishe tu wewe msomaji kwamba kwa nchini Marekani mtu anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja kwa upande wa wanaume awe anaingilia au anaingiliwa kinyume na maumbile, wote hujulikana kama mashoga. Pia miongoni mwao wapo wanoingilia na kuingiliwa kinyume na maumbile.

Habari za kuuawa kwa Dk. Alfonso zilisambaa kwa haraka sana jijini Miami na kuleta hofu miongoni mwa jamii ya mashoga nchini Marekani, na kusababisha jamii hiyo kuituhumu FBI na Polisi wa Florida kwamba hawafanyi juhudi zozote za kumtafuta muuaji na kumtia mbaroni kwa sababu tu wanaouawa ni jamii ya mashoga.

Wakati msako wa muuaji Cunanan ukiendelea, majivu ya Gianni Versace yalisafirishwa kwandege ya kukodi kwenda nchini Italia kwa mazishi ya kifamilia ambapo kabla ya mazishi kulifanyika misa maalum katika kanisa la Milan, huku kukiwa na wahudhuriaji wengi maarufu akiwemo hayati Princess Diana na Elton John.

Huku matajiri na watu maarufu wakiomboleza kifi cha Gianni Versace, lakini vyombo vya Habari vgya nchini Marekani viliweka kipaumbele katika kumzungumzia muuaji Andrew Cunanan kuliko Gianni Versace.

Je huyu Andrew Cunanan ni nani? Je, alikuwa na uhusiano gani na na Gianni Versacempaka kufikia kumuuwa? Je, ni kitu gani hasa kilichosababisha awe anauwa watu hovyo tena Mashoga? Maswali yote hayo yalikuwa yakiulizwa na jamii ya Wamarekani, kwani kwa muda mfupi mno muuaji Andrew Cunanan alikuwa maarufu nchini Marekani.

Akielezewa na mama yake wa kumzaa, Andrew Cunanan alikuwa ni shoga Malaya aliyejipachika hadhi ya ya utajiri asiokuwa nao wakati alikuwa ni mtoto wa dalali mmoja aitwae Modesto aishiye Manila, nchini Philipine. Mtu huyu alijipachika majina na nyazifa nzitonzito katika jamii ya mashoga ili kuwafanya mashoga wenzie wamheshimu na kumhofia, na hii ilitokana na kutaka kuchukuliwa na mashoga matajiri na wenye hadhi.

Kuna wakati alijitambulisha kama Andrew De Silver mfanyabiashara na mmiliki wa viwanda kutoka nchini Mexicona wakati mwingine, akijiita Luteni kamanda Cunnings kutoka jeshi la wanmaji la Marekani u mwigizaji kutoka Hollywood, ama mtoto wa tajiri mmoja maarufuu kutoka kutoka Ufilipino.

Kwa ujumla Cunanan alikuwa anajiweka kulingana na mazingira anayojitambulisha nayokwani alikuwa na uwezo wa kucheza na sura yake kwa kujiremba kwa jinsi anavyotaka kwa sababu alikuwa ni mzuri kwa sura na alikuwa na haiba ya kuvutia hasa.

Alikuwa ni shabiki mkubwa wa mavazi yaliyobuniwa na Gianni Versace kwani mavazi mavazi yake mengi yalikuwa na lebo ya Gianni Versace zikiwemo hata chupi zake.

Kufikia mwaka 1997 maisha ya Cunanan yalianza kuporomoka na kupoteza ule muonekano wake wa awali aliokuwa akiuringia. Sura yake ilioneksana kuchakaa na hiyo ilichangiwa na ulevi wake wa pombe kali kupindukia.

Mabadiliko hayo yalimshushia hadhi aliyojipachika na kumshusha thamani kiasi cha kuwa shoga rahisi mno aliyekuwa akiuuza mwili wake kwa bei rahisi ili mradi apate hela ya kujikimu pamoja na ya kunywea pombe na kununulia dawa za kulevya ambazo alikuwa akizitumia kwa fujo.

Rafikie aitwae Mike Scott alieleza kwamba, mnamo April 1997, Cunanan alikwenda kituo kimoja kupima Ukimwi kilichopo San Diego na kugundulika kwamba ni muathirika wa Ukimwi.

Baada ya klupewa majibu hayo, Cunanan alichanganyikiwa na kuondoka Miami kuelekea Los Angeles, ambapo alikaa kwa siku moja na kisha alirejea na kwenda katika viunga vya Santa Monica Boulevard, mashariki mwa Hollywood na kuwa shoga Malaya wa mtaani akijiuza waziwazi.

Kuna wakati aliwahi kumweleza rafiki yake huyo kwamba alikuwa akichukuliw na na watu maarufu wa Hollywood ambao alifanyanao mapenzi bila kutumia kinga ndani ya magari yao na alikuwa akijisifu kwamba atakuwa amewaambukiza Ukimwi sawia.

Katika kipindi hicho, Cunanan alikuwa ameishiwa hasa, kwani alifikia hatua ya kukopa nauli ili anunue tiketi ya ndege aende Minnesota baada ya kumkumbuka mpenzi wake wa zamani aitwae David Madson aliyekuwa na umri wa miaka 33.

Alipofika Minnesota kwa mujibu wa kipolisi, inaaminika kwamba David Madson alikwenda kumpokea Cunanan kwenye uwanja wa ndege na kwenda naye moja kwa moja hadi nymbani kwake ambapo baadae walitoka kwenda kula chakula cha usiku. Wakijumuika nammoja wa rafiki zake David Madson walionekana wakitoka pamoja kurudi nyumbani.

Siku mbili baadae Cunanan alimwalika mtu mmoja aitwae Jeff Trail nyumbani kwa mpenzi wake Madson wakati huo Madson alikuwa hayupo.

Jeff Trail alikuwa ni mwanafunzi kutoka Chuo cha Kijeshi, ambaye alipata kuwa mpenzi wake Cunanan wakati akijiuza kwenye viunga vya San Diego, lakini hawakudumu kutokana na tabia ya Cunanan ya kutumia dawa za kulevya kupita kiasi.

Trial aliyekuwa na umri wa miaka 28 wakati huo inasemekana alitoroka jeshini na kukimbilia Minnesota. Mnamo majira ya saa nne usiku, siku ambayo Cunanan alimualika rafikie Trail nyumbani kwa Madson, mtu mmoja aishiye jirani na nyumba ya Madson alisikia mabishano ya wanaume wakitukanana nyumbani kwa Madson.

Siku mbili baadae Polisi waligundua mwili wa Jeff Trail ukiwa umeviringishwa na zulia nyumbani kwa Madson na ilionesha kwamba Jef Trail aliuawa kwa kupigwa na nyundo kichani na uso wake ulikuwa umepondwa pondwa kwa nyundo.

ITAENDELEA ………………

1 comment:
Andika Maoni Maoni

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi