ILIPOISHIA............
Tulimzika mke wangu na nikarudishwa hospitalini. Nilitoka hospitalini baada ya mwezi mmoja na kurejea nyumbani. Nyumba yangu mwenyewe ilinitisha na nilihisi simanzi kubwa kuwa mle ndani. Watoto wangu walinisikitisha zaidi. Lakini nilishaamua kuikubali hali halisi. Nilikuwa nimekubali kuanza upya maisha.
ENDELEA...........
Siku ya Tatu tangu kurejea nyumbani niliamua kupangua ili kuvipanga upya vitu vya marehemu. Nilipanga nguo zake na mapambo mengine ya kike. Halafu ilibidi kupanga vitu vilivyokuwa kwenye droo zake ambazo funguo zake alikuwa nazo mwenyewe marehemu. Kwa sababu sikuwa najua alipokuwa ameweka funguo za droo zile mbili ilibidi nizivunje moja baada ya nyingine.
Droo ya kwanza ilikuwa na barua na karatasi mbali mbali za mawasiliano na mambo mengine. Hapo nilianza kuzisoma barua. Barua ya kwanza ilikuwa ni kutoka kwa mpenzi wake. Haikuwa ni barua ya zamani, kwani ilikuwa imetumwa kwake miezi minne tu kabla ya kifo chake. Ilitumwa na bwana aliyekuwa ametuuzia ile gari iliyohusika kwenye ajali iliyomuua. Sehemu ya barua ile ilikuwa imeandikwa: Kuhusu hilo nisawa mpenzi.
Wewe mwambie nitawauzia kwa mkopo, tena kwa bei rahisi sana. Lakini hizo fedha utazichukua wewe. Kuhusu kwenda Harare nitakufahamisha, jaribu kwa upande wako kumwambia kwamba utakuwa na semina huko, April. Najua kufika Aprili tutaelekea huko. Nataka tuwe mahali huru na salama ili niufaidi mwili wako na wewe uumiliki wangu, Barua hii ilijaa upuuzi mwingi…… Nilipomaliza kuisoma nilihisi kama ninayeota au ambaye nitaugua kichaa.
Ni kweli huyu jamaa ndiye aliyetuuzia lile gari iliyochukua maisha ya mke wangu kwa bei ya chini sana. Gari Nissan Pajero kwa shilingi milioni 3.5 nzuri tu,hata kama imetumika! Kumbe ulikuwa ni mpango wake na mke wangu wa kuipatia familia yangu gari. Nilienda kupekua barua na hati kadhaa. Niligundua hati ya nyumba kwa jina la mke wangu.
Nyumba hii ilikuwa Kijitonyama. Nilipata barua nyingine. Hii ilikuwa ni ya bwana wake wa zamani lakini ilikuwa imeandikwa mwaka mmoja tu nyuma, ilikuwa ikimlaumu mke wangu kwamba hakuwa mkweli Sehemu muhimu katika barua hiyo ilikuwa imeandikwa:Ninajua wazi huyo…….ni mwanangu na hata rafiki yangu…….amesema tunafanana sana. kama umeamua kunidanganya , ni sawa, lakini kumbuka hiyo ni damu yangu.
Sitamchukua wala kumdai lakini kujua ukweli ni muhimu kwangu.Nilipomaliza kusoma barua ile nilishikwa na kizunguzungu. Nilitulia hapo kitandani kwa muda. Halafu niliendelea kupekua kwenye karatasi hizo. Niliona barua kadhaa na kadi za mapenzi.
Kadi mbili zilikuwa zinatoka kwa bosi wake. Barua moja ilikuwa ikitoka uingereza kwa mtu aliyeitwa P Hughes. Huyu ni wazi alikuwa ni mpenzi wa mke wangu kwa muda mfupi, alipokwenda Uingereza miaka miwili nyuma kwa kozi fupi ya miezi sita. Barua yake ilikuwa imejaa sifa nyingi, akimsifia mke wangu kwa kuwa na mwili mzuri na kuwa mtaalamu wa mapenzi na ilisifia shanga zake pia.
Nilihisi nikibana kifua na mapigo ya moyo wangu yalikuwa kama yamesimama. Bila shaka siku ile ndipo yalipoanzia maradhi yangu ya shinikizo la chini la damu, ambayo ninayo hadi sasa.Nilivunja ile droo ya pili ambayo ilikuwa na pichas kadhaa. Zote zilikuwa ni picha za mapenzi. Nilitazama mbili za kwanza, nikatoka chumbani mle nikiyumba.
Naomba nisiseme sana kuhusu picha hizi, kwa sababu, hata kama mtu sio mke wako, ni mwanamke unayemfahamu tu, ukiona picha zake akiwa kwenye hali kama ile, utatahayari sana. Picha unazoziona kwenye mikanda ya ibilisi au kwenye mtandao wa inteneti ndizo zilizokuwa pale kwenye droo, zikiwa ni za mke wangu na wanaume watatu tofauti.
Yule aliyejifanya kutuuzia gari na nyingine za wanaume wawili ambao sikuweza kuwafahamu. Baadae mchana baada ya kupata nguvu nilimpigia simu kaka mkubwa wa marehemu na kumwomba apite nyumbani. Huyu ni mtu wa hekima sana na hadi sasa tunaelewana sana.

Alipofika nyumbani nilimwomba radhi na kumwonyesha barua na picha zile. Alizitazama kidogo na kunirudishia, alikaa kwa muda na kusema, “Huyu sio dada yangu niliyekuwa namfahamu mimi, hii ni aibu kubwa sana shemeji” Hakuweza kusema chochote baada ya hapo, Alipoondoka kwa huzuni kubwa nilichukua nguo zote za mke wangu, barua, picha na vitu vingine vyote ambavyo vingenipa kumbukumbu yake na kwenda kuvichoma moto.
Nilivichomea moto shambani kwangu, Kiwangwa Bagamoyo na kufukia majivu yake. Tangu siku ile hadi leo sijakanyaga kaburini kwake, watoto wake wankwenda na huwa nawahimiza kufanya hivyo. Yule mkubwa anajua mengi hivi sasa baada ya kusimuliwa na baadhi ya ndugu. Nilimwambia kwamba maneno yale hayana ukweli.
Lakini najua anafahamu kuwa yana ukweli, kwani kuna siku aliniiuliza, mbona haoni picha za mama yake ukutani. Nilimwambia, zinanitia uchungu zaidi. Ilibidi niende Afrika Kusini kupima DNA, ili kujua kama yule mtoto mdogo ni wangu kweli.
Bahati nzuri ilionesha kwamba ni wangu kwa asilimia kubwa sana. Hii ilinipa moyo sana. Kilichonitokea kimenifanya nisiwe na hamu hata ya kuwa karibu na mwanamke, achilia mbali kuoa.
Mtu ambaye umemuamini kuliko binadamu mwingine , kumbe ndiye anayefanya uasi usio na kipimo gizani. Nasema hivi mnapaswa kuwaamini wapenzi au wake zenu. Kilichonitokea mimi ni bahati mbaya na ninaamini kam marehemu angeendelea kuishi ni lazima ningekuja kumnasa. --
******************MWISHO*****************

lilofanywa gizani hata hivo limejulikana hadharani. Inasikitisha kuwa limefahamika baada ya yeye mhusika kuuacha mwili..:-(
ReplyDeletenatumaini labda kama lingejulikana kabla huyu bwana asingekuwa na ugonjwa wa moyo :-(
Kaka, life must go on. Upende usipende lazima hao unawakimbia utakuwa nao tu karibu...wenzio tulidhani kama hivo hivo lakini tukaishia kuwa nao :-(
@Kause: pamoja na simulizi hii natumaini alishasaidiwa kupitia FAJI
Hii bonge la elimu Mtambuzi
ReplyDelete