0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Jan 7, 2010

JELA MIAKA MITATU, KISA DADA WA KIJANA KANIKATAA!

Niliamua kurudi shamba na kuwa mkulima


Kwa kifupi sana ni hivi. Mwaka 1975 nikiwa mwalimu kijana bado, nilifanya jambo ambalo kwa wakti ule wala halikunisumbua ingawa lilikuwa bay asana. Bila shaka, wale wanaokumbuka mfumo wa elimu wa wakati ule wanajua kuhusu wanafunzi waliokuwa wanaitwa maripita ambao walikuwa ni wale wanaoanguka mtihani wa darasa la saba shule fulani na kwenda kudurusu darasa hilo kwenye shule nyingine.

Serikali ilikuwa inakataa kabisa wanafunzi kukariri tena darasa la saba au la nyuma yake baada ya kuanguka mtihani. Nikiwa shuleni kule Mbeya mwanafunzi mmoja ambaye baba yake alikuwa na urafiki na mkuu wa shule niliyokuwa nafundisha alikuja kudurusu darasa.

Siku alipokuwa anakuja kuripoti, nilikuwepo mimi ofisini kama mwalimu mkuu msaidizi. Kijana huyo aliletwa na dada yake ambaye alikuwa anafanya kazi hospitali ya mkoa. Nilimpokea kijana yule nikijua kwamba anarudia shule.

Baadaya kumpokea na kujua dada yake anapofanyia kazi, niliona nami ningepata. Kama mkuu wa shule alipata fedha kupitia Yule kijana kudurusu darasa, nilijua na mimi ningepata rushwa ya mwili. Nilimwandikisha kijana huku nikisema kwamba, kudurusu darasa ni mbaya
sana. Yule dada wa kijana alisema ni kweli, lakini ni suala la kusaidiana.

Nilitania kwakusema, “nasi tukija kuomba msaada hospitalini itabidi tusaidiwe.” Yule dada alisema hakuna tabu. Basi kijana alianza masomo darasa la saba nami nilianza kumfuatilia dada yake kule hospitali ya mkoa. Nilifuatilia kwa miezi miwili bila mafanikio zaidi ya ahadi tu.

Nilijua kwamba, Yule muuguzi, dada wa yule kijana alikuwa anataka tu kuvuta muda ili mdogo wake amalize masomo ili anitolee nje. Ilibidi nimwambie kwamba, kama asiponikubalia ombi langu, mdogo wake ni lazima angeanguka mtihani kwani ningekwenda kuchongea mkoani kuhusu kudurusu kwake.

Yule dada aliniambia, kama hilo ndilo lengo langu, ni vizuri nikalifanya. Kuanzia hapo sikufuatilia tena na nilipania kumchongea Yule mdogo wake, jambo ambalo sikujua kwamba, lingemdhuru na bosi wangu, yaani mwalimu mkuu. Ni kweli nilikwenda mkoani na kutoa taarifa kisiri kwa wanaohusika.

Ukweli ni kwamba kijana Yule ambaye alikuwa na uwezo sana darasani alishindwa baada ya jina lake kukatwa na mkuu wa shule kushushwa cheo. Nilifurahi sana baada ya matokeo hayo. Nilikwenda kule Hospitalini kumjulisha Yule dada mtu kwamba mimi ndiye niliyemwangusha mdogo wake.

Yule dada alilia nikiwa hapohapo, huku moyo wangu ukiwa umeridhika. Jioni ya siku ile ile, Yule kijana alikuja nyumbani kwangu hapo shuleni na kuniuliza ni kwa nini nimemfanyia roho mbaya . Nilimwambia amuulize dada yake na kumsisitiza kwamba sio mimi bali ni sheria za
nchi.Yule kijana aliondoka huku akisema, Mungu ndiye anayejua kulipa au kutoa hukumu kwa haki . Nilicheka na kumwambia aende akafie mbali. “Dada yako ni ndege mjanja amenasa kwenye tundu bovu” Nilimpigia kelele. Aligeuka na kunitazama kwa muda, halafu aliondoka. Nadhani angekuwa na nguvu angeweza kunipiga ngumi nyingi sana, lakini hakuwa
na ubavu.

Miaka ilipita na nikawa nimesahau kabisa jambo lile. Ilikuwa ni miaka 25 baadae, mwaka 2000 ni kwamba mwaka 1995 niliacha kazi ya ualimu na kurudi kwetu Iringa. Nilianzisha biashara na kuwa mfanyabiashara. Mwaka huo 2000 nilipata matatizo ambayo yalinifikisha mahakamani.

Kesi iliendelea kwa mwezi mmoja, kabla ya kutolewa hukumu. Haikuwa kesi kubwa, wala ambayo ingenitisha kwa kweli, Haya hukumu yake kwa mujibu wa wanasheria ambao niliwauliza, hakimu alikuwa anaruhusiwa kutoa faini au kifungo cha nje. Sijui walinidanganya kunipa moyo au vipi.

Lakini siku ya hukumu hakimu alinihukumu kwenda jela miaka Mitatu adhabu ya juu kabisa ya kosa langu. Nilibabaika sana na wala sikuamini kama nimehukumiwa kwenda jela. Wakati nikipelekwa kufungiwa selo Yule hakimu aliyenihukumu alinijia na kuniambia.

“Siyo mimi, bali sheria za nchi. Nadhani safari hii dada yangu sio ndege mjanja tena.” Ilinichukua muda, lakini polepole akili ilizibuka wakati nikiwa jela mwezi wa pili, ambapo nilikumbuka lile tukio la mwaka 1975. Sijui nilihisi nini, lakini niliumia sana. Sipendi kukumbuka nilivyoishi kwa huzuni kule jela, nikijutia ufedhuli ule nilioufanya kwa kijana yule wakati ule.

Baada ya kumaliza kifungo changu, bado nikiwa na harufu ya jela nilikwenda nyumbani kwa hakimu yule na kubisha hodi. Alifungua mlango na kunikaribisha ndani kwake bila kinyongo. Nilimsalimia na kumwambia moja kwa moja . “Naomba radhi kwa yale niliyokufanyia wakati ule….”

Yule hakimu alinikata kalma na kusema, “hukufanya lolote baya, ilikuwa ni sheria kweli. Kama ambavyo nami nimetimiza sheria za nchi. Wala huna haja ya kuomba radhi, labda tu kwa sababu, wewe ulikuwa unalipa kisasi baada ya dada yangu kukukataa, wakati mimi sikutimiza wajibu wangu kwa kinyongo.”

Niliinuka na kutoka nje, nikielekea kwangu. Maisha yalikuwa ndiyo kwanza yanaanza na uzee umeingia . Kisa kujisahau.

6 comments:
Andika Maoni Maoni
 1. See my vintage picture blogs:
  http://mynewoldpictures.blogspot.com
  http://mypetarts.blogspot.com
  http://mynaturepictures-benmil.blogspot.com

  ReplyDelete
 2. Kaka shaban mada zako kwa kweli ni mafunzo mazuri sana maana kila ukisoma hapa unatoka na kitu. Ahsante sana kwa lidarasa hili. Endelea kutupa mafunzo haya mazuri ya maisha.

  ReplyDelete
 3. safi and very touching. i think it's fictitious, au?

  ReplyDelete
 4. Mwaipopo, kama umfuatiliaji wa blog hii ya utambuzi, basi hukuwa na haja ya kudhani kuwa habari zinazoandikwa humu ni FICTION.

  Niliwahi kueleza hapa kinagaubaga kuwa nitakuwa nikiandika ushuhuda kutoka kwa watu mbalimbali walioko tayari kusimulia masaibu yao ili wasomaji wapate kujifunza kupitia uzoefu wao juu ya maisha.

  Kuna baadhi ya ushuhuda uliwahi kuandikwa katika Gazeti la JITAMBUE ambalo mimi nilikuwa ni mmojawapo wa waandishi waaandamizi wa Gazeti hilo.
  Kwa muda sasa nimekuwa nikirejea baadhi ya ushuhuda huo ili wale ambao hawakupata nafasi ya kusoma Gazeti la jitambua wapate kujifunza na wale waliowahi kusoma basi sio vibaya wakizirejea makala hizo.
  Shahidi mzuri wa kukuthibitishia hili kuwa hizi habari sio FICTION ni KAMALA NA CHACHA WAMBURA.

  naomba kuwasilisha

  ReplyDelete
 5. mkuu upo matawi ya juu, yaani matawi ya juu yaani matawi ya juu yaani matawi ya juu. msisitizo sina mengi mkuu mungu mkubwa

  ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi