0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Apr 17, 2009

MAZOEA YETU HUJENGA TABIA

Watoto hujifunza kutoka kwa wazazi
Kuna wakati sisi wanadamu tunaweza kujiuliza maswali ambayo ni vigumu kuyapatia majibu ya moja kwa moja. Mojawapo ya maswali niliyojiuliza hivi karibuni ni kuhusu maisha tunayoishi. Nimegundua kwamba tunaishi kimazoea mno, kiasi kwamba hatujui kwamba tunaishi kimazoea, tunaona kama maisha tunayoishi ni ya kawaida.

Hebu tuangalie kwa mfano, kila siku tunaamka asubuhi majira kati ya saa kumi na moja na saa moja asubuhi, tukishaamka tuna piga mswaki tunaoaga kisha tunavaa tayari kwa kwenda shule au kazini. Tunatoka majumbani kwetu aidha kwa magari yetu au kuelekea kituoni kupanda mabasi au kupanda taxi.

Hayo ndio mazoea ninayoyazungumzuia na ninaamini hakuna kati yetu atakayedai kuwa katika maisha yake hafanyi mojawapo kati ya hayo niliyoyaeleza na kama yupo basi labda huyo sio binadamu wa kawaida.
Kwa muktadha huo basi nimekuja kugundua kuwa jambo lolote tunalolifanya kila siku kwa muda mrefu hugeuka na kuwa tabia, kwani mazoea hujenga tabia.

Wote tumejifunza kila kitu kutoka kwa wazazi, walezi ndugu au jamii, kwani tumezaliwa nakukuta wakifanya hayo mambo na sisi labda bila kuuliza tukajikuta tukifanya, inawezekana tulifundishwa au kujifunza mpaka tukaweza na sasa tunafanya.

Hata hivyo sio kwamba mazoea hayo ni mabaya au hayafai, la hasha, sina maana hiyo. Najua kutakuwa na ugumu kunielewa kuwa nalenga kitu gani, lakini taratibu utanielewa. Wewe endelea tu kufuatana na mimi katika habari hii kwani utajifunza jambo moja muhimu sana.

Katika makala zangu nyingi nilizowahi kuandika, huko nyuma niliwahi kueleza kuhusu nguvu ya mawazo, na namna ya kufikiri vizuri, kama hukuwahi kusoma hiyo habari nitakukumbusha.

Niliwahi kusema kuwa, mawazo yamegawanywa katika makundi mawili.Mawazo ya kawaidaMawazo ya kina
Nikasema mawazo ya kawaida ndiyo unayotumia sasa hivi. Haya ndiyo yanayotuwezesha kuwa na utashi wa kuchagua, kwa mfano mavazi ya kuvaa, vyakula tunavyokula, vitabu tunavyosoma na kadhalika na kadhalika. Kwa kawaida maamuzi yote tunayofanya yanaratibiwa na mawazo haya ya kawaida. Pia ndiyo yanayoratibu hii milango mitano ya fahamu, yaani kugusa, kunusa, kuona, kusikia na kuonja.Mawazo haya yanafanya kazi unapokuwa macho.

Unapolala yanapumzika. Huna uwezo wa kuyazuia mawazo haya. Inakadiriwa kwamba, kwa siku moja binadamu huwaza au hupitiwa na mawazo 50,000 mpaka 60,000.Kwa upande wa mawazo ya kina, haya huwa hayapumziki, hata kama umelala yanaendelea kufanya kazi (hayajawahi kupumzika).Yalianza kuhifadhi kumbukumbu tangu ulipokuwa tumboni. Wataalamu wanasema kwamba, mawazo haya huanza kuhifadhi kumbukumbu mimba inapofikisha miezi minane na nusu (hupokea sauti kwa njia ya mawimbi) na kuzihifadhi kwa ajili ya matumizi (rejea) ya baadaye.

Mawazo ya kina hufanyia kazi kile ambacho kimeombwa na mawazo ya kawaida (imani zetu). Imani ni mambo anayokubali mtu kuwa ni ya kweli na anapaswa kuyaheshimu, au ni maoni ya moyo yanayomfanya mtu awe na mkabala fulani juu ya jambo au kitu. Kanuni ya ufanyaji kazi wa mawazo yetu ya kina ni imani zetu (kanuni hii haivunjwi kwani ni ya kimaumbile).Kwa kawaida, matukio, hali zetu za hisia na matendo yetu ni majibu ya mawazo yetu ya kina kwa mawazo yetu ya kawaida.

Mfano: unapoamini katika ushirikina au hofu, matokeo yake yanakuwa ni kulogwa, kuugua, hofu na kukata tamaa. Lakini chenye kupelekea hali hizo siyo ushirikina au hofu, bali imani yako kwenye hofu hizo.Mawazo haya hayana akili, hayachagui kibaya au kizuri, hayana huruma, yanafanyia kazi chochote yalichopewa na mawazo ya kawaida. Wale wenye uwezo wa kutumia vizuri mawazo yao ya kina, wamefanikiwa sana maishani, ingawa siyo kwa mali bali kwa kuwa na furaha au vyote viwili (fikra zao ni nzuri na wamemudu kufuta fikra mbaya kwenye mawazo yao).Mawazo ya kina ndiyo yanayobainisha aina ya maisha tunayoishi.

Mpaka hapo naamini utakuwa umepata mwanga, kuwa nataka kuzungumzia nini. Kama bado inakuwa ni ngumu kung’amua kuwa nataka kuzungumzia nini, basi usiwe na wasiwasi, utanielewa hivi punde.

Awali nimeeleza kuhusu kuishi kwa mazoea, Nimeeleza jinsi mazoea yanavyoweza kujenga tabia. Kwa hiyo kama mazoea yanaweza kujenga tabia, sasa kwa nini tusianze kubadili namna yetu ya kufikiri kwa kuanza kufikiri vizuri, kuanza kufikiri juu ya yale yanayotupa nafuu, yale yanayoweza kutujengea kujiamni?

Nimesema kuwa kile tunachofikiri ndicho kinachoakisi maisha tulionayo leo, kwa hiyo kama tukianza kufikiri kwa namna chanya, kwa namna ambayo itatuletea tija tunaweza kubadili kabisa aina ya maisha tunayoishi.

Ni kiasi tu cha kuamua, na kuanza kubadili namna yetu ya kufkiri na kujenga mazoea kitu ambacho kitageuka kuwa tabia kama vile tulivyojijengea taratibu nyingine za maisha ambazo tunafanya kila siku.

Unaweza kuona ugumu sana kuanza kufikiri vizuri, kwa sababu tulifundishwa kufikiri vibaya, lakini kama utaamua kuwa kuanzia leo nataka kufikiri kuhusu mambo mazuri, mambo yenye kunipa nafuu, yaani kujenga tabia ya kujiamni kuwa unaweza na hakuna lisilowezekana kabisa, kwa maana ya kuwa kama unahitaji kitu chochote, ambacho kitakupa ridhiko lakini hakitamuumiza mtu mwingine inawezekana kabisa kukipata kitu hicho.

Hapa naomba nitahadharishe kuwa, haitakiwi kukokotoa kama utapataje, hiyo haikuhusu, muachie mungu, nimeeleza kuhusu ufanyaji kazi wa mawazo ya kina yenyewe ndio yatakayojua kuwa utapataje na hiyo sio kazi yako, na haikuhusu.

Kukotoa maana yake ni kumpangia (mungu) namna ya kukuletea hicho unachokilitaka, wakati hiyo sio kazi yako, ni kazi yake yeye, na hahitaji kuelekezwa. Mara nyingi watu wengi wanashindwa kupata vile vitu wanavyotaka kwa sababu ya kutojua kanuni hii. Ni kiasi tu cha kusema na kuamini kuwa inawezekana, basi kazi yako imeisha.

Kwa hiyo kama tutajenga mazoea ya kufikiri vizuri, naamini itageuka kuwa tabia, na hivyo kuishi katika maisha yenye amani na utulivu kwa sababu tuna uwezo wa kupata kile tunacho hitaji.

1 comment:
Andika Maoni Maoni
  1. Kaluse; nimefurahi umetoa mada hii ni kweli mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Binafsi nafurahi sana jinsi wazazi wangu walivyotulea mimi na kaka zangu.

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi