0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Apr 8, 2009

KILA MTU ANAVUNA ALICHOPANDA

Tuwe mfano bora kwa watoto wetu

Kila mtu maishani ni zao la mbegu fulani. Hakuwezi kuwa na zao bila mbegu. Kila jambo ambalo linatutokea ni lazima limepandwa na sisi wenyewe au wengine, na sisi tukalipokea kwa sababu tunatembea kwenye masafa ya mawimbi ya aina moja.

Kila jambo tunafikiri, kutenda, au kusema, kwa sababu ni nguvu, ni lazima lizae matokeo kama hayo au makubwa ama mabaya zaidi. Kama ni baya, litazaa baya zaidi na kama ni zuri litazaa zuri zaidi, huwezi kupanda mahindi, ikaota bangi.

Kama mawazoni mwako kumejaa chuki , vitendo vyako ni vya kiharamia na kauli zako ni za kuchonganisha, basi usitarajie nafuu, kwani kamwe hutaweza kuvuna nafuu kutoka katika mbegu hizo unazopanda. Utavuna ulichopanda, hiyo ni kanuni ya maumbile, huwezi kuibadili.

Kila mtu maisha anayoishi ndiyo uchaguzi wake, ameyapanda mwenyewe na sasa anavuna.

Ni vigumu wengi kukubali kwamba maisha wanayoishi ni uchaguzi wao. Hata baadhi ya wale waliofanikiwa kupata watakacho wanaweza kukuambia, “Ni kazi ya Mungu bwana, amenijaalia.”

Hawajui kwamba, wao ndiyo mungu kwenye kutaka nini kitokee maishani mwao.
Baadhi ya dini zinasema, jisaidie na ndipo Mungu atakusaidia. Nyingine zinasema, bisha hodi utafunguliwa. Kubisha hodi ni hadi utembee na kufika mlangoni, bila kufika mlangoni hutafunguliwa. Hii inaonesha kwamba ni sisi tunaoanza kufanya ili jambo liwe.

Kama tunataka kupata tunacholenga kwenye maisha yetu, hatuna budi kujua pia tunachopanda kila siku kupitia mawazo, vitendo na kauli zetu.

Kama unawapenda baadhi ya watu na kuwachukia wengine, utavuna kutoka pande zote, chuki na upendo.

Kufikiri, mitazamo, imani, hisia,vitendo na kauli, ni mbegu ambazo zinapokuja kuzaa baada ya kupandwa hutuletea mazao tuliyoyapanda. Inawezekana tulisahau au kutojua kwamba, tunapanda mbegu fulani. Hili la kutojua halizuii mbegu hiyo kuzaliwa na kukua, hadi kuvunwa, ikiwa ni ya mmea huo huo.

Kwa kadiri tunavyotilia nguvu mawazo, hisia, vitendo, kauli, mitazamo na imani fulani tulizonazo, ndivyo ambavyo tunanyweshea na kutilia mbolea mbegu hizo na matokeo yake yatakuwa mazuri sana kwa ubaya au uzuri, kutegemea tulipanda nini.

Jambo la msingi hapa ni kuchagua kupanda kile ambacho mtu anakipenda.


Ruhusu kwenye mawazo yako, imani zako, hisia zako, mitazamo yako, vitendo na kauli zako, yale tu ambayo yatakupa furaha, amani na utulivu.


Pia ambavyo vitakupa ridhiko, upendo na uelewa.

Usiruhusu hofu, ukosefu, chuki, kijicho,na chochote chenye kuumiza au kumuumiza mwingine, maana hicho ndicho kitakachokujia hata kama hukitaki.

4 comments:
Andika Maoni Maoni
 1. Shabanii, uko sawa kabisa usemayo, ni kweli huwezi kupanda muhogo na ukafikiri utavuna muhindi. Ni kweli inabidi tuwe mfano kwa watoto wetu kwani wao ni wepesi sana kuiga vitu.

  ReplyDelete
 2. Hapa nitarejea kunena jambo. Kuna ukweli ulimo humu

  ReplyDelete
 3. wengine wanaita law karma. kwamba maisha yako ya sasa na ya leo yanategemea maisha uliyoishi huko nyuma. inasemekana kuna sababu ya wewe kuwa kama ulivyo. kwanini huwe kilema, kipofu, kiziwi albino nk. hata wewe mlevi, mzinzi namateso kibao. baadhi ya matukio na maumbile yaweza kuwa adhabu kutokana na unyambisi uliyowahi kufanya huko nyuma.

  onyo! usimnyanyase wala kumchukulia kinoma mwenye mapungufu au nyongeza kwa sababu unahisi labda ni adhabu. sheria kuu kutoka kwa maumbile (Mungu?) inatwambia kuwa; love and respect must be offerd to every God's creation.

  vinginevyo utavuna karma kazi nyingine sio zako mzee

  ReplyDelete
 4. hapo kamanda umelonga ukweli mtupu
  ndio maana hata mimi niliwahi kusema kuwa kuna vijana walio na bahati na wasio na bahati.

  wale waliojengewa msingi mzuri na wazazi wao nawaita wenye bahati na wale ambao hawakuienewa haana bahati na wana kazi kubwa ya kujikomboa wenyewe

  ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi