0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Feb 10, 2009

KWA HILI, UCHAWI HAUNA NAFASI

Furaha yote ya ndoa inaweza kuishia hapa.

Tafadhali ningeomba kusisitiza tena kwamba hupaswi kuwa mtumwa wa mwanamke au mwanaume. Leo hii kuna wanawake na wanaume ambao maisha yao ya ndoa yamekuwa ni jela zao wenyewe. Wanaume na wanawake hawa wamekuwa wakiishi kama vile roho zao ni hao wanaume au wanawake.

Bahati mbaya ni kwamba ndugu na jamaa wa wanaume au wanawake hao huwa wanadhani kwamba ndugu zao wamelogwa na wanawake au wanaume hao wanaowageuza watumwa wao. Je unajua kwamba kuna wanaume hapa nchini ambao huwa wanaombwa na wake zao wahame vyumba kwa sababu wake hao wana wageni ambao ni mahawara zao?

Je unajua kwamba kuna wake wa ndoa ambao huwa wanaletewa na wanaume zao mahawara wa wanaume hao kila wakati na kutambulishwa kwao kwamba “Huyu ni hawara yangu” na bado wake hao wakanyamaza na kuendelea kuwaheshimu waume zao? Wapo, tena wengi kuliko unavyoweza kuamini wewe.

Basi kwa taarifa yako hakuna uchawi wala limbwata katika jambo hili, bali kuna utegemezi wa kiakili na hata kimwili. Mwanamke au mwanaume anafikia mahali ambapo anaamini kwamba akiachwa au kuachana na mke au mume aliyenaye hataweza kuishi kwa amani tena, hatamudu kamwe kuishi bila kumuona. Wengine wanaamini kwamba wakiachana na waume au wake hao hawatamudu maisha peke yao. Huu ni utegemezi mbaya kuliko sumu inayouwa haraka.

Kituo cha FAJI kilichoko Kimara kona kinatoa ofa kwa watu wenye matatizo kama haya au wenye ndugu walio kwenye vifungo hivi wafike kwenye kituo chetu kwenye jengo lililoandikwa “ELIMU YA UTAMBUZI INAPATIKANA HAPA” au watupigie simu kwa namba hizi: +255 713 250701, +255 0715 729292 au +255 754 771601 pia wanaweza kutuandikia kupitia anuani ya barua pepe ya blog hii:
kaluse2008@gmail.com ili tuwape msaada na pia kuwaonyesha kwamba huko sio kulogwa.

3 comments:
Andika Maoni Maoni
 1. Maswala ya siri ya nyumba hayo!:-(

  Nilishawahi kusimuliwa na ndugu yangu wa huko Ukuriani kuwa kulikuwa na jamaa linasifia jinsi gani penzi la kupiga mke linavyotunza na kustawisha ndoa yake.

  Basi ilikuwa kila jioni wakitoka na washikaji zake kwenye KUNYOSHA MIGUU a.k.a kutoka kwenye KILAJI, huyo jamaa nyumba yake ndio ilikuwa ya kwanza na akiingia tu nyumbani washikaji wanaanza kusikia mwanamama anapiga mayowe ya kupigwa. Basi jamaa nao wakaanza kuiga wakifika kwao wanakong'ota wake zao . Mwisho wakaja kustukia kesho ya kipigo ni wanawake zao tu waliokuwa wanahitaji matibabu ya kipigo.

  Kumbe lile jamaa lililokuwa linatoa ushauri wala halikuwa linapiga mke ila walikuwa wanaigiza kwa sababu waliambiwa kabla hawajaamia Ukuriani kuwa kwa Wakuria inabidi upige mke ili mke akuheshimu na walikuwa hawataki kufanya hivyo ila hawakutaka pia kuonekana wao ni tofauti.

  Mambo ya ndani ya nyumba za watu ukisimuliwa unaweza kushangaa. Unaweza kusikia mpaka mambo ya mimba ya mtoto ni ya Baba Mzazi!:-(

  Ila pia kuna stori nyingi sana za kubuni katika maswala ya ndani za nyumba za watu , mtu usipokuwa mwangalifu unaweza kujikuta umejiingiza kwa yasiyokuhusu kujaribu kusuluhisha yasiyopo.

  ReplyDelete
 2. Kaka Kitururu: DUH!!!!!
  ..............

  Kaka Mtambuzi Nimekutumia email juu ya haya uliyoyaandika.
  Naomba tuzungumze nyuma ya Pazia.

  ReplyDelete
 3. Ni kweli maarifa yanapatikana katika kituo cha FAJI yametukomboa wengi katika utumwa wa mambo mbali mabali likiwemo na hilo la utegememezi wa kimwili, kiakili na kihisia.

  Tofauti na maarifa mengine tunayoyafahamu pale unafundishwa namna ya kujisaidia mwenyewe kwa kutenda. Hakika ukipata maarifa hayo na ukayatumia kwa vitendo utapata nafuu ya maisha.

  ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi