0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Feb 16, 2016

Uhusiano uliopo kati ya ngono za mapema na talaka


[​IMG]
Siku hizi idadi ya watoto wa kike wanaoanza ngono mapema ni kubwa kuliko inavyofikiriwa. Lakini pia kuna ushahidi kwamba, wale watoto wa kike wanaoanza ngono mapema wanakabiliwa na matatizo mengi yakiwemo ya maradhi ya kisaikolojia na kihisia. Tafiti zinaonyesha kwamba, miongoni mwa maradhi yanayotokana na kujamiiana kuna yale ambayo yanapokosa tiba ya mapema hayawezi tena kupona.


[​IMG] 
Kuna idadi kubwa ya wasichana ambao walianza ngono utotoni ambao wameathiriwa sana na maradhi haya. Kulikuwa na ubishani wakati fulani miongoni mwa wataalamu wetu wa tiba waliposema kwamba hakuna uhusiano kati ya msichana kutoa mimba na kushindwa kupata watoto au kuwa tasa. Binafsi nakubaliana na hoja hiyo, lakini ninachoweza kusema ni kwamba kuna uhusiano kati ya wasichana wanaoanza ngono wakiwa na umri mdogo na kukosa kizazi ukubwani.Je kinachotokea ni kitugani hasa?
Ni kwamba, katika kuanza ngono za utotoni, msichana anakuwa hajui hata kujikinga na hata anapokuwa nadalili za maradhi ya kuambukiza yanayotokana na kujamiiana anaweza asing'amue mapema.
Ukweli ni kwamba, baadhi ya virusi wa maradhi haya ya kujamiiana wanapokomaa, wasichana hawa huweza kuathirika katika viungo vyao vinavyoshughulika na uzazi. Kwa njia moja ama nyingine, binti huyu anaweza kushindwa baadaye kupata ujauzito kutokana na kuharibika kwa viungo hivyo. Wakati mwingine virusi hao wakikomaa huweza kumsababishia mwanamke kupata kansa kwenye viungo vyake vya uzazi.
Halafu leo hii watu wanashangaa kwa nini wanawake wengi wanashambuliwa na kansa ya kizazi, naamini sasa mmeshajua kwamba hata ngono za mapema kwa wanawake zina mchango wake. Kumbuka kwamba, msichana mdogo anaweza kufanya tendo mara moja tu na kujikuta ameambukizwa maradhi ya zinaa. Kama ameambukizwa moja ya haya maradhi ambayo huathiri mfumo wa uzazi ni wazi matokeo yake ni kuathirika mfumo wake wa uzazi na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kukosa watoto pindi atakapohitaji.
Lakini pia katika utafiti ulioripotiwa hivi karibuni kwenye jarida la Marriage and the Family (Ndoa na Familia), inaelezwa kwamba, kati ya kila wanawake kumi ambao walishiriki ngono za mapema, watano huwa wanaishia kwenye talaka.
Utafiti huo unaonesha kwamba,ngono za utotoni huathiri vibaya uwezo wa msichana kumudu kuwa na uhusiano imara wakati wa ndoa yake. Kwa sababu uhusiano wa vijana mara nyingi umejaa kuachana kusiko na kichwa wala miguu, jambo hili linaweza kumfanya msichan akujenga dhana potofu kuhusu uhusiano na wanaume. Dhana hii baadaye huweza kuathiri uhusiano wake na atakayekuwa mume wake. Kule kuvunjika vunjika kwa uhusiano wakati wa usichana wake, humfanya kushindwa kujifunza na kujua namna au maana ya uhusiano imara unavyotakiwa kuwa. Msichana ambaye ameingia kwenye uhusiano ukubwani, anakuwa anaingia akifahamu kuhusu kujifunga kwenye uhusiano. Huyu aliyezoea kuachwa mara kadhaa kwenye uhusiano wa kingono wa utotoni,hudhani hiyo ndiyo maana ya uhusiano.

1 comment:
Andika Maoni Maoni
  1. Hii ni kweli kabisa hata juzi tu nimesikia hii habari na mbaya zaidi wamesema ya kwamba siku hizi vijana wengi hawatumii kinga na hii inazidi kusababisha maambukizi.

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi