Wanawake ndio hupata tabu zaidi lijapo swala la kuchagua
Hiki ni ni kizazi ambacho binadamu anatakiwa kufanya uchaguzi mwingi. Kuna mambo mengi na vitu vingi, kwa hiyo binadamu anatakiw achague miongoni mwa vingi ili apate cha kumfaa.
Mababu zetu wa kale walikuwa awana tabu hii a kuana uchguzi. Kwanza wasingeweza. Sisi tunaweza kufanya uchguzi lakini hata sisi tunauchosha ubongo. Kipindi ca mababu zetu vitu havikuwa vingi. Mara nyingi kulikuwa na mambo mawili: kupata kitu au kukosa.
Kwa hiyo walikuwa hawana uchguzi. Mathalani, akienda porini kuwinda ama angepata mnyama au kukosa. Mababu zetu walikuwa na uhaba wa chakula, uhaba wa usafiri na usafiri wao ulikuwa miguu yao. Kutokana na hilo, katika suala la uchaguzi mababu zetu walikuwa na kazi ndogo tu wa kuchagua kilichobora sana.
Ili kunufaika sana na neema iliyopo mbele ako yahitaji mahali ambapo huna uchaguzi yaani vitu vya kuchagua ni vichache. Maisha ya kisasa yana vitu vingi vya kuchagua tofauti na enzi za mababu zetu. Kwa hiyo si rahisi kunufaika sana kutokana na jambo utakalolichagua kulifanya.
Mathalani kama ni mkiriimba kwa maan kwamba unazalishaaina Fulani ya zao peke yako, utanufaika zaidi kuliko kama kitu hicho kingekuwa na wazalishaji wengi.
Ndio maana nasema kwamba, watu wa kale walikuwa wananufaika sana kutokana na ukiritimba huo wa kuwa na uchaguzi kidogo ukilinganisha na maisha a siku hizi ambapo uchaguzi ni mkubwa na hivyo kutokuwapo ukiritimba ambao ungeleta manufaa kwa mtu mzalishaji. Enzi za mababu, vitu vilikuwa adimu, na siku hizi vitu ni vingi. Kwa kawaida uchaguzi huleta wasiwasi kwa sababu tunalinganisha; kwamba tumefanya lakini tungeweza kufanya kwa ubora zaidi.
Mababu zetu wasingekuwa na maswali ya kujiulizanamna hii kuhusu ubora wa kazi zao kwa sababu walikuwa awana vitu vya kuchagua vya kutosha kuweza kujilinanisha. Ni sawa na mtu msikini kufikiria kukodi ndege. Kama ana fedha kidogo basi atapanda basi au lori badala ya ndege. Kitu ambaho hana uwezo nacho hana uwezo wa kukichagua. Kiko nje ya mkono wake.
Kama nilivyosema awali kama kuna uhaba wa vitu, mtu halzimiki kufanya uchaguzi. Hata akichagua kitu kibaya sio aki kumlaumu. Lakini maisha ya sasa ukichagua vibaya tapata lawama kwa sababu una vitu na mambo mengi ya kuchagua.
Kukiwa na vitu vingi vya kuchagua utapatashinikizo khakikisha unafana uchaguzi kwa usahihi kabisa. Kwa mfano, umepewa vitu 25 mbele yako vinavyofanana na vyenye bei moja ili uchague kimoja; ukichagua kibaya utajilaumukwa sababu ulikuwa na nafasi a ya kuchagua kitu kizuri pia. Kwa hiyo, hapa busara ilikuwa inahitajika katika kufanya uchaguzi huo. Mwanasaikoljia Barrry Schwartz anasema kwa kukiwa a mambo mengi ya kuchagua sisi binadamu tunabaki na hali ya kutokutosheka hata kama tutakuwa tumefanya maamuzi sahihi; hata pia kama tumepata mafanikio.
Kila wakati tunahaha kujua kama tulifanya uchaguzi sahihi au la, kwa kuwa tua uchaguzi mwingi; mababu zetu walikuwa awasumbuliwi na mambo ya uamuzi sahihi au usio sahihi. Maisha ya siku hizi kama uamuzi unaonekana ni wa utata matokeo yake ni mashaka na wasiwasi. Ukiwa na vitu vichache vya kuchagua hukuondolea hofu na wasiwasi. Mababu zetu walikuwa wanaomba itokee siku moja wawe vitu vingi na kuweza mkuanya uchaguzi.
Walikuwa wanadhani kwamba kukiwa na vitu vingi, basi maisha kwao yangekuwa bora zaidi. Hata sisi wa kizazi hiki tunafikiri hivyohivyo. Lakini tumethibitisha kwamba maisha yenye vitu teletele hayana amani wala furaha..
Katika mulimwengu wa sasa ambapo tuna mambo mengi ya kuchagua, ni vizuri kuwa na maamuzi mazuri na si lazima yawe mazuri sana. Kwa maana hiyo ni kwamba, lengo si kufanya mambo kwa usahihi sana bali kawaida ili kupunguza kuchanganyikiwa pale malengo yako yatakapokuwa hayakutimizwa.
Jizoeshe kufanya maamuzi kwa haraka hasa maamuzi yanayohusu mambo madogomadogo na katika ununuaji wa vitu vidogovidogo ambavyo vinatakiwa kununuliwa mara kwa mara. Jenge kujiamini. Kataa kutumia muda mwingi ukisononekea maamuzi mabaya uliokwishayafanya.
Badala yake jifunze kutokana na makosa uliyokwisha kufanya ili kuweza kufanya vizuri baadae.
Pambana na hisia zinazokzonga baada ya maamuzi na matokeo mabaya uliyopata kwa kuona kwamba bora kufanya maamuzi mabaya kuliko kutokufanya maamuzi kabisa.
Ni hei kukosea katika maamuzi kuliko kukwepa kufanya maamuzi. Jitahidi ufanyapo mikataba iwe ni ilea ambayo hutataka kuibadilisha kiholela na hasa ambayo ni maamuzi makubwa yamefanyika. Kuna maelezo kwamba, mababu zetu waliishi umri mrefu, pamoja na mengine ni kutokanana hali hii ya kukosa vingi vya kuchagua. Ingawa hawakupenda hali hii, iliwasaidia sana kuwatoa katka hofu zisizo za lazima.
Sisi tunakabiliwa na hofu na mashaka yasiyo na mwisho kwa sababu tuna vingi vya kuchagua na kila tunapochagua tunajikuta tukitamani kama tungefanya uchaguzi tofauti.
Ni kweli tunao uchaguzi mwingi ambao pia una maana ya vifo vingi.
Ndio mkuu nashukuru kwa utambuzi hoja wako huu, na naupamba kwa usemi usemao ukichagua sana Nazi utaishia koroma!
ReplyDelete