0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Feb 9, 2011

AJALI KOROGWEAjali hii niliyoishuhudia nikitokea Arusha ilihusisha gari aina ya Scania yenye tank la kubeba mafuta, ilitokea jana majira ya Mchana nje kidogo ya mji wa Korogwe karibu kabisa na Daraja, kama kawaida wananchi wa eneo hilo walikimbilia eneo la tukio wakiwa na ndoo wakitarajia mafuta yatamwagika wajichotee lakini kwa bahati mbaya kwao hilo halikutokea. Kama mnavyoona katika picha hizo wananchi hao walilisogelea gari hilo kwa karibu sana kwa tamaa ya kuchota mafuta na yuko mmoja alitaka kulitoboa lakini Polisi waliwahi katika eneo hilo. Inasikitisha kuona watu wakihatarisha maisha yao kiasi hiki wakati wanajua kuwa kuna uwezekano wa gari hilo kulipuka na hiyo imeshatokea mara nyingi lakini sijui kwa nini watu hawaelewi?

2 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Duh! inaonekana ajali ilikuwa kubwa lakini hata hivyo watu wanajali kupata mafuta tu. Na kama ilivyo wanajali maisha yao tu sio ya wengine. Pole kwa ajali natumaini hakukuwa na waliojeruihiwa wengi.

    ReplyDelete
  2. Umasikini huu, umasikini huu...utaisha lini. Watu kumetokea ajali , lakini kinachowazwa sio kusaidia ni jinsi gani nitapata chochote kwenye hiyo ajali hata ikibidi kuua...utu umeisha umbebakia unyama!

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi