0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Dec 10, 2010

ABRAHAM, MWANABLOG MTARAJIWA ATIMIZA MIAKA MITATU LEO!
Mtoto Abraham S Kaluse ambaye ametimiza miaka mitatu leo akiwa katika mionekano tofauti.

4 comments:
Andika Maoni Maoni
 1. Hongera Abraham, Mungu azidi kuwa nawe daima na daima, amen.

  Nje ya topiki, nimependa sana mazingira ya nyumba yenu.

  ReplyDelete
 2. kabla sijampongeza Abraham, namshukuru sana sana mno (kama kuna msamiati mwingine niongezeeni tafadhali) kwa kumfanya mwana mpotevu, blog aliyekupa kisogo kublog kwa miezi mitatu sasa kurejea ulingoni...siamini atapotea tena.....

  kisha.....

  Hongera sana mtoto mzuri Abraham kwa kufikisha umri huo. Najivunia kukufahamu kama mtoto mpole, mwenye adabu, mkarimu, msikivu na mwepesi wa kujifunza mema. Nakutakia kila la kheri, afya njema, furaha tele ili ukuwe uje kuwa kaka bora, mjomba bora, baba bora, rafiki bora, mlezi bora, mwandishi bora, na zaidi, kiongozi bora.

  kwako Shaban na mama Abraham....

  nakutakieni furaha daima katika ndoa yenu ili mumlee mtoto katika maadili na upendo aishi akiamini maisha ni furaha, upendo, kuwajibika na uaminifu......

  kwa Mwenyezi Mungu.....

  ninamwomba amsimamie vema Abraham katika makuzi yake na maisha yake kwa ujumla.....

  Amina.

  ReplyDelete
 3. HONGERA SANA MTOTO, NA twaweza kusema mtoto wa nyoka ni nyoka, na maji hufuata mkono, au sio.
  Kama mtarajiwa, tunaona uhudi zako, kama picha ionyeshavyo, kuwa naye hachezi mbali na ulipo, hapo unamfundisha kivitendo, na watoto wengi sana huiga kile wzazi wanachopendeela kukifanya.
  Mungu amjalie ashike hatamu zako, na ampe afya na baraka. Nanyi wazazi twawaombea heri na baraka katika ulezi na majukumu mengine
  Ni hayo tu kwa sasa

  ReplyDelete
 4. Hapa ni shangazi wako wa hiari Abraham. Nakutakia kila la kheri kwa siku hii ya kuzaliwa , hakika siku zinaenda kasi mara hii una miaka mitatu. Hongera sana pia wazazi kwa kukulea na kuwa mtoto mwema, msikivu/mwelevu na uendelee kuwa hivi. Hongera.

  ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi