0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Apr 1, 2010

MALAIKA WA KIFO!

Muuaji Orville Lynn Majors

Kila mgonjwa aliyewahi kukutana na muuguzi Orville Lynn Majors, alimuona kama nesi mpole na mwenye upendo wa hali ya juu na anaejua kuwahudumia wagonjwa kwa uadilifu mkubwa. Lakini katika hali kushangaza ikawa kila mgonjwa anaehudumiwa na muuguzi huyu katika Hospitali hiyo ya Vermillion County iliyopo katika jimbo la Indiana akawa anakufa katika mazingira ya kutatanisha.

Mpaka kufikia mwaka 1995 takwimu za idadi ya vifo vilivyokuwa vikitokea katika Hospitali hiyo iliyokuwa na idadi ya vitanda 60 tu vya kulaza wagonjwa ilikuwa ni ya kutisha na hata wafanyakazi wa hospitali hiyo walipoulizwa hawakuwa na majibu ya kuridhisha. Mnamo March 7 1995 uongozi wa hospitali ya Vermillion ulikuwa na wakati mgumu wa kujibu tuhuma hizo kwani kulikuwa na uwezekano wa hospitali hiyo kushitakiwa kwa uzembe wa kusababisha idadi kubwa ya vifo katika hospitali hiyo ambapo watu walihisi kwamba huenda kuna mchezo mchafu unaochezwa na baadhi ya wauguzi wa hospitali hiyo ambao unahitaji kufanyiwa uchunguzi wa kipolisi.

Uongozi wa hospitali hiyo ulitoa ripoti yao kwa askari wa upelelezi ambao ulikuwa ukionyesha kwamba vifo vilivyokuwa vikitokea kwenye chumba maalum cha wagonjwa mahututi vilikuwa vimeongezeka ghafla kutoka wastani wa asilimia 20 kwa mwaka hadi asilimia zaidi ya 100, kwani watu wapatao 147 walikuwa wamepoteza maisha katika chumba hicho kuanzia mwaka 1993. Polisi walianza kuangalia rekodi za utendaji kazi wa kila mfanyakazi wa hospitali hiyo.

Katika ripoti karibu zote za watu waliopoteza maisha katika hospitali hiyo jina la Orville Lynn Majors lilitajwa kama muuguzi aliyekuwa zamu katika chumba cha wagonjwa mahututi wakati kifo kinatokea. Polisi pia waligundua kwamba vifo hivyo vya mfululizo vilianza wiki chache tangu Orville aanze kazi katika hospitali hiyo. Kwa mujibu wa rekodi zilizopatikana katika hospitali hiyo ilionyesha kuwa Orville alikuwa zamu wakati vifo vya wagonjwa 130 kati ya vifo 147 vilivyotokea katika hospitali hiyo.

Ripoti hiyo ilikuwa ni tofauti na muonekano na tabia aliyokuwa nayo, kwani alikuwa akijulikana na uongozi wa hospitali hiyo pamoja na wagonjwa waliowahi kutumia hospitali hiyo kama muuguzi mwenye kujituma na mwenye upendo kwa wagonjwa. Baada Polisi kutilia mashaka utendaji wake, mnamo March 9 1995 ilibidi uongozi wa hospitali hiyo umsimamishe kazi ili polisi wapate fursa ya kufanya upelelezi wao kwa ufanisi.

Kwa mshangao na wafanyakazi wengi wa hospitali hiyo kwani wengi hawakuamini kama Orville angeweza kuwa mtu wa kwanza kutuhumiwa kwa kusababisha vifo vya wagonjwa katika hospitali ile. Hata hivyo kitendo cha Orville kusimamishwa kilikuja kuibua makosa mengi ambayo aliyafanya bila ya kujulikana wakati akiwa kazini.

Katika uchunguzi uliofanywa hospitalini pale ilikuja kugundulika kuwa Orvile alikuwa akifanya kazi za kitabibu kwa wagonjwa wakati alikuwa hana ujuzi nazo, pia ilikuja kugundulika kuwa alikuwa akiwachoma wagonjwa sindano ambazo kitaalamu huchomwa na mtu maalum aliyesomea ujuzi huo. Kutokana na kugundulika kwa makosa hayo mnamo April 1995 Orville alifukuzwa kazi rasmi.

Msemaji wa Bodi ya wauguzi ya Jimbo la Indiana Gerorge Patton Jr. alimzungumzia Orville kama mtu hatari kwa wagonjwa. Kitendo cha Orville kusimamishwa kazi kilikuwa kimeitikisa taaluma ya uuguzi. lakini polisi walikuwa na mtihani mwingune kwani pamoja na kuamini kwamba Orville alihusika na mauaji ya wagonjwa zaidi ya 100 lakini walikuwa na wakati mgumu wa kupata ushahidi wa kumtia hatiani.

Katika ushahidi uliokusanywa katika ripoti ya vifo vingi vya ghafla vilivyotokea katika hospitali hiyo ulionyesha kwamba vilitokana na moyo kushindwa kufanya kazi ghafla au matatizo yatokanayo na mfumo wa kupumua. Wataalam walidai kwamba kama Orville atakuwa ndiye muuaji, basi atakuwa amewauwa kwa kuwachoma sindano yenye kemikali ya Potashiam Kloraid (Potassium Chloride) Ni kitu gani kinachosababisha kuwepo na ugumu kuthibitisha madai hayo?

Kwa kawaida sindano yenye kemikali ya Potashiamu Kloraidi hutumika kwa kuwauwa watu walihukumiwa kunyongwa, ambapo kwa upande wa Orville kulikuwa hakuna ushahidi wa kuthibitisha madai hayo. Kwa muda wa miezi 15 waliotumia wapelelezi wa polisi lakini bado walikuwa hajapata ushahidi wa kina wa kumfungulia Orville mashtaka.

Ingawa walikuwa wamepata hizo kemikali za potashiamu kloraidi nyumbani kwake lakini huo haukuwa ushahidi wa kuthibitisha madai yao. Pamoja na polisi wa upelelezi kuchukuwa miaka 3 katika upelelezi wao dhidi ya Orville ambao uliwagharimu walipa kodi wa jimbo la Indiana kiasi cha dola milioni moja na nusu lakini bado ushahidi wa kumtia orville hatiani ulikuwa ni wa kimazingira zaidi.

Kwani wapelelezi wa polisi waliamini kwamba, ikiwa ni kweli Orville alihusika na mauaji ya wagonjwa zaidi ya 130 katika kipindi cha miezi 32 aliyofanya kazi katika hospital hiyo, basi ni wazi kuwa hakuacha ushahidi wowote nyuma yake zaidi ya takwimu tu.

Hata hivyo bado polisi walikuwa na tegemeo jingine la ushahidi kutoka kwa mtaalamu kutoka jimbo la Washington ambao waliongozwa na mwanasayansi aliyejulikana kwa jina la StevenLamm.

Katika uchunguzi wao ambao uligharimu kiasi cha dola laki tatu, wataalamu hao walikiri kwamba kwanza kuna ukweli wa kimazingira wa kumuhusisha Orville na vifo vya wagonjwa 130 kati ya wagonjwa 147 waliopoteza maisha katika Hospitali hiyo, ambavyo vyote vilitokea Orville akiwa kazini.

Katika ripoti yao ilionyesha kwamba wagonjwa wote waliopoteza maisha katika Hospitali wakati Orville akiwa kazini walikuwa wakifa kila baada ya masaa 23 na dakika 1, isipokuwa mgonjwa mmoja ambae alifariki baada ya masaa 551 na dakika 6, ambapo Orville hakuwepo ikazini. Mmoja wa wauguzi wanaofanya kazi katika hospitali hiyo alidai kwamba hali ilikuwa mbaya sana kutokana na kushuhudia vifo vya wagonjwa kila Orville awapo kazini.

Muuguzi huyo alikiri kwamba kuna wakati walikuwa wakicheza kamari kwa kuwekeana dau juu ya mgonjwa gani atakufa pindi Orville atakapokuwa kazini, na mara zote mshindi alikuwa akipatikana na kujizolea kitita cha fedha. Pamoja na ushahidi huo ambao ulielemea zaidi kwenye minong’ono na maneno ya mitaani, lakini bado wapelelezi walikuwa na wakati mgumu wa kujenga ushahidi madhubuti wa kumtia Orville hatiani.

ITAENDELEA…………………

1 comment:
Andika Maoni Maoni

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi