0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Apr 4, 2010

MALAIKA WA KIFO! SEHEMU YA MWISHO


ILIPOISHIA.......

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya Orville kusomewa mashitaka, wakili huyo aliwaambia waandishi wa habari kwamba mteja wake amestushwa sana na mashtaka yale.
Wakili yule aliendelea kusema kwamba, anadhani kuwa baada ya miaka mitatu mingine huenda mtu mwingine akafunguliwa mashtaka yanayofanana na yale kwa sababu vifo vyote vilivyotokea katika Hospitali ya Vermillion County kwa jinsi ninavyofahamu vilikuwa ni vifo vywa kawaida kabisa. Siamini kabisa kama kuna mtu alihusika na vifo vile.

ENDELEA NA SIMULIZI HII………………

Akiendelea kufafanua kauli yake wakili yule alisema kwamba kilichotokea ni kuwa kulikuwa na wagonjwa ambao wengi walikuwa wazee ambao walifikishwa katika hospitali hiyo kwa matibabu na kama inavyojulikana kuwa mji wa Vermillion County ni mji wa pili kwa ongezeko la watu katika jimbo la Indiana hivyo hospitali hiyo ilishuhudia ongezeko hilo la wagonjwa wengi wazee huku kukiwa hakuna maandalizi yoyote ya kuongeza wataalamu.
Wakili huyo aliendelea kubainisha kwamba kimsingi Hospitali ya Vermillion County haina wataalam wa kutosha ambao wangekwenda sambamba na ongezeko hilo la wagonjwa, ambapo hasa wengi walikuwa ni wazee, na kama wangekuwepo vifo hivyo visingetokea.

Naye mwendesha mashtaka wa mahakama hiyo aliyejulikana kwa jina la Mark Greenwall akionekana kujiamini aliwaambia waandishi wa habari kuwa anayo kesi nzito dhidi ya Orville na kesi hiyo inategemea zaidi ushahidi kutoka kwenye jopo lake la wapelelezi wakishirikiana na wataalamu wa kitabibu ambao ndio waliopewa jukumu la kuchunguza vifo 160 vilivyotokea katika hospitali hiyo kati ya mwaka 1993 na mwaka 1995, ambapo asilimia 50 ya vifo hivyo vilionekana kutokea katika mazingira ya kutatanisha.


Akizungumzia kitendo cha Orville kufunguliwa mashtaka ya mauaji ya watu 6 tu badala ya watu 160 ambao ndio aliokuwa akituhumiwa kuwauwa awali, Greenwall alisema kwamba kitendo cha Orville kufunguliwa mashtaka ya watu sita tu hakimaanishi kuwa kulikuwa na vifo vya watu sita tu, bali walichukuwa kesi za watu sita ambazo walikuwa na uhakika wa kupata ushahidi wa kutosha ambao ungemtia Orville hatiani bila ya kutia shaka yoyote.
Baada ya Orville kusomewa mashtaka, nje ya mahakama ile ambayo ilifurika umati wa watu ambao walikuwa wakiifuatilia kesi ile ambayo ilivuta hisia za watu wengi, miongoni mwao wapo waliokuwa wakimtetea Orville.

Akizungumza nje ya mahakama mdogo wake na Orville aitwae Debbie McClelland alisema kuwa kaka yake hana hatia kwa sababu hakuhusika na mauaji yale.
Kwa maneno yake mwenyewe Debbie alisema “tangu uchunguzi wa kesi hii uanze na mpaka kufikia sasa hivi ambapo kesi ipo mahakamani wazazi wetu wamekuwa na wakati mgumu sana na hii imevuruga kwa kiasi kikubwa maisha yao lakini mungu anatupa nguvu na kuendelea na maisha yetu kama kawaida, japokuwa tunatiwa moyo na majirani zetu lakini hali si ya kuridhisha pale nyumbani”

Nae mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina la Ida Harris ambae aliwahi kuwa muhudumu wa wazazi wa Orville pale nyumbani kwao wakati Fulani alisema kuwa kwa jinsi anavyomfahamu Orville haamini kwamba alihusika na mauaji yale, na anaona kabisa kwamba hawamtendei haki. Kesi ile ambayo iliahirishwa kwa zaidi ya mwaka mmoja hadi mwaka 1999, ilipangwa kuhamishiwa katika mji mwingine uitwao Brazil ambao upo maili kadhaa kutoka katika mji wa Vermillion kusini mwa mji mwingine wa Terre Haute, na hii ilitokana na kwamba mji huo ndipo idadi ya watu waliopoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha katika Hospitali ya Vermillion County ni kubwa.

Mashahidi wapatao 79 walijitokeza kutoa ushahidi wao ambapo wengi walikiri kumuona Orville akiwachoma sindano ambazo zilipelekea vifo vya wapendwa wao, ambapo kimsingi alikuwa haruhusiwi kuwachoma wagonjwa sindano hizo. Mnamo October 17, 1999 Orville alipatikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya watu sita na hivyo kuhukumiwa kifungo cha miaka 360 gerezani.

*****************MWISHO*******************

No comments:
Andika Maoni Maoni

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi