0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Apr 23, 2010

KISA CHA MWANAMKE WA ZIWANI

Carol Park
Gordons Park

Mnamo August 12, 1997 majira ya Mchana Katika wilaya ya Lake nchini uingereza kundi la wazamiaji kutoka mji mdogo wa Kendal waliamua kwenda kufanya mazoezi katika mto ulioko jirani wa Caniston.

Mmoja wa wazamiaji wale alifanikiwa kwenda kina kirefu zaidi ya mita 21 na ndipo alipohisi harufu kali ya kitu kinachonuka, alipozidi kusogelea eneo lile aligundua ni mabaki ya mwili wa mwanadamu uliofungwa kwenye mfuko wa plastiki.

Mzamiaji yule pamoja na wenzie ilibidi wasitishe mazoezi yao na kuwafahamisha Polisi.
Baadae mchana huo huo kikosi cha Polisi wazamiaji walifika kwenye eneo la tukio na kufanikiwa kuyatoa mabaki ya mwili ule.

Walipofungua ule mfuko wa plastiki walikuta mabaki ya mwili wa mwanamke ambae alikuwa akionekana dhahiri kwamba alikuwa na umri wa chini ya miaka 30 na ilionekana dhahiri kwamba alikaa ndani ya maji kwa miaka mingi sana kwani hata mavazi aliyokuwa ameyovaa yalionyesha hivyo.

Alikuwa amevaa vazi la usiku la miaka ya 70 na alionekana kwamba alikuwa amepigwa na kitu kizito kichwani na kisha kutupwa mtoni. Ndani ya mfuko wa plastiki uliokuwa umehifadhi ule mwili kulikutwa pia vipande vizito vya vyuma ambavyo viliwekwa kwa makusudi na muuaji ili ule mwili uzame moja kwa moja bila kuibuka.

Kwa kuanzia askari wa upepelezi walianza kuchunguza kesi zaidi ya 50 za watu walioripotiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha kwenye miaka ya 70. Ukweli ni kwamba hata vazi alilokutwa nalo Carol lilirahisisha sana kutambuliwa kwake kwani haikuwachukuwa muda mrefu Polisi kutangaza kuhusu kutambuliwa kwa mwili ule ambao ulikwisha harbika vibaya kutokana na kukaa katika maji kwa takribani miaka 21.

Mnamo August 21, 1997 ikiwa ni siku 9 baada ya kugundulika kwa ule mwili, Polisi wa upelelezi walitangaza rasmi kwamba ule mwili ulikuwa ni wa Carol Park mama wa watoto watatu na mwalimu wa shule ya msingi aliyekuwa na miaka 30 wakati huo alipotoweka.

Taarifa za Kipolisi zilionyesha kwamba Carol alitoweka nyumbani kwake mnamo July, 1976.
Inasemekana kwamba mnamo tarehe hiyo Familia yao ilikubalina wafanye safari ya kwenda katika mji wa Blackpool ili kupunga upepo kwenye Hoteli za ufukweni lakini Carol alisitisha uamuzi wa kwenda huko kwa madai kwamba anajisikia vibaya, hivyo mumewe Gordon Park ambae pia ni mwalimu pamoja na watoto wao wakaamua kwenda bila ya mama yao.
Lakini waliporudi usiku hakumkuta mkewe, na ilimchukuwa wiki 6 kuripoti kutoweka kwa mkewe polisi.

Alipoulizwa sababu ya kuchelewa kutoa taarifa wakati huo aliwaambia Polisi kwamba katika miaka ya karibuni mkewe alikuwa na akitoka nje ya ndoa na wanaume tofauti tofauti tabia ya kutoweka pale nyumbani na kurejea na akiwa salama. Utokana na tabia hiyo mume huyo alidai kuwa hata maisha yao ya ndoa yalishaanza kuyumba.

Polisi walikuja kugundua baadae kupitia kwa majirani kwamba Maisha ya ndoa kati ya Gordon na mkewe Carol yalikuwa si mazuri na yaliyojaa misukosuko mingi. Majirani waliwaeleza Polisi kwamba Carol aliwahi kuwaambia kuwa alikuwa na wanaume wawili waliokuwa wakiishi katika maeneo tofauti na alikuwa akienda kuishi nao katika vipindi tofauti. Taarifa zaidi zilibainisha kwamba kuna wakati aliwahi kutoweka nyumbani kwa miezi 18.

Pia majirani hao walijenga hisia kwamba huenda Carol alikwepa safari ya kwenda Blackpool akichukulia kama ni nafasi muhimu kwake atakayoitumia ili kutoroka pale nyumbani kwake na kwenda kuanza maisha mapya mahali pengine na mwanaume mwingine. Hata hivyo kaka yake Carol aitwae Ivor Price alidai kwamba ni jambo lisiloingia akilini kuamini kwamba dada yake anaweza kuwatelekeza watoto wake watatu na kwenda kusikojulikana bila mawasiliano nao kwa kipindi chote alichopotea kwani hata kipindi cha nyuma alichowahi kutoweka alikuwa akiwasiliana nao. Pamoja na maelezo yake, Polisi hawakuonekana kuyatilia maanani kwani waliona kwamba hakuna haja sana ya kushughulika na kesi ya mtu ambae alikuwa na tabia ya kutoweka nyumbani kwake mara kwa mara.

Hata hivyo Polisi hawakuipuuza sana ile kesi, kwani waliona ni busara kuichunguza ile kesi kwa makini zaidi, hasa ikizingatiwa kwamba tukio lenyewe lilitokea zaidi ya miongo miwili iliyopita.
Ili kuthibitisha hayo mwendesha mashtaka wa serikali(Detective Superintendent) aliyejulikana kwa jina la Ian Douglas ambae aliipa kesi hii jina la “mwanamke wa ziwani”(Lady of the Lake) aliwaambia waandishi wa habari kwamba Polisi wanaishughulikia kesi ya Carol kama ya mauaji ya kukusudia, kutokana na mazingira ya jinsi mwili ulivyopatikana.

Pia Msemaji huyo alitanabahisha kwamba Polisi watawahoji ndugu na watu wa karibu wa Carol akiwemo Aliyekuwa mumewe Gordon Park ambae alikuwa ameshastaafu kazi yake ya ualimu, na kwa wakati ule ambao mwili wa Carol umepatikana alikuwa ameenda Likizo nchini Ufaransa akiwa na mke wake wa tatu aitwai Jenny.

Alipoulizwa na waandishi wa habari kama kuna uwezekano wa Gordon Park kuchukuliwa kama nimtuhumiwa wa mauaji hayo. Msemaji huyo alisema kwamba haingekuwa vyema kwa Polisi kumtuhumu moja kwa moja Gordon, na hawezi kuwaomba Polisi wa nchini Ufaransa wamkamate kwa sababu kuna mambo mengi ya kuangaliwa kabla ya kumtia mbaroni.

Kwa maneno yake mwenyewe Douglas alisema “Bado tuna jukumu la kuwatafuta na kuwahoji watu waliokuwa wakiishi jirani na familia ya Gordon Park wakati Carol alipotoweka, na pia ndugu wa karibu wa familia husika pamoja na marafiki, ni jambo ambalo linahitaji muda na umakini wa hali ya juu hasa ikizingatiwa kwamba ni siku nyingi tangu tukio hili lilipotokea, na ikumbukwe kwamba tunazungumzia tukio lililotokea miaka 21 iliyopita, ni vigumu watu kuwa na kumbukumbu za tukio zima”

Alipoulizwa kama Polisi watakwenda kuchunguza nyumba ambayo familia ya Gordon Park ilikuwa ikiishi. Msemaji huyo alisema kwamba hilo linawezekana kwa sababu teknolojia imekuwa kubwa katika miaka ya karibuni na kuna uwezekano wa mtuhumiwa kukamatwa.
Siku mbili baada ya Msemaji wa Polisi Ian Douglas kutoa taarifa kwa waandishi wa habari juu muenendo wa upelelezi wa kesi ya Carol Park.

Msemaji huyo pamoja na timu ya wataalamu wa kuchunguza mazingira ya eneo la tukio walikwenda kuchunguza nyumba anayoishi Gordon Park iliyoko katika eneo la Borrow-in-Furness. Pia Timu hiyo ilikwenda kuchunguza Boti ya uvuvi(Yatch) ya Gordon ambayo ilikuwa imeegeshwa kando ya ziwa Caniston. Timu hiyo iliondoka na vitu kadhaa kwa ajili ya kuvifanyia uchunguzi.

Pamoja na kuondoka na ushahidi huo lakini Douglas alionyesha wasiwasi na muonendo mzima wa maisha ya Gordon. Kwani Polisi walijenga wasiwasi kutokana na kitendo cha Gordon kuuza Boti yake ya uvuvi ya awali ambayo aliipa jina la “Lady J” muda mfupi tu baada ya Carol kutoweka.

Wakati Polisi wakiendelea kumsubiri Gordon arejee kutoka Ufaransa alipokwenda kwa likizo, waliona ni vyema wawahoji watoto wao watatu ambao ni Jeremy aliyekuwa na miaka 27 lakini wakati mama yake anatoweka alikuwa na umri wa miaka 6, mwingine ni Rachel aliyekuwa na miaka 26 na Vanessa aliyekuwa na miaka 29 wakati mwili wa mama yao ulipopatikana.
Katika mahojiano hayo, Polisi waligundua kwamba Vanessa hakuwa mtoto wa Gordon wa kuzaa, bali alikuwa ni binti wa dada yake Carol aitwae Christina ambae aliuwawa na bwana ake
mnamo mwaka 1969, ambapo Carol na Gordon waliamua kumuasili na kumfanya binti yao.
Hata hivyo Polisi walikanusha kuwepo kwa mahusiano kati ya kesi hizo mbili.ITAENDELEA............

2 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Duh! inasikitisha lakini kweli mume anaweza tu kuacha hayta kumtafuta mkewe hata kama ana mazoea ya kutoka nje? Ngoja nisiseme sana nasubiri muendelezo.....

    ReplyDelete
  2. Nasuburua kaka. Usichelewe vinginevo utapata shida....

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi