0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Apr 24, 2010

KISA CHA MWANAMKE WA ZIWANI-SEHEMU YA PILI

Gordond Park na CarolGordons Park na Mkewe Jenny aliyefunga naye ndoa baada ya Carol kutoweka

ILIPOISHIA……………..

Wakati Polisi wakiendelea kumsubiri Gordon arejee kutoka Ufaransa alipokwenda kwa likizo, waliona ni vyema wawahoji watoto wao watatu ambao ni Jeremy aliyekuwa na miaka 27 lakini wakati mama yake anatoweka alikuwa na umri wa miaka 6, mwingine ni Rachel aliyekuwa na miaka 26 na Vanessa aliyekuwa na miaka 29 wakati mwili wa mama yao ulipopatikana.
Katika mahojiano hayo, Polisi waligundua kwamba Vanessa hakuwa mototo wa Gordon wa kuzaa, bali alikuwa ni binti wa dada yake Carol aitwae Christina ambae aliuwawa na bwana ake mnamo mwaka 1969, ambapo Carol na Gordon waliamua kumuasili na kumfanya binti yao. Hata hivyo Polisi walikanusha kuwepo kwa mahusiano kati ya kesi hizo mbili.

ENDELEA KUSOMA HAPA……..

Ukweli ni kwamba Polisi hawakupata ushahidi wowote wa kumtia Gordon hatiani, kwani wale watoto wote watatu hawakuwa na kumbukumbu za matukio yote yaliyotokea kabla na baada ya mama yao kutoweka. Pia Polisi walitaka kutengeneza taarifa ya kumbukumbu (Profile) ya maisha ya Gordon Park na familia yake mpaka kufikia mwaka 1976.

Kazi hiyo ilikuwa ngumu kwa sababu watu waliotaka kuwahoji walikuwa aidha wamehamia katika maeneo ya mbali au wamefariki Dunia. Hata hivyo Polisi walifanikiwa kumpata mama mmoja aitwae Mary Robins aliyekuwa na umri wa miaka 61 ambae alikuwa akifanaya kazi ya uyaya kwenye familia ya Gordon Park. Mama huyo alikiri kuwa anakumbuka vizuri sana siku Carol aliyotoweka.

Akizidi kuwasimulia Polisi mama huyo alisema kwamba, hata yeye binafsi alijenga wasiwasi na namna carol alivyotoweka, na alihisi kwamba huenda kuna jambo ambalo si la kawaida limemtokea. Kwani pale mtaani kila mtu aliliona tukio la kutoweka kwa Carol kama kitu cha kushangaza, kwa mtu kuwatekeleza watoto wake ghafla kiasi kile na kutokomea kusikojulikana bila kuwasiliana na wanae kama alivyokuwa akifanya awali.

Mama Robinson aliendelea kuwaeleza Polisi kuwa, yeye alidhani labda ameamua kwenda kuanza maisha mapya huko nchi za ulaya kwa sababu hata hivyo alikuwa ni mwalimu mzuri hasa katika kufundisha lugha ya kiingereza. Mnamo August 24 1996, Gordon Park na mkewe Jenny walirejea nchini uingereza wakitokea nchini Ufaransa. Baada ya kufika nyumbani kwake katika eneo la Barrow-in-Furness ambapo alishusha mizigo kutoka kwenye gari, kisha akaondoka na kuelekea katika kituo cha Polisi kujisalimisha kwani pamoja na kwamba alikuwa nje ya Uingereza lakini alikuwa akiifuatilia ile habari ya kupatikana kwa mabaki ya mwili wa aliyekuwa mkewe kupitia vyombo vya habari na hasa Luninga.

Alipofika alishikiliwa kwa muda na kuhojiwa. Wanafamilia na marafiki pamoja na majirani zake walionyesha kusikitishwa kwao na kukamatwa kwa Gordon, akizungumzia tukio hilo mmoja wa marafiki zake aitwae Paul Shaw alisema kwamba alitokea kumfahamu Gordon kwa miaka mingi, kwani walisoma pamoja. Akizidi kumuelezea Paul kwa maneno yake mwenyewe alisema “Ni mtu anaejiheshimu, muungwana, anaeheshimu kila mtu, na katika kipindi alipokuwa mwalimu alikuwa akifanya kazi zake kwa uadilifu mkubwa na asiyependa kumkwaza mtu.

Pamoja na kuzungumziwa vizuri na marafiki na majirani zake lakini kulikuwa na wingu la mashaka lililotanda kwa upande wa familia ya Carol dhidi ya Gordon. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya misa ya kumuombea dada yake, kaka yake na Carol alisema “Bado nina mashaka dhidi yake lakini, mpaka hapo atakapokamatwa muuaji ndio atakuwa hana hatia”
Baada ya masaa 36 tangu Gordon kukamatwa, msemaji wa Polisi, akizungumza na waandishi wa habari waliokuwa wakisubiri nje aliwaambia kwamba Gordon Park amefunguliwa mashitaka ya kuhusika na mauaji ya Carol.

Kwa maneno yake mwenyewe msemaji huyo alisema “mnamo majira ya saa mbili na nusu usiku, kuna mtu amefunguliwa mashitaka ya kuhusika mauaji ya Carol Park, na kwa taarifa yenu mtu huyo atafikishwa katika mahakama ya Barrow siku inayofuata”

Baadae msemaji huyo alibainisha kwamba mtu huyo alikuwa ni Gordon Park.
Siku inayofuata Gordon alifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ambapo alikanusha kuhusika na mauaji hayo.


Kesi hiyo iliahirishwa mpaka wiki inayofuata ili kuruhusu upelelezi wa kesi hiyo ukamilike.

Baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, wakili wa Gordon aitwae Michael Graham aliiomba mahakama impe dhamana mteja wake, lakini mwendesha mashitaka katika kesi hiyo aliyejulikana kwa jina la Elizabeth Grant, alikataa Gordon kupewa dhamana na alitoa sababu zifuatazo, kwanza alidai kwamba mshitakiwa anaweza kuingilia upelelezi wa kesi hiyo, pili alisema kwamba kuna uwezekano wa wa Gordon kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na mwisho ni kutokana na usalama wake mwenyewe, Mama Grant alisema kwamba kuna uwezekano wa mtu yeyote ambae ameguswa na kifo cha Carol kujichukulia sheria mkononi na kumdhuru mshitakiwa, hivyo kutokana na kukataliwa Dhamana ilibidi aendelee kubakia Rumande.
Hata hivyo wiki mbili baadae Mwendesha mashtaka mama Grant alibatilisha uamuzi wake na kuruhusu Gordon kuachiwa kwa dhamana kwa masharti kwamba akakae kwa dada yake aishie katika mji wa Manchester, pia asalimishe Hati yake ya kusafiria na awe anaripoti Polisi kila siku na hakutakiwa kutoka nje ya mji wa Manchester.

Kesi yake iliahirishwa mpaka Januari 1998, ambapo iliwapa Polisi fursa ya miezi minne kufanya uchunguzi. Mnamo Januari 7, 1998 ikiwa imebaki wiki moja ili kesi ya Gordon kusikilizwa, msemaji wa Polisi aliwaambia waandishi wa habari kwamba polisi wameamua kutoendelea na kesi ya Gordon, kwa sababu ya kukosekana kwa ushahidi madhubuti wa kumtia mshitakiwa hatiani. Taarifa hiyo ilipokelewa kwa furaha sana na Gordon,na kusema wazi kwamba hana hatia ya kuhusika na mauaji ya Carol.

Akiongea na waandishi wa habari Gordon, kwa maneno yake mwenyewe alisema “Kwa jinsi Carol alivyonitendea katika ndoa yetu, watu wanadhani nilihusika na mauji yake, lakini ukweli ni kwamba sikuhusika na mauaji hayo, najua watu wanatilia mashaka kutokutiwa kwangu hatiani labda mpaka hapo mhusika wa mauaji hayo atapofikishwa mahakamani na kutiwa hatiani ndio watu wataamini kwamba sikuhusika na mauaji hayo”

Hata hivyo Mnamo Januari 2002, Polisi walianza upelelezi wa siri kwa kuunda timu ya watu sita wakiongozwa na Detective Chief Inspector Keith Churchman. Timu hiyo ilitangaza zawadi ya paundi 5000 kwa mtu yeyote atakaye jitokeza na kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa kuuaji na pia kituo kimoja cha Luninga nchini humo cha Channel 4 kuonesha kipindi maalumu (Documentary) kuhusina na kesi hiyo iliyopewa jina marufu la Lady in the Lake wakiifananisha na jina la kitabu cha riwaya kilichotungwa na mwandishi maarufu wa vitabu vya riwaya Raymond Chandler, ambapo kilikuwa na jina kama hilo.

Hatua hiyo ilizaa matunda baada ya watu wawili ambao waliwahi kufungwa katika jela ambayo Gordons Park aliwekwa rumande watu hao walitoa taarifa Polisi kuwa Park aliwahi kukiri kumuua mkewe kwa kumpiga na kitu kizito kichwani, watu hao waliokuja kujulikana kwa majina ya Michael Wainwright na mwenzie Glen Banks walimnukuu Park akiwaambia, “anastahili kufa, kwani nilimkuta chumbani akiwa na mwanaume mwingine” Ushahidi huo maarufu kama Jailhouse Snitch ndio uliopewa uzito zaidi na Polisi katika kumtia Gordons hatiani.
Walidai kuwa katika kipindi cha siku 14 alizokuwa amewekwa rumande akisubiri kusomewa masitaka ndipo alipokiri kuhusika na mauaji ya mkewe Carol Park.

Baada ya timu hiyo kukusanya ushahidi mnamo Novemba 2004, Gordons Park alifikishwa mahakamani kwa mara ya pili na kufunguliwa mashitaka ya kuhusika na mauaji ya mkewe Carol Park.
Wakati wa kuendeshwa kwa kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa na Mheshimiwa Jaji McCombe katika mahakama ya Manchester Crown, ilielezwa kwamba Park alimpiga mkewe Carol kichwani na kitu kizito wakiwa chumbani hapo mnamo julai 1976.
Baadae aliuhifadhi mwili huo kwenye Jokofu kabla ya kwenda kuutelekeza katika ziwa la Caniston wiki moja baadae.

Mahakama ilielezwa kwamba wanandoa hao hawakuwa na mahusiano mazuri katika maisha yao ya ndoa na kuwa walikuwa wakijihusisha na shajara za kubadilishana wanawake, maarufu kama ‘'wife-swapping' parties’ ambapo katika tukio moja la shajara ya chakula cha usiku Carol Park aliondoka na kwenda kulala na rafiki wa mumewe aitwae Colin Foster, huku Gordond Park akiondoka na mke wa Colin Foster kwenda kulala naye katika chumba kingine.
ITAENDELEA………….

No comments:
Andika Maoni Maoni

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi