0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Jan 6, 2009

KWA NINI WATU WAKUCHUKIE WEWE TU?

Kila mtu ni mbaya kwako, kila mtu anakuchukia, wewe tu, kila mtu hakutendei haki, kila mtu ana kasoro?
Je wewe ndivyo unavyoishi hivi? Kama jibu ni ndiyo au kama una mtu wako wa karibu ambaye anaishi katika mtindo huu wa maisha, unapaswa kujua kwamba, una mtu ambaye ana matatizo makubwa.
Mtu yeyota ambaye anapenda kusema kwamba, kila mtu anamchukia au kila mtu hamwelewi, basi jua kwamba huyo ni mtu ambaye kimsingi ana matatizo makubwa sana.
Kwa nini?
Haiwezekani kila mtu akawa kama mwingine, yaani akikuchukia huyu na yule ni lazima atakuchukia, ni lazima hatakutendea haki na mengine ya aina hiyo.
Kwa nini sasa wote wawe na tabia za aina moja, yaani wafikie kukuchukia?
Kwa kuwa watu hawafanani kitabia, kimwenendo na kimtazamo, ni wazi ukiona wote wanakuchukia wewe, tatizo haliko kwao, kwa sababu hawawezi wote kuwa na mkabala wa aina moja. Ina maana kwamba wewe ndiye ambaye hujipendi na kutojipenda kwakokunaonekana kwa watu hao.

Tuanposhindwa kujipenda, hasira dhidi yetu huwa tunazitolea kwa watu waliotuzunguka.
Kwa hiyo kama unahisi kwamba watu wanakuchukia, jitahidi kujiuliza kuhusu jambo hilo. Ni wazi haliwezi kuwa jambo la kweli hata kidogo.
Kama ni kuchukiwa, hivi inawezekana ukachukiwa na kila mtu kweli?
Ukichunguza ni wazi utagundua kwamba wenye tatizo sio hao watu.
Mwenye tatizo ni wewe na watu hao ni kioo chako kwa tabia yako.

Kama kila unakopita, iwe ni kazini au popote unajikuta ukiondoka umeacha watu wengi wakiwa wanakuchukia badala ya kukupenda, ujue kwamba wewe ndie mwenye tatizo, wewe ndio mwenye kasoro. Haiwezekani watu wakae kikao cha kukuchukia, bali watu wanaweza kukerwa na kutojiamini kwako au vitendo vyakohadi ikaonekana kama wamekula njama kukuchukia.

Kwa tabia zako, wanajikuta wakikujadili na kuambiana ‘humjui, ndivyo alivyo huyo’ Basi wanakuwa wameunda aina ya timu ya kukuchukia.
Kumbuka tu kwamba kila binadamu anapenda kuona anapendwa na kuheshimiwa, ingawa ni vitu visivyo na maana sana kwake.
Na kama unashindwa kumfanyia hivyo, anaingia mahali ambapo anaona huenda kuwa karibu na wewe ni hatari au haipendezi.
Kama hii ndio tabia yako, utamfanya kila mmoja ahisi kukereka kuwa karibu na wewe.

Hapondipo kuchukiwa kunapoanza.
Naomba nikwambie ukweli kwamba usije ukasema unachukiwa na watu fulani au kwamba watu fulani hawakupendi.
Ukisema hivyo, watu wanaojua tabia za binadamu, watajua kwamba wewe ni mkorofi sana. Ukiona mtu anasema jirani zake, watumishi wenzake, wanafunzi wenzake, ndugu zake, wanaye, wazazi wake au kundi fulani la watu wanamchukia, basi kwa kiwango kikubwa mtu huyo ni mkorofi.
Tafadhali kama imetokea ukahisi kwamba watu fulani wanakuchukia, au hawakupendi inabidi uanze kujiuliza bila kujipendelea kama wewe sio chanzo cha chuki hizo.
Acha kujipenda sana kwa hasara yako, kuwa wewe katika kiwango chako cha juu.



This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi