0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Jan 5, 2009

PABAYA LAKINI UNANG'ANG'ANIA!

Huwa najiuliza inakuwaje mtu analalamika kuhusu kazi yake, lakini bado anaendelea kuifanya. Unaweza kukuta mtu mwenye ujuzi na ambaye angepata kazi mahali pengine, lakini haondoki ila kulalamika ni kila siku akilaani kazi yake.

Unaweza kukuta mtu akiwa kwenye ndoa yenye kumuumiza, inayomzuia kufanya yale anayoyataka kwenye maisha yake, lakini badala ya kutoka kwenye ndoa hiyo yenye kumuumiza, anang’ang’ania huku akilalamikia ugumu na ubaya wa ndoa yake kila wakati. Nabaki najiuliza hivi ni kwa nini haondoki?

Unakuta mtu ana tabia fulani mbaya ambayo inamgharimu na anajua.
Ni tabia ambayo akiiacha anaweza lakini haiachi, na kila tabia hiyo ikimuumiza analalamika sana, lakini hayuko tayari kujitoa kwenye tabia hiyo. Hata akipewa msaada wa namna ya kujitoa, haufuati, hataki kuiacha ingawa inamuumiza.

Kwa mujibu wa wanasaikolojia, wanabainisha kwamba kwenye ubongo wa binadamu kuna sehemu iitwayo eneo la liwazo. Kupitia eneo hilo binadamu anajisikia ana usalama akiwa mahali au kwenye hali fulani aliyoizoea, na nje ya mahali au hali hiyo, binadamu anajihisi hayuko salama na wala hana amani.

Kwa binadamu walio wengi hata kama hawana amani moyoni wanonelea ni vyema kubaki mahali au katika hali fulani kwa sababu ya mazoea tu na kwa kuwa kwa kufanya hivyo wanajiona wako salama.
Ndio maana utakuta mtu ananyanyasika kazini au katika ndoa wakati umuhimu wa mambo hayo kwake haupo tena. Anachokiogopa hakijulikani!

Ukweli ni kwamba usalama wetu hautokani na msaada kutoka nje; usalama wetu unatakiwa utokane na sisi wenyewe.
Lakini kama nilivyosema mazoea yanamfanya mtu kuamini kwamba ni afadhali mateso ya mahali na hali aliyoizoea kuliko kuondoka wakati hajui ataangukia wapi.
Kwa bahati mabaya kama utang’ang’ania kubaki katika eneo lako la liwazo tu, kamwe hutaweza kuujua uwezo wako halisi uliojaaliwa nao au kukijua kipaji chako na kile uwezacho kukifanikisha kwa ufanisi mkubwa.

Ukiamua kwa makusudi kusogea mbele nje ya jamaa unaofahamiana nao; nje ya mazingira uliyoyazoea; na nje ya uzoefu wako, utakuwa umejiondoa katika eneo la liwazo kuelekea njia ya kukua.
Hii ni njia ya kupanua upeo wako. Mtu yeyote anayeanza kujifunza somo jipya shuleni; ajifunzaye lugha mpya; ajifunzaye mchezo mpya; au anayeanza kazi mpya anakuwa amejisogeza nje ya eneo la liwazo.

Hebu kaa utafakari kwa makini na ujiulize kama kuna haja kweli ya kuendelea na kazi hii, tabia hii au uhusiano huu.
Kama ukiona kuna haja ya kubadilika basi fanya uamuzi ulio sahihi,
maana hatima ya maisha yako iko mikononi mwako.

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi