0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Oct 14, 2009

NJIA YA MAISHA YAKO INAPOFUNGWA GHAFLA, SEHEMU YA MWISHO


Nilitembea asubuhi hiyo hadi hospitalini. Nilikwenda upande wa utawala na kuomba nimwone mama mkubwa. Ilikuwa ni vigumu sana kwa sababu ya watu ambao siku hizi wanitwa ‘wapambe’ Walikuwa wananizuia kwa maelezo kwamba mama mkubwa haonwi hovyo tu. Wakati tunabishana, kwani nami nilikuwa mkali nikiwa sijui nilitoa wapi nguvu hiyo ya kubishana, alitokea mamammoja mzungu aliuliz kulikoni, ambap walimweleza. Alinisogelea na kuniambia nimweleze shida yangu. Sikumwambia kuwa niliota kuhusu mama mkubwa bali nilimsimulia kwa kifupi madhila yangu na kumwambia nilikuwa nataka msaada w kusoma.Alinisikiliza sana na baadae alisemaangepanga nionane na huyo mama mkubwa. Saambili baadae nilikuwa ofisini kwa mama mkubwa. Alikuwa ni mama wa kizungu mtu mzima sana, lakini mjanja na msikivu sana. Nilizungumza naye kwa kirefu nikimweleza kia kitu. Alishindwa kuvumilia kwani alimwaga chozi.
Hapo nikafanikiwa kupata mfadhili wa kunisaidia kusoma. Nilikwenda shuleni na kuendelea na masomo. Nilikuwa ninaishi chini ya uangalizi wa mzee mmoja aliyekuwa anaitwa Alois, ambaye nimeambiw ameshafariki. Nilikuwa nikiishi kwenye chumba kimoja karibu na wodi ya wagonjwa hapo hospitalini. Wale ambao bado wapo hospitalini pale kama watumishi wanakumbuka, bila shaka. Nilimaliza darasa la saba na kuanguka kwa njia ambayo bado ni mshangao kwangu, hadi leo. Mama mkubwa alisikitika sana. Alimwomba Mzee Alois anitafutie shule nirudie. Nilirudia shule nyingine ya jirani. Mwaka mwaka uliofuatia nilifaulu peke yangu shuleni hapo.

Niliendelea na masomo. Bila shaka huhitaji kujua habari za shule ya sekondari. Lakini nilimaliza kidato cha sita mwaka 1987 na kumaliza masomo ya chuo kikuu nchini Uholanzi mwaka 1992. Nilirudi nchini na kuanza kazim kwenye kampuni9 moja ya madini kule shinyanga.

Mwaka 1994 nilikwenda Turiani, lengo likiw ni kwasalimu wote ambao nilikuw nafahamiana nao pamoja na dada yangu. Kwa kweli nilikuw nimemsamehe dada yangu yule kutoka ndani kabisa ya moyo wangu. Niliamua kwa makusudi niende nikashukie kwake. Nilipofika pale nyumbani kwake kulikuwa na mabadiliko sana. Ile nyumba ilikuwa imechakaa karibu kuanguka na palionyesha ukiwa wa wazi. Nilibisha hodi na mama mmoja mtu mzima sana alifumgua mlango kutokea ndania na kusimama mlangoni.
Kwa muda sikuweza kumjua. Lakini htimaye nilijua kuwa ni dada yangu.
‘Dada shikamoo, habari za siku’ nilimsalimia, lakini yule mama pale mlangoni alishindwa kujibu na kwa muda fulani ilionekana kama vile hakuwa anajua kinachoendelea. ‘Marahaba’ Alijibu, lakini ilikuwa ni kwa mazoea tu. ‘Nani mwenzangu, maana na huu uzee nao,’ Alisema akijichekesha.

‘Ni mimi Joseph, mdogo wako Joseph, mtoto wa mzee Richard Mbega wa Sindeni.’ Nilisema kwa kumfafanulia. Nilimwona dada akijishika vizuri pale mlangoni, lakini hakuweza. Alienda chini pole pole na kukaa kati kati ya mlango. Kw muda fulani nilijua alikuwa hajui alipo na kinachoendelea.

Wakati nikiwa najiuliza nifanye nini mama mwingine aliingia kutokea huko nyuma ya nyumba. Nilimtazama lakini sikumfahamu. Yeye alipiga kelele. ‘Kaka Jose jamani, kaka Jose,wala siamini…….’ Ilikuwa zamu yangu kushngaana laijua hilo kwani aliniambia, ‘Ni mimi mpwa wako Msekwa.’ Nilihisi kitu kikilipuka huko moyoni na matumbo yangu yalishikw na kubana ghafla.

Msekwa, alikuwa ni mama mzima, amechakaa na kuchoka kabisa. Kati yetu, yeye angeonekana kuwa mkubwa sana kuliko mimi. ‘Mungu wangu nashukuru nimekukuta…’
Halafu tulimsikia dada yangu akipiga yowe la kilio akidai kwamba hakuwa anajua alichokuwa anakifanya. Akiwa anaongea Kizigua alisema, ‘Mungu wangu mie nifanyeje sasa, naumbuka ….’ Nilimbembeleza, ingawa Msekw alisema nimwache augulie kwa sababu anastahili.

Baada ya kupumzika, nilijua kwamba wale wapwa zangu watatu wengine, aliyekuwa hai ni mmoja tu wa kike. Mmoja alifariki kwa kuajribu kutoa ujauzito na yule wa kiume alikuwa amefariki kwa kunywa sana pombe. Huyu mwingine alikuwa ameolewa na kuachwa na alikuwa eneo linaloitwa Dakawa. Nilikaa Turiani siku tatu na nilimwomba Msekwa tuondoke wote aje Dar ajifunze kozi yoyote. Hapa ninaposimulia makala haya, ni muuguzi siku nyingi. Dada yangu alikataa katakata kuja kwangu kwa aibu.

Inasikitisha hata hivyo kwamba, miezi mitatu tu tangu nilipofika kwake alifariki.Wanasema kila wakati alikuwa akijilaumu kwa yale aliyokuw amenitendeana alianza kujiambia kwamba, hana sababu ya kuishi kwa sababu hana maana. Naamini tunapanda nguvu hasi na huja kuturudia wenyewe.

Tulienda kuzika na kurejea Dar. Juhudi yangu yote ilikuwa ni kumpata yule shemeji yangu, iwe yuko hai au kaburi lake lilipo ili angalau nilijengee kama zawadi yangu kwake. Lakini juhudi zangu ziligonga ukuta kwa kadiri nilivyojitahidi. Nilikwenda hadi TPC, Moshi lakini sikumpata.

Hata hivyo hatimaye nilimpata katika mazingira ambayo sitaweza kuyasimulia hapa.
Naamini kwa simulizi hii, kuna jambo ambalo umejifunza. Katika maisha haya tunayoishi ni vyema tukawa tunapanda mbegu chanya na sio hasi, kwani kwa kupanda kwetu mbegu hasi, ndio hatimaye huturudia mara tatu zaidi ya kile tulichopanda na maumivu yake kihisia huwa ni makubwa sana. Lakini kama tukipanda mbegu chanya, hakika mavuno yake huwa makubwa kuliko kawaida, hebu jaribu uone.
Jambo lingine ni kusamehe, kusamehe ni muhimu kwetu, hata kama utakuwa umefanyiwa jambo baya kiasi gani. Kwa kusamehe kwetu tunakuwa tumejipa nafuu dhidi ya maumivu ya kihisia pale tukumbukapo juu ya yale tuliyotendewa na wenzetu. Zipo faida nyingi sana tunazopata pale tunaposamehe, lakini kubwa zaidi ni kule kumudu kusahau yale tuliyotendewa na hivyo kuwaza mambo mazuri ya yenye tija katika maisha yetu, badala ya kufikiria mabaya au kulipiza kisasi dhidi wale waliotutendea kinyume na matarajio yetu.
*******MWISHO********
Ndugu wasomaji, habari hii hainihusu mimi binafsi, bali iliwahi kuandikwa katika gazeti la jitambue. Hii ni habari ya kweli kabisa ambayo ilimpata msomaji wa gazeti la Jitambue, ambapo kwa hiyari yake aliamua kuiweka habari ya maisha yake katika gazeti hilo ili wasomaji wapate kujifunza kupitia uzoefu wake. Ukweli ni kwamba, katika gazeti la Jitambue tulikuwa tukiandika ushuhuda mbalimbali kutoka kwa wasomaji wetu ambao walijitolea kuandika historia za maisha yao. Na mimi nimeona sio vibaya nikizirejea baadhi ya stori hizo ili wasomaji wa kibaraza hiki nao waweze kujifunza.

3 comments:
Andika Maoni Maoni
 1. Nashukuru kaka Shabani, ni simulizi yenye kuelimisha kwa hakika.

  ReplyDelete
 2. Kweli hii simulizi....tena simulizi hasa inayoweza kukufanya ukasahau muda wa kwenda kazini, pole bwana mbega.

  ReplyDelete
 3. ahsante kwa simulizi leo nadhani sitalala niburudike na makala zako, kwa kweli nimelimiss gazeti la jitambue hivi bado lipo?
  leo katika kuhangaika nikapata hii blog thanks

  ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi