0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Oct 29, 2009

NIKAONA MAITI ZAO, SEHEMU YA MWISHO

ILIPOISHIA……………………..
Nilikata kipande kile cha gazeti la kingereza kilichokuwa na habari ile. Nilichukuwa kipande hico na kukiwekamkwenye nDiary yangu. Deni, Ningelipa vipideni la watu? Nilijikuta nikipiga magoti na kuomba. Mungu alipe uwezo wa kuja kulilipa deni la mtu yule mwema. Kwa njia yoyote. Mungu naomba uje uniwezeshe kulilipa kwa sura na namna ujuavyo wewe. Nataka kulilipa deni ili nami niwe nimemfanyia jambo marehemu , niliomba. Nilirejea Dar siku hiyo hiyo

ENDELEA…………….

Kwa sababu ya mambo mengi na hasa baada ya matokeo ya usaili ule kuwa mbaya kwangu, nilijikuta nikiwa na mambo mengi na kusahau haraka sana kuhusu mtu yule aliyenisaidia mbaye ni marehemu. Nilifanikiwea hata hivyo kupata nafasi ya kusoma Chuo cha Saruji na baasae chuo cha ufundi na hatimaye nilibahatika kwenda nchini Uingereza. Mwaka 1991 nilianza shughuli zangu.

Ilikuwa ni mwaka 1995 nikiwa ofisini kwangu pale lilipokuwa jengo Nasaco ambalo liliungua mwaka 1996, ambapo lilijengwa upya na kubadilishwa jina na kuitwa Water Front. Nikiwa nafanya kazi zangu niliambiwa na sekratari wangu kwamba kulikuwa na kijana aliyekuwa anaytaka kuniona. Nilimuuliza ni kijana gani, akasema hamjui. Nilimwambia amruhusu aingie. Kina huyo aliingia ofisini. Alikuwa ni kijana mdogo wa umri miaka kama 17 au 18 hivi, mweupe mrefu kidogo. Alikuwa amevaa bora liende , yaani hivyohovyo huku afya yake ikiwa hairidhishi sana.

Nilimkaribisha ilimradi basi tu, kwani niliona atanipotezea bure muda wangu. Nilazima niwe mkweli kwamba sikuwa mtu mwenye huruma sana na nilikuwa naamini sana katika watu wenye pesa au majina. Nilimuuliza “nikusaidie nini kijana na ukifanya haraka nitashukuru maana nina kikao baada ya muda mfupi”. Nilisema na sikuwa na kikao chochote , lakini nilitaka tu aondoke haraka.

“Samahani mzee, nilikuwa na shida…..nimefukuzwa shule na sina tena mtu wakunisaidia kwa sababu …..nime….niko ….kidato cha pili na hivyo tu natafuta tu kama atatokea mtu……..
Nilimkatisha “Sikiliza kijana. Kama huna jambo lingine la kusema, ni bora ukaniacha nifanye kazi. Hivi unafikiri kama nikiamua kumsaidia kila mtu aliyefukuzwa shule si nitarudimkwetu kwa miguu! Nenda Wizara ya Elimu waambie……Kwanza wazazi wako wanafanya kitu gani, kwa nini washindwe …..Kwa nini walikupeleka shule ya kulipia kama hawana uwezo, wanataka sifa?”

“Hapana wazazi wangu walikufa na ninasoma shule ya serikali . Nimekosa mahitaji ya msingi na nauli ya kwendea shule. Nasoma shule ya Kwiro, Morogoro. Shangazi ndiye anayenisomesha, naye ana kansa nahivi sasa hata kazi hafanyi….,” Alianza kulia.
Huruma Fulani ilinijia na nilijiambia, kama ni nauli tu na matumizi, kwa nini nisiwe mwema, angalau kwa mara moja tu. “Baba na mama walifariki lini?” Niliuliza nikijua kwamba, watakuwa wamekufa kwa ukimwi, maana kipindi kile ndipo fasheni ya ukimwi ilipoanza, ambapo kila anayekufa huhesabiwa kwamba kafa kwa ukimwi.

“Walikufa kwa ajali nilipokuwa mdogo sana, nilipokuwa na miaka mitatu. Ndio shangazi yangu akanichukua na kunilea hadi sasa anakufa kwa kansa.” Yule kijana lailia zaidi. Naomba nikwambie wewe msomaji unayesoma hapa kwamba, kuna nguvu fulani na sasa naamini kwamba ziko nyingi ambazo huwa zinaobgoza maisha yetu bila sisi kujua.

Kitu Fulani kilinipiga akinini paaa! Nilijikuta namuuliza yuel kijana “Kwa nini umeamua kuja kwangu, ni nani alikuelekeza hapa na wazazi wako walikufa mwaka gani na wapi?”
Yule kijana alisema, “Nimeona nijaribu tu kwa mtu yeyote ambaye anaweza kunisaidia, na ndio nimejikuta nikiingia hapa, sijui……..sikutumwa na mtu. Wazazi wangu walikufa mwaka 1979 huko Same na mimi wanasema nilikuwa kwenye ajali, nikaokoka. Niliumia tu hapa. Alishika kwenye kovu juu ya paji lake la uso.

Nilihisi kitu fulani kikipanda tumboni na kuja kifuani halafi niliona kama vile nimebanwa na kushindwa kupumua. “Baba yako alikuwa anaitwa nani?” “Alikuwa anaitwa Siame….Cosmas Siame….” Niliinuka ghafla hadi yule kijana laishtuka . Nilikwenda kwenye kabati langu mle ofisini na kuchakura kwenye droo moja na kutoka na diary. Mikono ikinitetemeka, nilitoa kipande cha gazeti ndani ya diary hiyo, nilichokuwa nimekihifadhi.

“Ndio alikuwa anaitwa Cosmas Siame. Huyu ni mtoto wake, ni yule mtomto aliyenusurika.” Nilinong’ona. Nilijikuta nikipiga magoti na kusali. “Mungu, wewe ni mweza na hakuna kinachokushinda. Nimeamini baba kwamba kila jema tunalofanya ni akiba yetu ya kesho na kesho hiyo huanzia hapa duniani.” Halafu nillinyamaza na kulia sana. Nililia kwa furaha na ugundiuzi wa nguvu zinazomgusa binadamu kwa kila nalofanya.

Nilisimama nikiwa nimesawajika kabisa. Nilihisi kuwa mtu mwingine kabisa. Nilimfuata yule kijana na kumkumbatia huku nikiwa bado ninalia. “Mimi ni baba yako mdogo, ndiye nitakyekulea sasa. Ni zamu yangu sasa kukulea hadi mwisho” Naye alilia bila kujua sababu na alikuwa amechanganyikiwa kabisa. Nilirudi kwenye kiti na kumsimulia kilichotokea miaka 17 iliyopita.

Tuliondoka hapo na kwenda kumwona shangazi yake Ubungo, eneo la maziwa ambako alikuwa ampapanga chumba. Kutokana na hali yake nilimhamishia kwangu, baada ya kumsimulia kilichotokea. Huyo dada yake Cosmas alifurahi sana hadi akashindwa kuzungumza kwa saa nzima. Alifariki hata hivyo mwaka mmoja baadae, lakini akiwa ameridhika sana.

Kijana Siame alisona na kumaliza Chuo Kikuu na hivi sasa yuko nchini Australia anakofanya kazi. Ukweli ni kwamba ni mwanangu kabisa sasa. Naamini huko waliko Mbinguni wazazi wake wanafurahia kile walichokipanda miaka mingisana nyuma. Lakini nami najiuliza bado. Ilikuwaje Cosmas akanipa msaada ule? Halafu najiuliza ni kitu gani kilimvuta mwanae Siame hadi ofisini kwanguakizipita ofisi nyingine zote? Nataka nikuambie, usiwe mbishi sana bila sababu, kuna nguvu za ziada zinazoongoza matokeo maishani mwetu…………
*************MWISHO********************
Habari hii iliwahi kuandikwa katika gazeti la jitambue.

4 comments:
Andika Maoni Maoni
 1. Hongera kaka hadithi ni nzuri,insikitisha na inauzito wa ajabu.ahsante kwa kuimalizia.nasubiri nyengine naomba usichelewe.

  shukran.

  ReplyDelete
 2. mmh leo nami nimeona nguvu fulani nilikuwa nasaka gazeti la jitambue mwaka jana sikulipata na sikujua kulikoni hadi leo nilipoifuma hii blog hongera sana kaluse napenda nakala zako

  ReplyDelete
 3. Ni uzoefu mkubwa sana wenye fundisho kubwa kuhusu nguvu tunazozalisha na kupokezana.

  ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi