0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Oct 18, 2009

KINDUMBWENDUMBWE CHA MAISHA!!! SEHEMU YA MWISHO.....

Nilianza kuipata picha na niliojua kwamba yule mke wa mwenyeji wangu hakuwa akitaka yule binti kuishi nao, kwa sababu zake. Alikuwa akifanya mambo na kumsingizia yule binti. Nilijiambia kwamba siku ya kuondoka pale ningemambia yule jamaa kuhusu ile redio. Lakini ingesaidia chochote?

Kesho yake jumapili nyumba nzima ilijianda kwenda kanisani, isipokuwa yule binti ambaye niliambiwa kwamba anaitwa Patience. Huyu aliachwa kwa ajili yakupika chakula cha familia. Niliona bila shaka ule ungekuwa muda mzuri kwangu kuzungumza na binti yule. Walipoondoka wote nilimfuata Patience jikoni na kumwomba nimsumbue wakati anapika kwa kuzungumza naye.Alisema wala simsumbui. “Nitashukuru maan sina mtu ninayezungumza naye humu. Wote wananidharau hadi huyu dada anayesaidia kazi” Alisema.

Nilimwambia ninaelewa, nimeona na nilimpa pole. Nilimuuliza kama ni kweli anaibana ni mbeya na anafanya tabia chafu za kihuni. Yule binti alibadiliaka ghafla na kusema, “Yqaani wameshakwambia niko hivyo, sasa mimi nimemkosea nini mjomba na familia yake” Akianza kulia, nilijisikia vibaya na kujilaumu kwa kumwambia vile. “Patience, nisikilize. Hebu nichukulie mimi kama baba yako. Naomba utulie unisikilize, kw sababu siamini hata jambo moja waliloniambia” Patience aliacha kulia na kunitazama sana hadi nikaogopa. “unasemaji?” Nilijikuta namuuliza. “hapana” alisema akijifuta machozi. Kwa kweli nilipokuw nikimtizama nilishinda kujua kama nilikuwa ninampenda, ninamwogopa, ninamwonea aibu au ninamfananisha. Ili mradi tu nilishindwa kuelewa.

Nilijisikia vibaya kuwa katika hali hiyo, lakini sikuweza kujizuia. “samahani, mama na wewe mlikuwa manishi wapi kabla hajafariki? Nilimuuliza. Alinitazama tena kama awali. “Tulikuwa tunaishi Arusha” Nilitaka kujua vitru fulani ili niamue kama ningeweza kumsaidia kumpata baba yake.

Lakini nilikuwa naogopa, maswali mengine huenda yangemkera.

“Mama yako alikwambia baba yako alikuwa anaitwa nani?” Yule binti alishika vidole vyake na kuchezesha miguu kwa muda kabla hajasema, “kama jina lako” nilijua alikuwa akinitania au alitaka kutumia mbinu ili niondoke naye. Ningeweza hata kufanya hilo kwa sababu kwa maisha kama yale ni wazi angeharibikiwa.
“Kwanza wewe unajua jina langu?” Niliuliza kwa mzaha. “ nalijua, si nilimsikia mjomba akisema akimwambia shangazi, Mr……….akija atatumia chumba cha kwanza. Alisema na nilianza kuingiwa na wasi wasi.

Alilotaja ni jina la ukoo, hivyo niliona niendelee na maswali, nikijua labda binti yule angekuwa ni mtoto wa ndugu yangu “Jina la kwanza na baba yako alikwambia ni nani?” Nilimuuliza. “Alinitajia, nimelisahau, alikuwa akipenda kutaja hilo la pili” Binti alisema.

Halafu alisema, “ Ninayo picha yake alipiga na mama, mnafanana naye kidogo. Ngoja nikaichukue .” aliondoka na kwenda huko chumbani kwake. Alikuwa akilala, kwenye kijichumba ambacho nadhani kilikuwa hasa ni stoo karibu na choo cha jumla cha mle ndani.

Nilijua ni mzaha mwingine, lakini nilitaka kumjua huyo mama na baba yake. Alirudi baada ya dakika kumi, bila shaka hiyo picha ilifichwa mbali sana. Alinipa picha hiyo na niliipokea kwa shauku kubwa. Nilitegemea kumwona ndugu yangu au mtu yeyote ninayemfahamu. Sikumwona yeyote kati ya hao ninaowafahamu. Ilikuwa ni picha ya mwanamke ambaye nilikutana naye kwenye semina ya maziwa, pale Shirika la Elimu kibaha mwaka 1981.

“Germana!” Nilinong’ona. Nilihisi nikiloa jasho mwili mzima na kwa muda fulani sikujua hasa nilipokuwa. Nilijikuta nikikaa kweky kiti hapo jikoni. Ni kama ndoto, ni ka hadithi, ni ka sinema fulani.
Nakwambia ukweli sijawahi kuhisi hali ile maishani na sijui kama nitakuja kuhisi, maana nashindwa hata kukueleza.
Yule binti alinishika na kunitazama machoni, “Unamjua mareehemu mama?” Alniuliza na sikuweza kumjibu. Nilitembe na mwanamke huyu ambaye ndio najua kwamba ni marehemu, siku moja tu kwenye semina ile. Hakuna aliyekumbuka kuchukua taaarifa kamili za mwenzake, kwa kuzingatia kwamba hatukuwa waajiriwa na tulikuwa ndio tuaanza maisha, vijana tunaochemka. Mambo ya semina, kutenda na kusahau.

“Kumbe Germana alizaa aliza mtoto mzuri hivi, mtoto wangu. Damu yangu inateswa na kudhalilishwa hivi”. Niliinama na kuanza kulia. Halafu niliinua kichwa na yule binti alikuwa akibubujikwa na machozi pia.
“Mi-mi, mimi ni baba yako Patience. Nisamehe, tusa-tusamehe sana halikuwa kosa letu……sikuweza kuendelea.

Waliporudi kanisani walishngaa kukuta tukiwa na Patience kule chumbani mwangu tukiongea na kucheka sana. Yule mke wa mwenyeji wangu ambaye sasa ni shemeji yangu alimwita Patience kwa nguvu na kisirani.

“Umeanza siyo? Unataka kumvuruga huyo baba wa watu, kisa?”
“Yaani wewe mtoto nitakuuwa tu, lazima” Nilimambia Patience akae kwanza hapo chumbani. Nilitoka mimi na kumfuata mke wa jamaa yangu, “Hapana dada, ni mimi nilimwita”

halafu nilimwita mwenyeji wangu aliyekuwa akitokea chumbani mwake kuja sebuleni.
Alipokuja nilimkabidhi ile picha niliyopiga na dada yake, alipoichukuwa aliitizama na kunitizama, aliitizama tena na kunitizama. Halafu alikwenda kukaa kwenye kochi na kushusha pumzi kwa nguvu.

“Naomba radhi, mimi ni baba wa mtoto Patience. Nimeamini kilichonileta huku Tanga siyo hii kazi yako bali ni nguvu ya damu yangu…..Mke wamwenyeji wangu aliingilia kati. “Ni kitu gani?”
Niliwasimulia kila kitu.

Sitaki kukuchosha. Hivi sasa Patience anasubiri kujiunga na masomo chuo kikuu baada ya kufaulu vizuri mtihani wake wa kidato cha sita. Amechelewa kusoma, ndiyo, lakini anataka kusoma na anamudu. Kumbuka jambo moja, Kila binadamu unayemtendea jambo baya, unaitendea damu yako jambo baya bila kujua. Kila binadamu unayemtendea jema, unaitendea jema damu yako bila kujua.

Sisemi kwa ubaya, lakini yule mke wa rafiki yangu alifariki mwaka 2001 kwa ugonjwa ambao inadaiwa kwamba ni ukimwi. Hali ya uchumi ya mumewa inatisha sana. Tazama naye yule mama marehemu aliacha watoto watatu. Je huko alipo atajisikia vipi watoto wake leo wakitendwa kama alivyokuwa akimtenda Patience? Kwani kuwapenda wengine gharama yake ni kiasi gani?

Je sisi wanaume tuna watoto wangapi huko nje ambao hatuwajuiwala kuwatambua? Lakini ni mara ngapi tunatamani na kuwafanya watoto hao kuwa wapenzi wetu?
Hatuoni tunafanya mapenzi na damu zetu?

*************************MWISHO***************************

1 comment:
Andika Maoni Maoni
  1. Kaluse, loooh, kisa hiki nimekifuata tangu ulipoandika sehemu ya kwanza, leo nimemaliza sehemu ya pili, kweli umenisisimua na nimefurahishwa mno kwa mwisho mwema wa Patience (wajina wangu Subira) ama kwa hakika jina lake limeendana naye, ndiyo maana huwa ninaamini kuwa majina yetu huwa yanabeba mengi kutuhusu, loh, ama kweli Subira huvuta heri, ni ufunguo wa faraja!

    Maswali ya tafakari uliyouliza mwishoni ni ya kweli na yenye uzito wa pekee.

    Huwa sisomi habari ndefu lakini inapokuwa ni kisa cha kweli, huwa napata nguvu ya ziada ya kusoma.
    Namtakia mafanikio mema Subira (Patience) mwambie Wajina anampa salam nyingi sana.

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi