0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Aug 16, 2009

WAUAJI WADOGO WA KISHETANI, SEHEMU YA MWISHO

Familia ya Lillelid


Mnamo Novemba 1997 watuhumiwa wote walifikishwa katika mahakama ya Greene County na kusomewa mashitaka 29 wote kwa pamoja.

Jaji aliyekuwa akiendesha kesi hiyo James Backner alikataa mapendekezo yaliyotolewa na jopo la mawakili waliokuwa wakiwatetea watuhumiwa kuwa kila mmoja ashitakiwe na kosa lake.

Jaji huyo alisema, watuhumiwa wote watashitakiwa kama kundi.
Wakati kesi hiyo ikiendeshwa, siri nyngi za watuhumiwa zilianikwa pale mahakamani.

Akitoa ushahidi wake mama yake Natasha aitwae Madona Wallen aliiambia mahakama kuwa mwanaye alikuwa ni mfuasi wa shetani na alikuwa ni muumini wa Ouija, ambayo ni imani kuwa watu walio hai wanaweza kuwasiliana na watu waliokufa.

Mama huyo alikiri kuwa, kuna wakati aliwahi kumuona mwanae, midomo yake ikiwa imetapakaa damu baada ya kunywa damu.
Naye rafiki wa karibu wa Natasha aitwae John Slayer aliyekuwa na umri wa miaka 19 akitoa ushahidi wake mahakamani alikiri kwamba, siku moja Natasha na mwenzie Karen walimuomba wamkata kifuani ili wapate kunyonya damu, naye akawaruhusu, ndipo wakamfunga kitambaa usoni kasha wakamkata na kuanza kumnyonya damu.

John alikiri pia kuwa zoezi hilo la kunyonya damu liliendelea kwa mtuhumiwa mwenzao John Risner na rafiki yao mwingine aitwae Jason Cecil.

Jambo lililowashangaza watu wengi wakati wa kusikilizwa kwa kesi hii ni kitendo cha Crystal Sturgil kumtaja mtuhumiwa mwenzake mwenye umri mdogo kabisa kuliko wote Jason Bryant kuwa ndiye aliyefyatua risasi na kuwauwa Lillelid na familia yake.

Wakati huo Jason alikuwa amehifadhiwa kwenye jela ya watoto ya Arizona akisubiri kusikilizwa kwa shauri lake tofauti na wenzie kutokana na umri wake.

Hata hivyo, kuna wakati alinukuliwa na mfungwa mwenzie aitwae Richard Arvizo akijisifu kwa kuuwa. Kwa mujibu wa maelezo aliyoandikisha polisi chini ya kiapo, Richard alidai kuwa, alipomuuliza Jason kama anajisikiaje kuuwa ? Jason alijibu kwamba, kuuwa huwa kunampa furaha na nguvu za ajabu.

Ushahidi mwingine uliotolewa pale mahakamani ni ule wa mwalimu aliyekuwa akimfundisha mmoja wa watuhumiwa Dean Mullins.
Akizungumzia tabia ya mwanafunzi wake wa zamani, mwalimu huyo alikiri kwamba, kuna wakati aliwahi kutoa zoezi la kuandika insha.

Mwalimu huyo anakumbuka maelezo yaliyoandikwa na Dean Mullins kuhusiana na namna ya kutoa macho kwenye mwili wa mtu aliyekufa.
Katka maelezo yake juu ya nadharia hiyo, Deana aliandika, “Imesemwa kuwa macho ni ufunguo wa rohoni, kwa hiyo kama nikiyachukua macho ya watu waliokufa nitakuwa nimechukua na roho zao pia, napenda sana nadharia hiyo”

Mtuhumiwa mwingine Crystal Sturgil maelezo yake yalikuwa ni yakusikitisha.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa mahakamani, ilibainika kwamba binti huyo alilazimika kukimbia nyumbani kwao na kuishia kuhama hama kutoka kwa ndugu huyu hadi mwingine kutokana na kunyanyaswa kijinsia na baba yake wa kambo.

Karibu watuhumiwa wote walikuwa wanatokea katika familia zilizosambaratika na zilizowapuuza. Lakini hiyo haikumfanya mwanasheria Berckley Bell kuyafumba macho yake dhidi ya yale yaliyofanywa na watuhumiwa hao.

Akizungumzia juu ya adhabu wanayostahili watuhumiwa pindi wakipatikana na hatia, mwanasheria huyo aliitaka mahakama itoe adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa watuhumiwa wanne waliokuwa na umri zaidi ya miaka 18, ambao ni Joseph Risner, Dean Mullins, Crystal Sturgill pamoja na Natasha, na adhabu ya kifungo cha maiasha bila uwezekano wa kupewa msamaha kwa watuhumiwa wawili waliokuwa na umri wa miaka 18 ambao ni Jason Bryant na Karen Howell.

Mnamo February 20, 1998 watuhumiwa wote walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka na Jaji James Backner.
Jaji Backner alipomaliza kuwasomea mashitaka aliwauliza kama watuhumiwa wote kwa pamoja wanakubaliana na mashitaka yote yaliyosomwa mbele yao au la.

Jibu lililotoka kwa watuhumiwa wote lilikuwa ni “ndiyo tunakubaliana na mashitaka yote tuliyosomewa”

Sikun ya hukumu, Jaji wa mahakama hiyo alisoma hukumi ambapo aliwahukumu watuhumiwa wote kifungo cha maiasha jela bila uwezekano wa msamaha wa parole.

Mara baada ya kumalizika kusomwa kwa hukumu hiyo, dada wa Delfina Lillelid aitwaye Ivette Zelaya alimpongeza jaji kwa kutoa hukumu hiyo, ambayo aliieleza kama adhabu nzuri inayowastahili watuhumiwa zaidi ya kunyongwa.

Akiongea na waandishi wa habari Zelaya alisema , “Ninayo furaha kubwa kwamba vijana hawa hawatapata fursa ya kuishi maisha wanayoyataka kwa kitendo chao cha kudhulumu roho ya dada yangu na familia yake na kuziacha familia zao zikiwa salama”

3 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Ahsante kaka Shabani kwa kukimalizia kisa hiki.........

    Unajua kwa wamarekani hili sio jambo la kushangaza kutokana na aina ya malezi ya watoto nchini humo.

    watoto wamepewa uhuru mkubwa sana kiasi kwamba wazazi hawana mamlaka kwa watoto wao, pia sheria za ndoa nchini humo zimepogoka mno kiasi kwamba kiwango cha talaka ni kikubwa kisicho cha kawaida.

    kama unavyojua kuwa talaka ina madhara makubwa sana kwa watoto, pale wazazi wanapotengana. Kama ulivyoona kwa yule binti Crystal Sturgil, kutokana na kunyanyaswa kijinsia na baba yake wa kambo ( naamini hata kubakwa alibakwa ) alilazimika kuhama nyumba moja baada ya nyingine na kutokana na kuwa alikuwa hathaminiwi kila alipokimbilia kutafuta hifandhi na ndio akaishia kujiunga na wenzie ambao wana similar back ground, na katika kujitafuta wakajikuta wakiishia kuua.

    Ni masikitiko makubwa kuwa waliodhuluimiwa uhai ni wanandoa vijana na waumini wazuri wa kikristo ambao walikuwa wakitokea katika kongamano la Kidini, Familia zao zilikuwa zikiwahitaji na jamii iliyowazunguka pia ilikuwa ikiwahitaji, lakini kwa mujibu wa maandiko matakatifu tunasema kuwa Mungu aliwapenda zaidi.

    Niliwahi kusoma katika kibaraza hiki wakati fulani kuwa kila jambo lina pande mbili, na mara nyingi tusichukie matokeo mabaya bali tujifunze kupitia matokeo hayo mabaya kwani ndio kujitambua. Naamini katika tukio hili kuna mambo kadhaa ya kujifunza, lakini kubwa zaidi ni kwamba kama hili lisingetokea unadhani dunia ingefahamu juu ya wale vijana? ni watu wangapi waliosoma mkasa huu na wanaoendelea kusoma mkasa huu ambao wamejifunza kuwa malezi ni kitu muhimu kwa watoto kwa ajili wa ustawi wa maisha yao?

    Bado kuna maswali kadhaa ya kujiuliza:
    Ni nini hatma ya mtoto Peter ( kama yuko hai) Je amewezaje ku corp na maisha baada ya tukio lile lililochukua roho za wazazi wake na dada yake?
    Je hatakuwa na kisasi juu ya wale vijana japo wako Jela?
    Je maisha yake sasa yakoje?
    Ni nini hatma ya wale vijana huko Jela, Je wanajutia makosa yao na wamekubali kumrudia mungu?
    Mwisho, baada ya hukumu kusomwa na wale vijana kuhukumiwa, dada yake Delfina Lillelid aitwaye Ivette Zelaya alisema.Nitamnukuu:
    "Ninayo furaha kubwa kwamba vijana hawa hawatapata fursa ya kuishi maisha wanayoyataka kwa kitendo chao cha kudhulumu roho ya dada yangu na familia yake na kuziacha familia zao zikiwa salama”
    Je maneno haya yalikuwa ni sahihi? Au ni kutokana na hasira?
    Tunahitaji kutafakari wote...............

    ReplyDelete
  2. Ahsante dada Koero kwa mchanganuo mzuri, ni kweli kuwa habari hii inahitaji tafakuri.

    Nimejifunza mengi juu ya kisa hiki na kwa mtazamo wangu, wazazi na jamii kwa ujumla wake imehusika kwa kiasi kikubwa kuchangia kuharibika kwa vijana hawa.

    Ni wazi kuwa walikuwa wanahitaji msaada wa kisaikolojia lakini hili halikuonekana. Hapa kuna mengi ya kujifunza, kwamba talaka sio jambo jema na hata kama ikitokea watu kutalikiana, basi inahitaji ushirikiano katika makuzi ya mtoto au watoto, kwani mapenzi ya wazazi wote wawili ni muhimu sana kwa ustawi wa watoto, ili kuwajengea future nzuri....

    Kaka shabani mimi nilikuwa ni mmoja kati wasomaji wazuri wa gazeti la Jitambue na mojawapo kati ya makala nilizokuwa nikizipenda ni ile ya kesi za utata, nimefurahi kuwa hatimaye umekubali ombi letu la kutuwekea makala hizi hapa katika blog yetu ya Utambuzi na kujitambua.

    Naomba nikiri kuwa mimi ni mmoja wa wasomaji wa blog hii niliyerkuwa nikimghasi kaka shabani atuwekee hizi makala za kesi za utata kwani nyingi zinafundisha kama tulivyoona hapa.

    Ingawa ni tukio la siku nyingi lakini bado kuna jambo tumejifunza wote.
    kaka naomba usiishie hapa uendelee kutuelimisha na makala zako za utambuzi..

    ReplyDelete
  3. Nashukuru kwa kuweka hiki kisa hapa kibarazani kwako kaka shabani. Ni kisa cha kusikitisha lakini pia ni cha kufundisha. Koero na Ramson wamesema yote ya muhimu. Ni kweli watoto wa ughaibuni wamelelewa vibaya mno. Imekuwa ni kinyume kabisa na Kwetu Afrika. Tupo pamoja kaka.

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi