0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Apr 21, 2009

KUFANIKIWA AU KUTOFANIKIWA NI UCHAGUZI WETU WENYEWE

Hata elimu ya ujasiriamali inalipa

Kuna watu ambao, kwa sababu ya kukosa kile ambacho jamii inakiona kuwa ndio ufunguo wa mafanikio, huwa wanaamini kwamba hawawezi kufanikiwa au kufanya vizuri maishani.

Kwa mfano, kwa kukosa elimu, ujuzi au utaalamu fulani, watu wengine hujihesabu kama wanyonge. Huchukulia kwamba ni wale tu wenye elimu, ujuzi na utaalamu fulani ndio wanaoweza au wanaotakiwa kufanikiwa.

Bila shaka umeshawahi kusikia au hata wewe mwenyewe kusema, “si wamesoma bwana, ndio wanaojaaliwa, sisi ambao hatuna shule kazi yetu itakuwa ni kuwatumikia”. Kauli kama hizi zina chimbuko lake mbali sana, pengine katika malezi yetu.

Wazazi walizoea au wamezoea kuwaambia watoto wao “Usiposoma, kazi yako itakuwa ni kuwabebea wenzako mizigo”. Kwa bahati mbaya mtoto aliyelishwa “sumu” hii anaposhindwa shule huamini kwamba yeye atabaki kuwatumikia wengine tu.

Tunapoamini kwamba, kwa sababu hatuna elimu ya kutosha na pengine ujuzi au utaalamu fulani, hatuwezi kufika juu kwenye mafanikio, ni wazi hatutafika. Moja ya vigezo muhimu vinavyoweza kutufikisha kwenye mafanikio ni kuamini kwetu kwamba tunaweza kufika huko. Tunapokuwa hatuna imani kwamba tunaweza kufika huko hujifungia njia wenyewe

Baadhi yetu huwa tuaamini kwamba tuna mikosi, balaa, au nuksi na pengine laana ambayo vinatuzuia katika kufikia malengo yetu. Tunaamini hivyo kiasi kwamba hata tukifikia karibu kabisa na mafanikio huwa tunajiambia ni kazi bure, tunaporomoka.
Na kweli kwa kuamini hivyo hujikuta tukiporomoka kila tukifika karibu na kufanikiwa au kufikia malengo. Kinachotokea ni kwamba, kwa kuamini kwetu kuwa tuna mkosi, balaa, laana au nuksi, huwa tunatenda kwa mkabala huo wa kinuksi au kibalaa na kimkosi, ambapo matokeo yake ni kujikwamisha.

Wataalamu wa elimu ya mafanikio wanaeleza kwamba, tunapoamini kuwa tuna mkosi au nuksi huwa tunayashauri mawazo yetu ya kina kutusaidia kuendelea kuwa katika hali hizo. Ndio maana sio rahisi kukuta mtu anayeamini katika nuksi akiondoka katika hali hiyo.
Baadhi yetu tumeokota imani fulani kutoka katika dini zetu, kwamba kupata au kukosa, kufanikiwa au kuanguka ni suala la kuandikwa kutoka mbinguni.

Nasema tumeokota nikiwa na maana kwamba tumetafsiri au kutafsiriwa aya yenye kuonyesha kwamba Mungu ndiye anayepanga kile akitakacho kutuhusu. Tafsiri ya aya hizi ni kwamba pale ambapo juhudi zetu zimeshindwa kuzaa matunda, hatutakiwi kulazimisha, kwani haitawezekana na tutajiumiza bure.

Kwa hali hiyo, kuamini kwamba hatupati au kufanikiwa kwa sababu ndivyo ilivyoandikwa, hutufanya tushindwe kuongeza juhudi hadi ukomo wetu na matokeo yake ni kukwama na kujaribu kuhalalisha kukwama kwetu na kusema “ Ni utashi wa Mungu” .
Ni kweli kwamba kuna wakati juhudi zetu haziwezi kushindana na mipango ya kimaumbile lakini pale ambapo tunachukulia kila jambo hata lile ambalo hatujalifanya kwamba ni kazi ya Mungu, huwa tunajitakia umasikini.

Wengi huwa tunapenda sana kusema, “siyo riziki” au “haikuandikwa” hata pale ambapo tunafanya makosa ya kukusudia. Badala ya kujifunza na kujirekebisha au kutumia makosa yetu kujifunza, huwa tunajiridhisha na kujifurahisha kwa kudai tu kwamba siyo riziki.
Hali hii iko sana pale ambapo tunashindwa kufikia malengo au kuanguka katika shughuli au juhudi za kufikia shughuli fulani. Badala ya kuchukulia maanguko yetu kama shule, kama sehemu muhimu ya kung’amua udhaifu wetu na kuurekebisha huwa tunachukulia maanguko yote kama kushindwa.

Huwa tunaamini kwamba huop ndio mwishomwa safari, tunajiona kwamba hatujitoshi wala kujimudu. Kwa kuchulia maanguko kama mwisho wa safari yetu kimaisha, tunaingia mahali ambapo tunajaribu kuukimbia ukweli. Tunaanza kunywa sana pombe ili kujiokoa na kiwewe cha kushindwa kwetu nap engine tunafikia hata kuamua kujiuwa au kufanya mambo mengine ambayo mwisho wake ni kutuacha tukiwa watupu.

Kuna baadhi yetu ambao tumefikai kuamini kwamba sisi ni watu wa kupata riziki tu, na sio zaidi ya hapo. Tunafanya kazi tukiwa na dhana hiyo, tunaweka akiba kwa kiwango cha dhana hiyo na juhudi zetu zinalenga dhana hiyo. Kwa hiyo kutokana na kuamini hivyo tunachohitaji ni riziki tu, mengine zaidi ya hapo hayatuhusu. Kuna wengine ambao ndio wanohusika katika kutafuta cha ziada, lakini siyo sisi.

Hapo tunakuwa tayari tumejiambia bila kujua kwamba ni lazima tufe masikini. Ni vigumu sana kama tumeshaamini kwamba sisi ni watu wa riziki tu, kuweza kupenya zaidi ya hapo. Maamuzi yetu ndio sisi wenyewe, hivyo hatuwezi kuwa wngine au vingine. Kama mtu ana imani hata moja kati ya hizo siyo rahisi kwake kuweza kuvukakkizingiti cha umasikini. Ni vigumu kwa sababu, mafanikio au kutofikia mafanikio kwa kiasi kikubwa ni suala la mtu mwenyewe kuamini.

Kuna wakati tunajidanganya kwa kauli za kisiasa kwamba kushindwa kwetu ni kwa sababu hatukupewa nafasi au “wageni” wamepora kila kitu. Inawezekana, lakini kama tutakaa na kubakia kulaumu tutajikuta tukifa masikini huku tukilaumu. Hata kabla ya mabadiliko ya kumpa Mmarekani mwenye asili ya Afrika, uwezo naye wa kujiamulia mambo yake, au kabla ya Makaburu wa hawajasalimu amri kwa utawala wa wengi kule Afrika ya Kusini, kulikuwa na weusi wengi ambao walikuwa na mafanikio makubwa huku wazungu wengi wakiwa hoi.

Suala hapa sio nafasi, bali kuamua kwamba mtu anaweza na kutenda kwa kujiona yuko sawa na mwingine na anastahili nafasi sawa ya kusonga mbele.

Sikatai. Ni kweli kwamba kuna vikwazo vingi vya hapa na pale, vya nje na ndani ya nchi, vilivyo ndani na nje ya uwezo wetu, ambavyo huchangia kuturudisha nyuma, hapa na pale. Lakini kama nilivyosema tukiviona kuwa hivi ni vikwazo na vigingi vya kutuzuia kufika tuendako, badala ya kuviona kama shule na sehemu muhimu ya safari yetu kimaisha, vitatupeleka kaburini tukiwa weupe kabisa wakati tulikuwa na uwezo wa kufanya wawili matatu ya maana.

6 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Umesema ukweli Bwana Kaluse, na sasa naweza kuuona mchango wenu ninyi watu mnaoshughulika na mambo ya kujitambua. Dhana hii ya kujiona mnyonge kwa vile tu mtu huna hiki au kile ni mnyororo tosha uliowafunga watu wengi - hata waliosoma na maPh.D yao. Watu wengi hawajiamini na kama hujiamini basi huwezi kufanya cho chote. Raisi Obama pengine ni mfano mzuri kabisa kuhusu hili suala la kujiamini na kukiendea kile unachokiamini na kukitaka hata kama kiko (au kinaonekana kuwa) mbali kiasi gani. Mada nzuri hii. Endeleeni kuelimisha jamii na Munga Tehenan huko aliko anatabasamu!

    ReplyDelete
  3. Kaka Kaluse, umeshawahi KUSHIBA NJAA? Ndio lishe na shibe tuliyonayo sasa. Ninakunukuu uliposema "tukiviona kuwa hivi ni vikwazo na vigingi vya kutuzuia kufika tuendako, badala ya kuviona kama shule na sehemu muhimu ya safari yetu kimaisha, vitatupeleka kaburini tukiwa weupe kabisa wakati tulikuwa na uwezo wa kufanya wawili matatu ya maana." Ndio maana nikasema namna uonavyo tatizo ndilo tatizo. Kwa tukio ama jambo moja unaweza kupata mitazamo elfu moja. Mtu anapoangalia namna ya kubadili aliyonayo kwa kukabiliana na vikwazo vilivyo mbele yake, ndio anapoweka maamuzi ya maiaha yake yajayo. Namkumbuka mchungaji mmoja aliyekuwa akipenda kusema kuwa "your mental picture will determine your actual future". Kwamba ukipanga kulima ekari 10 za mazao ukalima 10.25 utajiona umefanikiwa saaana wakati atakayepanga kulima ekari 20 kwenye nafasi hiyohiy msimu mwingine na akaweza kulima ekari 19 atajiona kama ambaye hajafanikisha malengo japo ana ekari 8.75 zaidi ya mwenzake.
    Kwa hiyo hakuna anayeweza kubisha kuwa KUFANIKIWA AU KUTOFANIKIWA NI UCHAGUZI WETU WENYEWE

    ReplyDelete
  4. Kaka zangu Kaluse,Masangu na Mzee wa Changamoto, nakubaliana na mawazo yenu, na nawapongeza kwa kuwa na mtazamo huu chanya katika harakati za kusaka mafanikio. Kila mtu hapa duniani anapenda kufanikiwa, kama yupo ambaye hapendi, basi huyo ana matatizo yake. Ukisoma nadharia za saikolojia ya mafanikio na hata sosholojia ya ukuaji, tunaelezwa kuwa mtu anaweza kufanikiwa pia kwa kujifunza kwa waliofanikiwa (social learning theories). Hili linawezekana, lakini kwa mtazamo wangu na hata ninyi kaka zangu mmeliweka wazi hilo, kuna vikwazo vinavyopelekea hata kama unajifunza kupitia wengine, bado ukakwama! Hapa unatakiwa kufanya nini?kukata tamaa?kuacha?la hasha!Nafikiri unatakiwa kujipa moyo lakini kubwa zaidi ni ku-strategize, na ikiwezekana kuwatumia wengine (umoja ni nguvu), kuwahamasisha na kuendeleza jitihada za kujikwamua kwa umoja wenu. Dhana ya umoja basi ni muhimu sana katika kusaka mafanikio. Ni kama vile ilivyo katika kuivunja mifumo inayozuia mafanikio, huwezi kufanya hivyo peke yako, lazima usaidiane na wenzako wenye mawazo kama yako. Hivyo nasisitiza suala la kuungana na kuwa na umoja thabiti ili kufikia mafanikio!

    Nawasilisha!

    ReplyDelete
  5. Haya Zuma huyooo anakuwa Rais wa Afrika Kusini. Kusoma kajifunza mwenyewe na karibu yote yaitwayo shule kajifunza mwenyewe na kwakujiamini simba jike kasingiziwa.
    Angekuwa mwingine asiyejiamini walioenda shule wangemkoma!

    Umemaliza Ambiere Kaluse!

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi