0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Mar 2, 2009

TUNANUNUA KWA UTASHI AU UHITAJI?

Mara nyingi tunanunua kwa utashi
Hivi unafahamu kwamba kuna watu wengi sana miongoni mwetu ambao hutumia fedha nyingi kwa vitu au mambo yasiyo ya lazima? Kwa kadri tunavyojipatia fedha zaidi ndivyo tunavyoitumia bila mpangilio. Hali hii ya mfumo wa maisha yanayo jail mali zaidi, imefanya watu wengi kuchanganyikiwa nakushindwa kujua tofauti kati ya uhitaji na utashi.

Kwa mfano mtu anaposema, ‘nahitaji televisheni ya nchi 36 sebuleni kwangu ‘ au ‘unahitaji viatu vinavyoendana au kumechi na nguo zangu.’ Je haya ni mahitaji au utashi, yaani kutaka kitu? Siku zote utashi umefungwa kwenye vitu au mambo ambayo ukiangalia kwa kina utagundua kwamba hayawezi kumfanya mtu ashindwe kuishi endapo atayakosa.

Kwa kutaka kwetu huwa tunajikuta hatimaye tukiingia kwenye maisha ya mashaka na hofu tunapofikia umri wa kati (miaka 35 hadi 55), kwa sababu ndiyo umri mgumu sana linapokuja suala la mtu kuamua kama akubaliane na maisha anayoishi au ajichanganye.

Kwa nini nilianza kwa kuzungumzia suala la hitaji na utashi? Jawabu ni kwamba kwa kuyajua vizuri maswala haya ndipo tunavyoweza kujitoa kwenye tafrani hii ya kimaisha. Kufahamu tofauti iliyopo kati ya hitaji na utashi kunaweza kabisa kutufanya kujua namna ya kutafuta yale ambayo ni mahitaji badala ya utashi.

Huwa tunahitaji chakula, mavazi, makazi/malazi, elimu, usafiri wa kuaminika, na tekinolojia kwa sababu ya kurahisisha shughuli zetu. Lakini pia tunahitaji mara chache kuwajali watu wa familia zetu.

Mbali na hayo hatuhitaji kuwa na televisheni ya inchi 36 yenye kushika stesheni 500 kwenye sebule zetu, gari flani la kifahari, nyumba yenye njia panda ndani au swimming Pool yenye kufanya kila kitu yenyewe. Huhitaji hayo kamwe lakini huwa tunakuwa na utashi nayo tunayataka. Sisi huku kutaka tunakuita kuhitaji.

Kumbuka kwamba hakuna makosa kwa mtu yeyote kumilika vitu hivyo na siyo vibaya kwa mtu kuvitafuta. Lakini ubaya ni kwamba vitu hivi kamwe haviwezi kutupa furaha. Badala yake mara zote vinatuunganisha na mnyororo unaotupeleka katika kufanya shughuli tusizozipenda.

Kwa nini kuna wauza ‘unga’ mjambazi, makuadi wa kisiasa na wengine wa aina hiyo? Thubutu! Wanafanya kwa sababu wanadhani wanachohitaji ni mahitaji wakati ni utashi.

Kuna wale wanaofanya shughuli halali lakini hawazipendi hata kidogo. Wanapata hata BP kutokana na shughuli kwa kawa huweza ikawa ni ngumu mno za hatari sana lakini wanang’ang’ania kwa sababu tu zinawapa kinachoweza kupata yale wanayodhani ni mahitaji.

Kuna wale wanaofanya shughuli zao mbalimbali kwa sababu wanazipenda na siyo kwa kuwaingizia pato la kuwapa yale wanayodhani ni mahitaji. Kwao inakuwa vigumu kuingiza pato na hata misukosuko ya kufilisika nayo huwa mingi. Lakini wanapokuja kusimama husimama kweli. Wale wanaofuata mlio wa fedha kwa kufanya chochote siku zote awali huwa na hali nzuri lakini baadae lazima waanguke vibaya.

Kuna haja ya kukumbuka kuwa, kuamini kwamba mali maana yake ni mafanikio na kila kitu cha gharama kubwa kifedha ni cha mahitaji ni tabia tu. Kama hiyo ni tabia inaweza ikabadilishwa.

Kwa mfano sasa imethibitika kwamba mtu anaweza kujifunza kufanya matumizi kidogo na ikawa ndiyo tabia yake. Kufanya matumizi kidogo ina maana ya kutafuta mahitaji kweli na siyo yale tunayodhani yatatupa thamani. Kwa kutegemea kidogo sana mambo ambayo wala siyo mahitaji katika kutupandisha thamani, huweza kutupa amani na furaha ya ukweli.

Kwani vitu vya thamani kamwe haviwezi kupima thamani aliyonayo mtu kwa kujitofautisha na wengine wasio navyo, ambapo kwa dhana hiyo wanaonekana kutokuwa na thamani.

Tukae tukijikumbusha tu kwamba thamani ya mtu haiwezi kupimwa kwa kulundika vitu ambavyo ni utashi na wala siyo mahitaji.

Lakini kuna ukweli kwamba mahitaji hayana maana yanapokuwa mengi au makubwa kwani ni mahitaji tu, maji ya kunywa ni gilasi moja hata kama una mapipa mia moja, huyahitaji kwa wakati mmoja hayo yote..

4 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Dunia ya sasa imeharibika kwani ni kweli kabisa kuna watu ambao hawahitaji vitu ambavyo ananunua isipokuwa anataka sifa au ufahari tu. Yaani ili mradi awe navyo na pengine hata havitumii. pia nyumba kubwa na pengene vyumba vingine hakuna anayelala na papo hapo kuna wanaohitaji sehemu ya kulala. Ahsante sana kwa somo hili kaka Shaban, nimejifunza mitu.

    ReplyDelete
  2. Kuna kipindi mchezaji maaraufu wa mpira wa miguu (David Beckham) aliwahi kuwa na tofauti na mke wake (Victoria)juu ya matumizi ya pesa.
    Victoria alimlaumu sana Beckham kwa kununua vitu vya gharama sana na wakati huohuo Beckham alimlaumu mke wake kwa kununua vitu visivyo na ulazima katika nyumba.
    Wawili hao walikuwa wanasumbuliwa sana na tatizo la utashi na uhitaji.
    Binadamu ana mahitaji matatu ya msingi, mavazi,malazi na chakula.
    Inapofikia mahali mtu anaanza kuchagua avae nguo gani ujue hapo anatoka katika hali ya uhitaji na kuingia katika utashi.Anapoaanza kuchagua ale nini pia anatoka katika suala la uhitaji na kuingia katika utashi vivyo hivyo katika suala la malazi.
    Ni wangapi tumekuwa na matumizi mabaya ya pesa bila kuzingatia uhitaji wetu?
    Miili yetu tumekuwa tukiilisha sumu kwa kudhani kuwa tunakula chakula cha gharama bila kuzingatia uhitaji wa mwili?
    Tufike wakati tuangalie zaidi uhitaji wetu kuliko utashi.
    Hongera kaluse kazi nzuri.

    ReplyDelete
  3. DUH!

    Somo kubwa na sina chakuongezea .Ila kuna uwezekano kuna mtu labda utashi ndio mahitaji.:-(


    Si kuna watoto na wajukuu wa chiefu Mareale na Gavana wa benki umkumbukaye kwenye noti za Tanzania tokea enzi za nyerere Moshi , Dar , Paris ,....na New York?

    Ambiere Tuko pamoja ingawa unanitenga !

    ReplyDelete
  4. Hili la utashi badala ya uhitaji nadhani kwa sasa ni janga la kitaifa.
    Ninalitazama kwa kina naona limeanzia mbali sana huko kwenye malezi yetu tukiwa watoto.Wazazi walio wengi walitufunza tuamini kuwa,kumiliki vitu vinavyoonekana vina thamani kv,gari,luninga nk humfanya anayevimiliki kuwa na thamani kubwa kuliko wasiokuwa navyo.Kauli kv soma uwe kama waziri fulani,au soma ili nasi tuwe na nyumba nzuri,video nk,humjenga mtoto kufikiri kuwa vitu vina thamani kubwa kuliko yeye.
    Mtoto anapoanza kupata fedha uelekeza nguvu zake ktk kununua vitu vitakavyomuonyesha kuwa na thamani ili apate furaha.Mwisho wa siku anakuwa na vitu vingi vyenye thamani kubwa,lakini furaha aliyokuwa anaitafuta inakuwa haijapatikana na vitu vingine vipya kuliko alivyonavyo vinakuwa sokoni vikiitaji watu kama yeye.
    Nashauri kuwa yatupasa tuwe na malengo na uchaguzi wa vitu tunavyovihitaji kabla ya kununua.UtaKapofika sokoni ukakutana na kitu kipya ambacho hakipo kwenye orodha yako,tafadhali usinunue na uwe na nidhamu kwenye suala hili.

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi