Kila mmoja wetu anajua kuhusu madai kuwa kuna uchawi au nguvu ambazo zinaweza kumfanya mwanamke kumdhibiti mumewe, wakati mwingine kwa lengo la uharibifu, ingawa ni katika kile kinachoitwa kupenda. Katika hali ambayo ni ya kustaajabisha kidogo, wataalamu wanasema hiyo ni kweli.
Lakini, ushikwaji huu unaonekana zaidi kuwa wa manufaa na hufanywa bila hiari ya mwanamke. Ina maana kwamba, mwanamke hujikuta akiwa yeye ndiye mwenye nguvu ya kuamua na mwanamume hulazimika kukubali nguvu hiyo kufanya kazi.
Karibu wanaume wote huathiriwa na nguvu hii ya mwanamke.
Ndiyo maana ni rahisi kusema wanaume wote wanashikwa au wameshikwa na mwanamke. Inatokeaje hali kama hii? Jibu lipo.
Inawezekana ni kweli wanaume wanaitawala dunia katika kile tunachokiita Mfumo Dume, lakini nao wanawake wanatawala kiota, siyo dunia. Ina maana gani? Kwa mujibu wa utafiti mpya wa hivi karibuni, inaonesha kwamba, wanawake wana nguvu kwenye maamuzi ya masuala ya nyumbani kuliko wanaume.
Watafiti wamegundua kwamba, wanawake kwa wastani, wanakuwa na nguvu kubwa ya uamuzi, unapokuja mjadala nyumbani unaohusu familia. Bila kujali kama ni mwanamke au mwanamume aliyeanzisha majadala huo, wanawake siku zote ndiyo wenye nguvu kwenye kauli ya mwisho.
Ndiyo maana ni rahisi hata kwa wanaume wakorofi kusikika wakisema, ‘nimeamua tufanye alivyotaka, ngoja mambo yaende vibaya, atanijua. Nimemwachia kusudi kama alivyotaka tufanye, lakini ataona mambo yakiharibika.’ Mara nyingi, mwanamke ndiye anayesikilizwa.
Lakini, inaonesha kwamba, kwenye zile ndoa ambapo wanawake husikilizwa zaidi yanapokuja masuala ya ndani, ndoa hizo zinakuwa imara zaidi. Hii inaonesha kwamba, huenda mwanamke mahali pake siyo jikoni, bali ni nyumbani, yaani ni mtaalamu wa masuala ya familia na uhusiano kwa ujumla, ingawa mwenyewe hajui.
Ndoa inapofikia miaka saba, kukawa na amani ya kuridhisha, kama wanawake kwenye ndoa hizo ndiyo wazungumzaji wakuu wa masuala ya ndani, mafanikio ya kindoa na kifamilia huwa mazuri, ukilinganisha na pale ambapo wanaume ndiyo wasemaji wakuu.
Hii ina maana pia kwamba, hakuna mwanamume anayeweza kudai kwamba hakushikwa kwa maana kwamba, ili kufikia mafanikio ya juu katika familia, mwanamume anapaswa kufunga mdomo, kwani majibu mengi anayo mwanamke.
Kwa wanaume ambao hawako tayari kuwasikiliza wanawake au kuwaacha wanawake kuwa wazungmzaji wakuu kwenye masuala ya nyumbani na familia, wanapata hasara kubwa. Ni hasara inayotokana na ukweli kwamba, wanaume wengi hawajui kitu kuhusu masuala ya nyumbani na familia kama wanavyojua wanawake.
Inaonesha kwamba, wanaume wanaokubali kushikwa na wake zao, yanapokuja masuala ya kifamilia na mambo ya ndani, ikiwemo maendeleo ya kifamilia na ushirikiano na watu wengine, wanafikia mafanikio ya haraka ya kifamilia. Kwa mfano, imethibitika kwamba, watoto hupata elimu nzuri na ya kutosha, ulaji ndani ya nyumba huwa mzuri na masuala ya bili kama za maji, umeme na mambo mengine huenda kwa mkabala mzuri.
Hata hivyo, hiyo hutokea pale ambapo ndoa ina amani na upendo. Lakini, kwa kiasi kikubwa pia hutegemea uwezo wa mwanamke katika kujua maendeleo na ukomavu mwingine. Lakini, bado wataalamu wengi wanakiri kwamba, mwanamke kimaumbile ana nguvu ya kusawazisha masuala ya kifamilia kuliko mwanamume, bila kujali ukomavu wake.
Utafiti huo umekanusha pia kwamba, wanawake huwa wanasema zaidi kuliko wanaume. Inaonesha katika utafiti huu mpya kabisa wa karibuni kwamba, wanaume na wanawake huzungumza sawa. Hapo kabla ilikuwa ikiaminika, baada ya tafiti kadhaa kwamba, wanawake huzungumza zaidi kuliko wanaume.
Hivi sasa imewekwa wazi kwamba, wote, wanaume na wanawake wana idadi sawa ya maneno. Pengine kinachofanya wanawake kuonekana wana maneno zaidi ni ule uwezo wao wa kusema hisia zao kirahisi.
Hii inaweza kuwa taarifa nzuri kwa wanaume, hasa wale anaoamini katika usawa. Ni taarifa nzuri kwa sababu, wanapaswa kujua kwamba, wanawake ndiyo waamuzi wa masuala ya familia kwa sababu, wanaonekana wako sahihi zaidi na wana hoja za msingi kwenye masuala hayo kuliko wanaume.
Lakini, wanaume wote wanapaswa kujua kwamba, huwa wanashindwa kwenye hoja na wake zao yanapokuja masuala ya nyumbani kwa sababu wanawake ni wazuri katika eneo hilo. Wanachoweza kufanya wanaume mara nyingi ni kulazimisha uamuzi wao kutokana na ubavu wa kimfumo dume.
Jan 21, 2009
JE HILI LINA UKWELI KIASI GANI?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Dah. Kaka hii darasa njema sana. Nashukuru saana na sitachangia maana nahisi kuna sehemu nishakuwa victim. Lol
ReplyDeleteAsantw sana Kaka
kofi la uso hili!
ReplyDeleteTamaduni pia zinamchango wake. Kwa wafini tofauti ya wanaume na wanawake kubwa ni kuwa mwanamke anapata mimba. Wanawake asilimia kubwa wa kifini ulichosema katika kuhusu wanaume ndio wanawake wa kifini walivyo.
ReplyDeleteHumpikilishi wala kumfanya akae nyumbani mwanamke wa kifini kirahisi na mabosi wengi mpaka Rais ni Mwanamke.Wafini wahusuduo mwanamke mwenye tabia za kianamke huoa Warusi au hata Wathailand.Kuna jamaa wakibongo huwa jasho linawatoka na wanawake wa Scandinavia.Unaweza kulinda nyumba yeye yuko bar kila akitoka kazini:-)