0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Nov 18, 2008

HOFU ZA KESHO BADO NI DUBWANA KUBWA LA KUTISHA?

Wamasai ni miongoni mwa jamii inayosifika kwa kufikiri vizuri, kwao kesho haina maana yoyote.

Naona makala yangu iliyopita inayozungumzia kuhusu kutoiogopa kesho haikueleweka kwa baadhi ya wasomaji.

Jana usiku nimepokea sms kutoka kwa msomaji mmoja akituhumu kuwa watu wa utambuzi huwa tunazungusha maneno.

Akilenga kwamba kesho ipo kwa hiyo ni lazima watu wahofu kuhusu hiyo kesho.

Nilijitahidi sana kuielezea mada hii kwa lugha nyepesi sana lakini inaonekana kwamba wapo baadhi ya wasomaji hawakunielewa.

Kwa kuwa nimeamua kufundisha kuhusu haya maarifa, sina budi kuweka sawa pale ambapo wasomaji hawanielewi.

Kimsingi sisi tangu tulipozaliwa tulifundishwa kufikiri vibaya, kamwe hatukufunndishwa kufikiri vizuri, ndio sababu watu wengi wanaishi katika maumivu makubwa kihisia na majuto.

Wapo watu ambao wanaamini kwamba kwa kuwa wazazi wao ni masikini, ambao kimsingi walitaka wenyewe, basi na wao watakufa masikini,

kwa nini? Kwa sababu wamefundishwa kwamba fedha huenda kwa wenye fedha na umasikini huenda kwa masikini.

Tumefundishwa kuwa, biashara kubwa kubwa ni kwa ajili ya wahindi na waarabu, biashara ya maduka ni ya wachaga na wakinga.

Tumeaminishwa hivyo ndio sabau tunashindwa hata kuthubutu, kwa sababu kila ukisema ujaribu zile sauti za kukatisha tamaa, kutoka kwa wazazi, ndugu, na jamii kwa ujumla zinakwambia, “huwezi acha kabisa, kamwe hutafanikiwa, hizo biashara zina wenyewe” Hata ukijaribu, ukipata changamoto kidogo, zile sauti zinarejea, na kukwambia, “ si tulikwambia bwana hizo biashara zina wenyewe”

Wakati fulani rafiki yangu mmoja alikuja kutaka kunikopa kodi ya kulipia fremu ya duka lake, kwa bahati mbaya sikuwa na hela. Rafiki yangu huyo alikuwa na wasiwasi sana, nilipomuuliza sababu, akaniambia kuwa mwenye hizo fremu ni mama mkorofi sana akicheleweshewa kodi hata siku moja anamfukuza mpangaji, nikamuuliza kwani alitakiwa kulipia lini hiyo kodi, akanijibu kuwa kesho ndio mwisho anatakiwa apeleke kodi ya watu.

Nikamshauri angoje hiyo kesho halafu aende kwa huyo mama mwenye nyumba na kumwambia ukweli kwamba amekwama kupata kodi kwa kuwa biashara sio nzuri, asikie mama atasemaje? Alikubali lakini bado alikuwa na mashaka kidogo.

Nilipokutana nae wiki mbili baadae aliniambia kuwa yule mama alikubali bila kinyongo kusubiri angalau kwa wiki mbili, na hakuonesha kukasirika, na alimwambia kuwa katika wapangaji wake wote yeye ndiye mpangaji muaminifu kuliko wote kwa sababu huwa anapeleka kodi kwa wakati.

Si unaona jinsi hofu zetu zinavyotuambia uongo. Wataalamu wa nguvu za mawazo wanasema, kwamba kwa kawaida hofu zetu zina asilimia 1 tu ya ukweli, asilimia 99 ni uongo.

Kama mtu unafikiri vizuri sidhani kama utaihofia kesho, kwani kesho ni nini?

Ipo kanuni moja inayosimamia namna ya kufikiri kwetu, huwezi kufikiri jambo hili ukavuna jambo lingine, ukifikiri kuhusu mafanikio utavuna mafanikio, kwani kile ambacho mawazo ya kawaida yanafikiri na kuamaini, mawazo ya kina yanakichukuwa na kukizalisha kama kilivyo.

Kanuni hii ilifundishwa na Yesu miaka 2000 ilioyopita kama Budha alivyofundisha kanuni hiyo miaka 500 kabla ya hapo, kwamba kile unachowaza na kuamini ndio mavuno ya kile ulichonacho leo.

Kwa kuhofia kwetu kuhusu kesho, ndio sababu wengi wetu tumekuwa watumwa wa waganga wa kienyeji.

Waganga wengi wamenufaika sana na ujimga huu, ndio sababu wanavuna kila siku, kwa sababu kila mtu anataka kujua kesho itakuwaje, iache ije, unahofu nini?

Unapoenda kwa mganga anaweza kukwambia, “naona yule jirani yako anataka kukumaliza kwa sababu anakuonea wivu na maendeleo yako”

Kwa kuwa unamuamini mganga, unaanza kujenga hofu na chuki dhidi ya jirani yako, kosa kubwa linaanzia hapo, kwani katika mawazo yako ya kawaida huwezi kufikiri kitu kingine zaidi ya chuki, hicho ndicho kitajkachoelekea kwenye mawazo yako ya kina.

Sasa hapo unafikiria utavuna nini? Ni lazima utavuna maanguko.

Ni sawa na kujenga daraja kuelekea katika maanguko yako.

Ili kuondokana na hali hiyo, kinachotakiwa ni kuanza kufikiri vizuri, kufikiri vizuri kwa maana kwamba tufikiri, malengo na mafaniko yetu na yale mambo yanayotupa faraja, na kutufurahisha.

Naona kwa leo niishie hapo, nikipata wasaa nitaandika makala inayofundisha namna ya kufikiri vizuri.

Hadi wakati mwingine, naomba kuwasilisha.

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi