0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

May 4, 2011

MSINIONE NAPENDEZA

Hapa ndipo ninaponunulia Viwalo vyangu............


Hivi karibuni nimemtembelea Rafiki yangu Musa Hassan maarufu kwa jina la Kambi, yeye ni muuzaji wa Nguo zilizotumika huko Ughaibuni maarufu kama Mitumba pale maeneo ya Karume. Ni siku nyingi kidogo tangu nilipoonana naye kwa mara ya mwisho. Nilizungumza naye mambo mengi juu ya maisha na mustakabali wa biashara zao pale Karume pamoja na rabsha za Askari wa Jiji.


Jambo moja ambalo lililonivutia ni kuhusiana na Machinga Complex, nilimdadisi kutaka kujua kwa nini hakuomba nafasi katika jengo lile ambalo hadi leo bado lina nafasi za kutosha?

Maelezo yake kwa kweli yaliniacha kinywa wazi.......... wiki ijayo mungu akipenda nitawawekea kile nilichozungumza na rafiki yangu huyu.

2 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Itakuwa poa sana kusikia mtazamo wake kwa kuwa nimesikia tu tetesi kuwa kuna matatizo yake pale complex!

    ReplyDelete
  2. Ni kweli kaka unapendeza na usidhani upo peke yako.... Kwa hamu kubwa sana twasubiri kusikia hicho kilichokuacha mdomo wazi...

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi