0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

Apr 11, 2010

MGUU ULIOPOTEA KWA AJALI YA NGUVU HASI-SEHEMU YA MWISHO

Kila kitu kilikuwa peupe


ILIPOISHIA.........
Upande alikuwa amekaa Waridi ukifikia kwenye shina la mwembe. Sikusikia tena kitu, wala kujua kilichotokea. Ni siku ya pili jioni niliposhtuka nikiwa Muhimbili. Nilimwona mke wangu akiwa kando ya kitanda changu pamoja na watumishi wa makao makuu ya idara niliyokuwa nafanyia.


ENDELEA KUSOMA HAPA..........

Nilihisi kama wepesi fulani huko chini. Nilipokaguia, niligundua kwamba, sikuwa na mguu wa kushoto.

Ilinichukua muda kabla sijakumbuka kilichotokea. Polepole nilikumbuka kutoka Iringa, Morogoro bado Mlandizi. Sikukumbuka tena kitu. Ilinichukua muda kukumbuka ajali na kumkumbuka Waridi. Nisingeweza kumuuliza mke wangu au yeyote pale kuhusu Waridi, Lakini nilikuwa na uhakika kwamba , alikuwa amekufa.

Nilianza kububujikwa na machozi. “Nilijaribu kusema , lakini sikuweza, ni midomo tu iliyokuwa ikicheza.

Amekufa, amekufa, uso wangu sasa naupeleka wapi, nauweka wapi jamani...” Mke wangu alisema na kuangua kilio. Nilimwelewa. Wale watumishi wenzangu walimtuliza.`tuangalie na kujali hali ya mgonjwa kwanza,` walimwambia.

Ni kweli, Waridi alikufa palepale kwenye tukio la ajali na mimi ni bahati tu kupona na kukatwa mguu mmoja badala ya miguu miwili na mikono. Nilikuwa na uhakika kwamba, makovu ya mwilini baada ya kupono yangekuwa yanatisha.

Kila kitu kilifahamika baada ya siku ya tatu tu. Mume wa marehemu Waridi alirejea safarini na kusimuliwa kila kitu. Aliahidi mbele za watu kwamba, angenimaliza na mimi, iwe kwa mvua au jua. Nilipopata taarifa hizo nilicheka kwa sababu, niliona akifanya hivyo angekuwa amenitua mzigo mzito. Labda aliambiwa baadaye nilivyokuwa nasema, ndiyo maana hakunifanya lolote.

Nilitoka hospitalini nikiwa na mguu mmoja baada ya miezi mitatu.Nilikuwa na nafuu kidogo. Mke wangu alishaanza uhusiano na yule mfanyabiashara na hakunificha. Ilibidi nifikie mahali niombe talaka. Talaka ilitolewa na kuwaacha waendelee. Hatimaye, mwaka 1985 walioana, ingawa ndoa yao ilivunjika mwaka 1990 kwa makeke na vurugu kubwa.

Mimi nimepunguzwa kazi mwaka juzi na hivi sasa nina shughuli zangu. Nilikuja kuoa mwaka 1987, mke ambaye tunaelewana sana na amekuwa ndiye kiongozi wangu kwa mambo mengi. Tuna watoto wanne Kuna watu wanapenda kuniita Zubeir Kaguu kwa siri. Nawaomba waniite kabisa kwa nguvu, kwa sababu ninastahili.


**********************************************


Tunajifunza kutoka kwa wengine, kama tumeemua kujifunza. Ka wale ambao wameamua kujifunza kupitia habari hii, ni wazi watakuwa wamejifunza kitu kikubwa na cha maana sana.

Wataalamu wa uhusiano wanadai kwamba, mtu anapotoka nje ni lazima atafumaniwa. Kama hatafumaniwa mwaka wa tatu tangu uhusiano wake na huyo mpenzi wake kuanza, basi ni lazima atafumaniwa kabla ya mwaka wa sita wa uhusiano huo haramu.

Kinachofanya mtu afumaniwe ni ule ukweli kwamba, baada ya kuzoea, mtu hujisahau na kuweka ngao yake ya kujikingia chini. Badala ya kwenda mbali kufanya mapenzi, watu watafanyia karibu, badala ya kuwaficha watu, ataambiwa mmoja ambaye anaitwa rafiki yangu wa kufa na kuzikana na hisia za umiliki badala ya wizi hujijenga.

Kufumwa kunaweza kusababishwa na chochote kati ya hayo au mangine. Kwa mfano, ajali ambayo imewatoa hadharani marehemu Waridi na Zubeir, inatokana na kuzoeana ambako kumeondoa hofu ya wizi wa `mali ya mtu`na kuwafanya wote, kila mmoja kuamini kwamba, huyo mwenzake ni mali yake.

Unaweza ukaamini kwamba , wewe ni mjanja na una maarifa mengi sana katika kukanusha, katika kuteleza, usifumaniwe. Lakini kwa sababu ni nguvu mbovu unazozippanda ni lazima utazilipia, kwani zitakurudia tu, utake usitake-

Unapotoka nje, jiandae kunaswa siku isyo na jina. Kama utaacha kabla hujanaswa, siyo kwa sababu ni mjanja, bali ni kwa sababu, hiyo nguvu uliyopanda ilikuwa haijakamilishwa mzunguko wake.

Unapoonywa na mpenzi wako, unapooneshwa wasiwasi kwamba, unatoka nje, kama ni kweli, inabidi uache. Kama utaendelea, jua tu kwamba, utapata shida utaumia baadaye.

**************MWISHO******************

1 comment:
Andika Maoni Maoni
  1. Na kufumaniw si lazima uwe ktk tendo. Hata sms tu yaweza kukutoa udenda na hapo fumanizi likawa kama vile umebambwa live....lol

    Kweli HUJAFA HUJAUMBIKA :-(

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi