0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Jan 3, 2009

GHARAMA ZA HOFU YA KUGEUKANA!!!!!!!

Je umewahi kufikiria ni kwa nini maisha yetu ya sasa tunawategemea sana wanasheria? Kama umenunua nyumba hivi karibuni, ni lazima utakuwa umesaini nyaraka chungu mbovu mbele ya wanasheria.

Nyaraka hizi ni lazima zisainiwe na muuzaji na mnunuaji ili kama mmoja anamgeuka mwenzie, yule anaegeukwa awe salama kwa kiasi fulani.

Kila kitu huanikwa wazi katika mikataba hii ili msirukane baadae ninyi mlioingia katika mikataba hiyo. Hakuna siri tena! Wanasheria wako upenuni mwetu kila kukicha, na ili uweze kusalimika kama utashitakiwa mahakamani huna budi kuweka wakili tena!

Kama unavyojua ni kwamba sheria za nchi zinatungwa na na wabunge. Humo bungeni hawakosekani wanasheria kwa sababu ndio wenye fani; hivyo sheria hizi kwa bahati mbaya tena hutungwa na wanasheria!

Jamii ya wanasheria huweka shinikizo ili tusiweze kuishi bila kuwategemea. Kila mtu katika maisha ya siku hizi analipa gharama kubwa kwa wanasheria ili kuogopa migogoro ya baadae kati ya muuzaji na mnunuaji. Kama ndio hivyo basi tumekwisha!
Kwa mfano kuuza shirika la umma , gharama za kisheria ni nyingi mno; inakadiriwa kufikia shilingi bilioni 100! Hizi ni gharama za kutisha!

Hizi fedha zinazomwagwa kwa wanasheria zingekuwa zinaenda kwa wenye kampuni kama hisa zao na kufaidi matunda ya kazi zao, badala yake zinaenda kwa wanasheria! Kwa kazi gani hasa mpaka walipwe fedha kiasi hicho?

Inatisha sana mpaka wakati mwingine najiuliza miaka 25 au 50 ijayo gharama hizi zitapanda kwa kiasi gani? Hizi ndizo gharama za matarajio ya kugeukana!

Mpaka hapa tunaweza kusema kwamba tuko katika wakati ambapo kila kitu tukifanyacho lazima kianikwe wazi kabisa na kutolewa maelezo ili kuzuia migogoro ya baadae!

Nina matumaini, mbali ya mikataba, kila jambo hata la kawaida linalofanyika ni lazima litafanyika kwa makubaliano ya kimaandishi kwa kila mhusika. Kwa upande wa mikataba ndio hiyo mikataba niliyoisema mapema.

Mikataba ya ndoa ya wapenzi kabla hawajaoana ni jambo la kawaida siku hizi na ni kivuno kizuri tu kwa wanasheria!
Talaka nazo ni biashara nono kwa wanasheria!

Hivi ni kwa nini binadamu asijifunze kusimama kwenye ahadi na kauli zake? Kwa nini asijifunze kula kilicho chake tu? Kwa nini asiwe mnyoofu asiyehitaji kutishwa ili atimize wajibu? Ni kwa sababu amepogoka, anataka kupata anataka kushinda maana kwake maisha ni mashindano.



This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi