0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Feb 22, 2009

USISITE KUMFAHAMISHA MWENZIO

Wanautambuzi wakiwa darasani
Wapendwa wasomaji wa blog hii ambayo lengo lake kubwa ni kutaka kuwafanya wanajamii kuanza kuyatazama upya na kuyatafakari maisha yao ya kila siku kwa mapana na kina kwa lengo la kujiletea mafanikio.

Ni kweli kwamba kuna ugumu kwa mtu kubadili tabia ambayo ameizoea na hasa kama siku zote amekuwa akiamini kwamba tabia hiyo ndio mtindo halisi wa maisha kwa sababu karibu kila mtu anaifuata.

Lakini pale ambapo mtu ataamua kubadilika, atagundua kwamba hakupaswa kuishi kama anavyoishi sasa, atagundua kwamba taabu na madhila aliyokuwa akijitwika kila siku hayakuwa na ulazima wowote kwake. Ninachoandika humu ni muhtasari wa yale tunayo
jifunza katika madarasa yetu ya utambuzi pale Kimara kona kwenye jengo la FAJI.

Hapa ninajaribu kuchambua mada moja moja ili angalau wasomaji wa blog hii waweze kuona umuhimu wa kujifunza maarifa haya ya utambuzi. Kama ungependa kujua zaidi faida za maarifa haya, unakaribishwa pale Kimara Kona kila Jumamosi na Jumapili kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa nane mchana.

Msomaji mpendwa kama utaona kwamba kwa kiasi fulani hata kama ni kidogo yale yanayoandikwa humu yana manufaa katika kubadili maisha yako, basi usisite kumjulisha mwingine kuhusu faida ya kujifunza maarifa haya. Kituo cha FAJI pale Kimara Kona kumejitolea kueneza maarifa ya utambuzi kwa wale wenye nia kubadilika, na pia kuwasaidia wale wenye ndoa ngumu, watumwa wa waganga wa asili, wanaoishi katika familia zenye ukorofi, wenye vipaji maalum lakini kwa bahati mbaya wameshindwa kuving’amua, na wenye nguvu za ziada ambazo kwa njia moja au nyingine zinawatesa.

Kama uko mbali na una jambo unataka kujifunza au unataka ufafanuzi zaidi kuhusiana na maarifa haya ya utambuzi, unaweza kuwasiliana na sisi kwa barua pepe kwa anuani hizi zifuatazo.
utambuzi1@yahoo.com, au utambuzi1@gmail.com.
Kwa wale wenye kuhitaji ushauri nasaha, wasisiste kufika pale kituoni kwetu Kimara Kona.

No comments:
Andika Maoni Maoni

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi