0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Nov 25, 2008

MAJIBU KWA KAMALA!!!!!!!!!!!!!!

Elimu ya utambuzi inapatikana hapa.


Kama nilivyoahidi kumjibu Bwana Kamala, nimeona si vyema kumuacha hewani.
Labda nikumbushe tu kwamba, kwenye makala yangu niliweka wazi kwamba ni vyema kama unataka kuelewa mada ya sisi ni nani, basi utoke kwenye dini kwanza au kwenye kile unachokiamini, hapo ndipo utakapoelewa mada hii vizuri.

Sisi tumefungwa sana na imani za dini, kiasi kwamba hatuwezi kuona kile kilichoko nje ya imani hizo, na kwa kawaida kama unataka kujifunza jambo fulani jipya ni lazima utoke kwanza nje ya hilo jambo au kwenye imani nyingine zinazokufunga ili uweze kujifunza vizuri.

Nikisema hivyo nina maana kwamba, wakati unapojifunza maarifa haya huenda kuna mambo ambayo yatakuwa yanakinzana na imani yako, hivyo utakuwa na wakati mgumu sana wakati unapojifunza kwa sababu utakuwa na mtazamo hasi juu ya maarifa haya, na hiyo haitakusaidia sana.

Sio lazima kujifunza haya maarifa kama unaona hayana maana kwako, lakini kama unaona kuna umuhimu wa kujifunza kitu kipya ili uyaone mambo kwa mkabala tofauti, basi inabidi ukubaliane na mimi kwamba ni vyema ukatoka nje ya kile unachokiamini.

Katika makala zangu zilizotangulia nilieleza vizuri sana, faida ya kujifunza haya maarifa, kwa hiyo sioni sababu ya kurudia tena.Ukweli ni kwamba nisingependa kuzungumzia imani ya wakiristo juu ya Yesu kupaa mbinguni akiwa na mwili, hiyo inahitaji makala inayojitegemea, na ni mada ya baadae sana.

Nilisema nitazungumzia Miili mitatu tuliyonayo sisi wanaadamu na kama ikibidi nitazungumzia mwili wa nne.

Miili niliyoitaja ni hii ifuatayo:

(i) Mwili huu tunao uona, yaani wa mwili wa nyama (Ambao nimeshauzungumzia)

(ii) Mwili wa akili

(iii) Mwili wa hisia

Kama ukijifunza kuhusu hii miili mitatu, na kutenda yale unayofundishwa naamini itakusaidia sana kujifunza mwili wa Roho na na kuuelewa kirahisi zaidi.
Hata hivyo ni vyema nikaweka wazi kwamba mwili wa roho ninaouzungumzia hauhusiani na dini kabisa.

Kuhusu kula nyama, hili nadhani imeelemea zaidi kwenye mambo ya kiafya, mara nyingi tanashauriwa kutokula nyama kutokana na madhara yanayotokana na nyama.
Hata hivyo lazima nitahadharishe kwamba kuna virutubisho muhimu vinavyotokana na nyama, kwa hiyo kama unaamua kutokula nyama basi ni lazime upate virutubisho hivyo kutoka kwenye vyakula vingine mbadala, na kama ikishindikana basi ule nyama kwa kiwango kidogo sana, lakini lazima ufahamu kuwa madhara yako pale pale.


Ikiwa una nia ya kutaka kujifunza maarifa haya kwa undani zaidi, basi unakaribishwa kwenye madarasa yetu.

Maarifa haya yanapatikana pale Kimara Rombo katika jengo moja lililoandikwa “FAJI, ELIMU YA UTAMBUZI INAPATIKANA HAPA”
Ukifika pale utapata majibu yote ya maswali yanayokutatiza.

2 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. ahasante kwa mafundisho yako mazuri ndugu mtambuzi.

    lakini je unadhani tunaweza kutoka nje ya dini zetu? mtu aliyebatizwa akiwa na miezi michache tu duniani, akasoma nursury ya dini, akafundishwa kipaimara fasta na kupewa kumunio huku akivalishwa mavazi ya dini na kumilikishwa dini hiyo, anaweza kweli kutoka nje ya dini?
    kumbuka hakuchagua hiyo dini, lakini amezungukwa kinoma, afanyeje? hujui akitoka nje ya dini anaweza kupata adhabu ya kufa, kuwa masikini, kuchomwa moto na kwenda kuzimu akaishi na shetani?

    ReplyDelete
  2. Kamala,
    Hukunielewa,
    Niliposema mtu atoke nje ya dini si kumaaanisha mtu aache dini yake, bali nilimaanisha kutoka kwenye dini kifikra, na kuwa huru kwa muda.
    Kwa sababu huwezi kuelewa maarifa haya ya utambuzi kama utakuwa unachanganya na hisia za dini.
    Nadhani umenielewa mzee.

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi