0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Jan 26, 2009

WANAUME WOTE WANA NYUMBA NDOGO?

Kuna idadi kubwa sana ya wanawake kuliko mimi na wewe tunavyoweza kufikiri, wanaoamini kwamba wanaume wote wana nyumba ndogo. Je wewe mwanamke ndivyo unavyoamini? Je wewe mwanaume umeshawahi kuambiwa hivyo na mkeo au mpenzi wako? Kama bado basi wewe una bahati.

Kwa nini wanawake hawa wanaamini hivyo? Kuna sababu kubwa moja tu ambayo ndiyo yenye kufanya imani hii kushika mizizi, nayo ni malezi. Wanawake kama ilivyo wanaume wamelelewa kwa kuamini kwamba wao ni dhaifu na wanaume ni imara. Wamelelewa kwa kufundishwa kwamba wao hawana haki zote ndani ya nyumba kama ilivyo kwa wanaume.

Katika kuamini huku wanawake wamejikuta wakiwa ni aina ya watumishi ndani ya ndoa na wamejikuta wakiwa ni watu wa jikoni ndani ya ndoa na waamejikuta wakiwa watu wa kupewa amri na kuzipokea ndani ya ndoa. Katika mkabala huo wanawake wamejikuta wakiwa hawana kauli wala sauti hata katika maswala ya kimaumbile.Kwa mfano ni mwanamume ndiye anayetakiwa kusema ‘leo sijisikii’ na siyo mwanamke na ni mwanaume anayetakiwa kusema ‘leo nahitaji’ na siyo mwanamke.

Mwanamke anapokua na mahusiano na mwanaume mwingine nje, anapewa haraka jina la ‘Malaya sana’ wakati mwanaume anaweza kupewa jina la sifa “mkali” au “mtu wa watoto” hata kama ana mahusiano na wanawake kumi. Hii sio nasibu ya mambo bali matokeo ya malezi yetu.

Kwa kupewa nafasi kama hii mwanaume amekua huru kushiriki tendo la ndoa kwa kadri atakavyo kwenye familia zetu. Nyumbani hua tunaona jinsi watoto wakiume wanapokua na marafiki wa kike lisivyo jambo la ajabu , bali tu pale watoto wa kike wanapo jaribu kuwa na marafiki wa kiume hata wale makaka ambao wao huwachezea madada wa wengine huko nje huwa wakali sana kwa madada zao.

Kwa mkabala kama huo, kwenye jamii yetu mwanamke kua mcheshi, mzungumzaji huru na mkaribishaji mzuri kuna maana moja tu kwamba huyu ni malaya, bali kwa mwanaume sifa hizo hubaki hivyohivyo na pengine kuongezewa uzito. Hata kama ndani ya sifa hizo kumejificha ufuska ulio kubuhu, hakuna atakayejali sana.

Kuna ukweli kiasi fulani kwamba, wanaume wengi huwa wana ‘nyumba ndogo’ au zaidi ya rafiki mmoja wa kike. Hali hii imepelekea hata watu kuamini kwamba wanaume wana hamu kubwa na tendo la ndoa kuliko wanawake, jambo ambalo limekanushwa na tafiti nyingi zilizofanywa kuhusiana nalo.

Wanaume kwa sababu za kamalezi na ubabe ulio katika mazoea ya kimapokezi tangu kale, wanaamini kwamba wao ndio wenye uhuru wakuchagua kama waendelee kua na mmoja au hapana. Kwa hiyo,kwa sababu wao ndiyo ambao wamejipa funguo ya maamuzi hufanya uharibifu mwingi.

Kwa kuwa wanaume wanaamini kwamba wanapaswa kuabudiwa na wanawake, linapotokea tatizo dogo tu la kindoa huamua kutoka nje, kwa sababu wanawake kwao ni vyombo vya starehe vinavyoweza kununuliwa mwanamume anapojisikia. Lakini pia hii ni kwa sababu, kutoka nje kwao ni aina ya sifa wakati mwingine.

Kutokana na malezi haya ambayo yanahalalisha mwanaume kuwa “kijogoo” wanaume wengi wamekua na urahisi wakutokua waaminifu . Lakini hata hivyo,hakuna ukweli kwamba wanaume wote wana nyumba ndogo. Nadhani unajua tofauti kati “wote” na “wengi”

Ni vigumu kusema idadi halisi kwa maana asilimia, kwani hakuna utafiti rasmi ambao umefanywa, lakini kwa utafiti usio rasmi imethibitika kwamba kwa hapa Jijini Dar es salaam, kuna uwezekano mkubwa kwamba katika kila wanaume kumi, saba wana ‘nyumba ndogo’ au rafiki wa kike zaidi ya mmoja.

Idadi hii ni kubwa sana na kuna haki kwa watu kuamini kwamba kila mwanamume ana ‘nyumba ndogo’. Lakini bila shaka umefika wakati kwa wanaume kujiuliza kama tabia hiyo ina manufaa yoyote kwao na kama huko sio kuwazalilisha wake au wapenzi wao. Je, wake zao wangekua wanafanya hivyo wao wangejisikia vipi,au wanadhani wanawake hawana hisia kama binadamu?

Tukutane wakati mwingine

5 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Nikuunge mkono kwa uiyoyaandika.

    Jana nilikuwa na dada mmoja pwani tukibadilishana mawazo,mara ikaja hiyo mada,yeye akasema wanaume wote wana uhusiano na zaidi ya mwanamke mmoja na akajaribu kutoa mifano kadha wa kadha kuthiditisha kauli yake.Nikachukua muda mrefu kidogo kumwelimisha aweze kutofautisha kwanza wengi na wote alipoenielewa ndiyo tukaja kwenye mada hasa.

    Nilichojifunza bwana Kaluse Malezi yetu ndiyo yanayopelekea wengi tuamini na kutenda hivyo.
    Unapoamini jambo jua maishani mwako jambo hilo litatendeka na kuonekana machoni mwako kwa mkabala ya unavyoamini haiwezekani ukaamini kuwa wanaume wote si waaminifu katika mahusiano ya mapenzi halafu ukaja ukakutana na vitu tofauti.

    Jamii yetu imewafanya wanawake wengi waamini kuwa mwanaume hawezi kukaa na mwanamke mmoja kwa maisha yake hapa dunia na wao wakaamini hivyo kwa hiyo kinachotokea ni kule kuamini kwao hivyo.Hivyohivyo wanaume wamefanywa kuamini hivyo na wakatenda kama waliavyoa aminishwa.

    Napenda ninukuu maneno ya mwanasaikolojia mmoja ambaye sasa ni marehemu,Munga Tehnani anasema "ukivaa miwani mieusi utaona vitu vyeusi na ukivaa mawani ya kijani vitu utakavyo ona ni vya kijani"mwisho wa kunukuu.Kama ukiamini kuwa wanaume wote wana nyumba ndogo basi tegemea wale utakao kutana nao maishani wote ni wale unaowaona kulingana na mkabala wa mawani uliyo vaa.

    Hata hao wenye wanawake wengi ukikaa na kuwahoji kwa nini wanakuwa nahiyo tabia jibu atatoa kwa jinsi alivyoambiwa na walezi au jamii aliyokulia.

    ReplyDelete
  2. Nadhani suala hasa ni mtazamo wa mtu husika. Mambo haya ni vigumu kuwa katika majumuisho ya jinsia.

    Siamini kwamba mwanaume asili yake ni nyumba ndogo. Nadhani tatizo ni namna wanaume fulani (pengine wenye nyumba ndogo) wanavyolikuza hili na kulinadi kwa hiyo kila mtu anayesikia anaona ndio mtazamo wa dunia na kujikuta anajitumukiza mumo.

    Binafsi nimefikia kuamini kwamba mwili wa mwanaume umekuwa designed for a woman. Tunayoyaona ni matatizo ya kujitakia na wala si asili yetu.

    ReplyDelete
  3. Nasoma kwanza utambuzi wa Munga Tehenan 'Maisha na Mafanikio', LEO SINA LA KUCHANGIA nawasoma wachangiaji wengine kama walivyofanya hawa. Nasubiri maoni ya Koero

    ReplyDelete
  4. !!!!!!!????????? Oooopsss,
    Kaaazi kweli kweli.......

    ReplyDelete
  5. Kweli ukikosa kuperuzi kwa siku tu unakosa mengi. Labda nirejee kwa swali hili kuwa kuna utafiti wowote uliowahi kuonesha ni kiasi gani cha wanaume wana nyumba ndogo? Labda tukipata idadi tutatafuta asilimia yao ndani ya wanaume wote ulimwenguni. Kwa ujumla nadhani kuna ukweli wa kiasi fulani lakini si wa kujuisha kila mtu.
    Labda nakosea

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi