Imebainika kwamba, iwapo warsha na makongamano yanayofanyika mbali yakitumiwa vyema na watu walio single na wanaotafuta wenza wa kufunga nao ndoa husaidia kufanikisha jambo hilo.
Kwanza, makongamano hukutanisha wadau mbalimbali wa rika tofauti tofauti walio single na wasio single ambapo kwa walio single wanaweza kutumia nafasi hiyo kusafisha nyota na kuvuta mpenzi mpya wa maisha.
Pili, kwa kawaida makongamano na warsha hukutanisha wadau wa kada mbalimbali ambao hujadili mada zinazoendana na taaluma au utashi wa waalikwa, hivyo ule muda wa mapumziko au majadiliano yanayofanyika kwa makundi huwawezesha wadau kujuana na vile vile kuzungumza lugha inayofanana kwa kuwa wote wana utashi unaofanana
Tatu, licha ya kwamba, makongamano na warsha huwa na mijadala mbalimbali na mafunzo, lakini pia katika ratiba kunaweza kuwa na shughuli mbalimbali kama vile ziara za pamoja kuona vivutio vya mji, sherehe za vinjwaji (Cocktails Party) au Chakula maalum cha usiku ambapo wadau hupata muda muafaka wa kujuana na kuzungumza kwa ukaribu jambo ambalo linaweza kutumiwa na wadau walio single kujaribu bahati zao na hata kupeana anuani kwa ajili ya mawasiliano huko mbeleni……
Hivyo basi kwa wale wanaotafuta wenza na walio katika nafasi nzuri ya kupata mialiko ya kuhudhuria makongamano na warsha zinazofanyika nje ya miji wanayoishi wanaweza kutumia hiyo fursa kujichanganya na kutumia mbinu ya mvuto ili kumvuta mpenzi mpya wa maisha na siyo kufanya ngono kwa ajili ya kujistarehesha, kwani hilo linaweza kuwakimbiza wapenzi wapya walio na nia ya kuoa au kuolewa kuwa mbali na wewe kwa kukuona kicheche…
No comments:
Andika Maoni Maoni