0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Feb 3, 2009

TUNAWEZA KUJIKATAZA KUHOFIA MAISHA YA KESHO!

Hatuna haja ya kuhofu

Nimeshawahi mara mbili au tatu kuzungumzia hofu katika maisha. Kwa kumbushana kidogo sio vibaya tukasema kwamba nilielezea hofu kama tabia ambayo badala ya kutupa ahueni hutuumiza, kwa kuhofia huwa tunaingia mahali ambapo tunashindwa kutafuta suluhu na badala yake kuanza kubabaika na kuharibu kila kitu.

Kuhofia maisha maana yake ni kuchukua maisha ya kesho ambayo ni ya kufikirika tu na kujaribu kuishi humo. Kwa kuwa maisha hayo ya kesho hayapo kuhofia ni hali ya kuishi nje ya uhalisia. Hofu hazijawahi kutatua tatizo lolote kwa mtu yeyote tangu kuumbwa kwa ulimwengu.

Hatukatazwi kupanga mipango yetu ya kesho na kesho kutwa, lakini tunapaswa kujua kwamba kuna tofauti kati ya kupanga na kuhofia. Kupanga ni kuweka katika utaratibu maalumu yale ambayo tungependa au tunatarajia kuyatekeleza baadaye. Kuhofia ni kuwa na hisia kwamba jambo au mambo hayatakwenda sawa kuwa na wasiwasi kwamba kuna baya litakalo tokea, iwe tunalijua au hatulijui.

Mara nyingi yale tunayohofia kuwa hayatokei kabisa. Kati ya mambo kumi ambayo yanatupa hofu imethibitika kuwa ni matatu au manne tu yanayotokea kama tulivyo hofu,. Unaweza kufanya jaribio hili. Chukua karatasi na kalamu, andika mambo yanayokupa hofu. Halafu ifiche karatasi hiyo mahali, baada ya miezi sita itoe karatasi hiyo huko mahali ulikoificha. Jaribu sasa kuangalia ni mangapi yametokea kama ulivyokua ukifikiri kati ya yale yaliyokuwa yanakupa hofu? Unaweza kushangaa bila shaka.

Lakini huenda haina maana sana nikikwambia kwamba usihofie kuhusu maisha, bila kukwambia au kukupa njia ambazo zinaweza kukusaidia katika kuondoa hofu ulizonazo au ambazo zinatarajia kukupata baadae.

Hofu za kimaisha huziko miguuni au machoni mwetu, bali zipo ndani ya vichwa vyetu. Kuanzia katika kufikiri kwetu tunajaza mawazo kwa fikra ambazo zinatufanya tuanze kuona kwamba mambo yatakwenda vibaya ama kuharibika. Tunapofikiri hivyo kwa muda mrefu hutokea tunaamini ambapo huanza kubabaika kana kwamba jambo tunalolihofia limeshatokea.

Ili tuweze kudhibiti hofu zetu inabidi tuanze kudhibiti au kukagua namna tunavyofikiri. Kwa sababu tangu tukiwa wadogo tulifundishwa kufikiri kwa namna fulani, na hivyo kuamini kwamba kufikiri ni suala lililo nje ya uwezo wetu, inabidi tutumie mbinu mbalimbali za kutufanya tujue au kugundua kwamba huwa tunafikiri na sisi ndio tunaowajibika na kufikiri kwetu.

Moja ya mbinu ya kutuondoa kwenye mawazo ya kututia hofu, hofu ambayo inaweza kukushangaza ni kuvaa mpira (rubber band) mkononi. Kila tunapojikamata tukianza kufikiri kwa njia ambayo inatutisha inatubidi tuvute mpira huo kwa nguvu na kuuachia huku tukijiambia kimoyomoyo ‘acha’ baada tu ya kufanya hivyo, inabidi tuyapeleke mawazo yetu kwenye jambo lingine ambalo litatupa moyo badala ya kututisha.

Njia nyingine ni kujiwekea muda kila siku ambao tutautumia kwa kuhofu tu. Inashangaza eh! Pamoja na kushangaza huko, njia hii imethibitika kuwa yenye msaada mkubwa sana katika kutuwezesha kujitoa kwenye mawazo yenye kututisha. Unakuwa na muda ambapo unawaza yale yanayokupa hofu za kimaisha unahakikisha unawaza hadi mwenyewe unasema “basi”.

Jambo ambalo inabidi tulizingatie ni kuhakikisha kwamba tukishamaliza kuhofu kwenye huo muda tuliojiwekea inabidi tusikubali kuweka tena mawazoni mwetu fikra za kutuhofisha. inatakiwa tuchukulie kwamba muda huo pekee ndiyo unayofaa na kuruhusiwa kuwa na hofu na hivyo kuzimalizia hapo hofu zetu.

Wakati mwimgine mawazo yenye kutuhofisha inaweza kuwa ni dalili ya tatizo la kiakili ambapo hufahamika kitaalamu kama
obsessive compulsive disorder ambapo mtu anajikuta hawezi kabisa kujiondoa kwenye kuhofia kwamba kuna jambo baya litakalotokea. Hata hivyo mtu mwenye hofu zitokanazo na tatizo hili, anakuwa na hofu za kiwango ambacho si cha kawaida. Kwa mfano; anaweza kuamka usiku hata mara kumi kukagua milango kama imefungwa kutokana na hofu ya kuibiwa.

Mtu kama huyu anatakiwa kumuona mtaalamu wa tiba ya kisaikolojia, ambaye anaweza kumrejesha kwenye kuiona hali halisi..

2 comments:
Andika Maoni Maoni
  1. Ahsante kwa maarifa haya ya namna ya kujikataza kuhofia maisha ya kesho,
    lakini kaka mtambuzi hiyo mbinu ya raba band, imenifurahisha sana.
    Kweli utambuzi una mbinu nyingi.

    ReplyDelete
  2. Ienibamba kweli kweli hadi kisogo kinawasha kwa utamu wa utambuzi

    ReplyDelete

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi