Tafiti nyingi zinaonesha kwamba,
karibu wanawake tisa kati ya kila kumi wanaridhishwa na maumbile ya sehemu za
siri za waume au mabwana zao.
Kwa hiyo, ni mmoja tu kati ya wanawake kumi
ambaye haridhishwi na saizi ya maumbile ya mpenzi wake.
Hii ina maana kwamba, ni wanawake
wachache sana wasioridhishwa. Lakini,
hawa wapenzi wao ni wale ambao kweli wana maumbile madogo kupindukia, ambao
idadi yao ni ndogo sana.
Kinachofanya wanaume kupanga foleni
kwa waganga kutaka kuongezewa ukubwa wa maumbile yao, ni kutokana na
kutojiamini kwa wanume hao.
Lakini lipo tatizo lingine, je ni lipi?
Wanaume wenye tatizo hili
linalofahamika kitaalamu kama small-penis syndrome, wanakabiliwa na
wasiwasi kwamba sehemu zao za siri ni ndogo, wakati wala sio ndogo, lakini
wanaume hao kwa bahati mbaya huamini
hivyo.
Kama nilivyosema awali, kuna wanaume
wachache sana wenye maumbile madogo kuliko kiasi, hali ambayo hufamika
kitaalamu kwa jina la kubeza la micropenis.
Hawa wenye wasiwasi wa kimaradhi, huaminikwamba, nao wako hivyo yaani maumbile
yao ni madogo kuliko kawaida, wakati si kweli.
Wastani wa maumbile yaliyowima ni
urefu kati ya inchi 5.5 hadi inchi 6.2. wale ambao wana maumbile madogo ambayo
hayawezi kukidhi utashi wa mwanamke wanakuwa na maumbile ya wima ya urefu wa
chini ya inchi 2.75. kumbuka nimesema maumbile wima, bila shaka mnanielewa
vizuri.
Ni wanume wachache sana wenye tatizo
hili, lakini karibu wanume watano kati ya kila kumi wangependa kuwa na maumbile
makubwa, bila kujali maumbile yao ya sasa hivi. Hii ni dunia nzima siyo hapa
nchini tu.
Hebu naomba mjipime kwanza kabla
hamjaingia kwenye ujinga wa kudhani kwamba maumbile yenu ni madogo au
hayawatoshelezi wake au wapenzi wenu.
No comments:
Andika Maoni Maoni