0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Dec 11, 2016

Mambo ya kuzingatia kabla ya kuwa mjamzito

UJAUZITO ni safari ndefu inayomchukua mwanamke miezi tisa au majuma arobaini hadi kujifungua. Ni safari yenye mikikimikiki na hatari nyingi kwa mama na mtoto. Tusichukulie suala la ujauzito kama jambo la kawaida ingawa pia ni wajibu kwa mwanamke.
Ujauzito siyo hali ya hatari au kutisha endapo mambo ya msingi yatazingatiwa kabla ya kuwa mjamzito na kipindi cha ujauzito hadi baada kujifungua.
Katika kipindi cha ujauzito kuna mambo mengi ambayo ni mabadiliko humtokea mama na mtoto aliye tumboni.
Katika makala haya tutazungumzia mambo ya kuzingatia kabla ya kuamua kubeba mimba, siyo kila mwanamke anaweza kubeba mimba kwa sababu wengine huwa na matatizo katika mfumo wao wa uzazi, aidha homoni zao hazifanyi kazi vizuri na mayai hayazalishwi au hayapevuki.
Huenda pia mirija ya uzazi imeziba au ana matatizo ndani ya kizazi.
NINI CHA KUFANYA?
Ni vyema upange sasa unataka kuwa mjamzito au mwezi fulani unataka kushika mimba, uwe na mpango. Hata hivyo, hakikisha umri wako upo zaidi ya miaka 20 kwa usalama zaidi wa afya yako. Mshirikishe mwenzi wako na mwambie ungependa upate ujauzito, siyo vizuri kushtukiza kwani inaweza kukupa ‘stress’ wewe mwenyewe au mwenzako endapo mmoja wenu hajajiandaa kisaikolojia.
CHEKI AFYA YAKO
Hakikisha una afya njema, huna magonjwa sugu kama kisukari, shinikizo la damu, magonjwa mengine ya moyo, kansa, HIV, kifafa, pumu, siko seli au grupu lako la damu ni RH Negative.
Endapo una matatizo haya hapo juu, basi haraka wasiliana na daktari wako wa masuala ya uzazi akupe ushauri kwani magonjwa mengine yatakusumbua wakati wa ujauzito, au magonjwa yenyewe yatamwathiri mtoto.
Hakikisha huna magonjwa au matatizo katika viungo vya uzazi, mfano kutokwa na uchafu ukeni wenye muwasho na harufu mbaya, vipele au vidonda sehemu za siri, maumivu wakati wa tendo la ndoa, kutokwa na damu au usaha ukeni. Vile vile mfumo wako wa uzazi uwe vizuri, matatizo katika mfumo wa uzazi ni kama vile maumivu ya tumbo chini ya kitovu, kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi, kutopevusha mayai na kukosa hamu ya tendo la ndoa.
VILEVI ACHA
Epuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara, hili hata kwa mwanaume anayetaka mtoto. Mwanamke kabla ya kuwa mjamzito hakikisha unakula sana mboga za majani ili upate kiwango kizuri cha vitamin ya Folic Acid, ni vema ule sana mboga za majani au upate virutubisho vya Folic Acid. Endapo hutakuwa na kiwango kizuri cha Folic Acid, kuna hatari ya kuzaa watoto wenye matatizo.
MAZOEZI
Fanya mazoezi mepesi mara kwa mara ili kuimarisha nyonga na viungo vyako vingine na usipate matatizo wakati wa kujifungua. Pata ushauri wa daktari kipindi muafaka.
Tibu magonjwa yanayoathiri mfumo wa uzazi, mfano maumivu ya korodani, maumivu ya njia ya mkojo, upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume. Kutoa manii mepesi sana kiasi kwamba baada ya tendo la ndoa manii zote zinatoka ukeni.

Nov 24, 2016

Wanawake na hisia za usaliti: zijue dalili zake

 



Inawezekana ukawa ni mke wa mtu au una mpenzi wako ambaye mna matarajio ya kufunga ndoa na kuishi pamoja. Kuna wakati unaweza kujaribiwa na kujikuta ukikabiliwa na hatari ya kumsaliti mpenzi wako. Kujaribiwa huko kunaweza kukutokea katika mazingira mbalimbali kutegemea na maeneo yako ya kazi au mahali unapofanyia shughuli zako za kila siku. Kwa mfano inaweza ikatokea umefahamiana na mwanaume mahali pako pa kazi, anaweza kuwa ni mteja au mfanyakazi mwenzio. Inatokea siku moja anakualika kwa ajili ya chakula cha mchana, baada ya mtoko huo, unajisikia kutoka naye kwa mara nyingine…………………

Nov 22, 2016

Athari ya kitambi kiafya


Kitambi ni hali ya kiafya ya mtu mnene ambapo mafuta ya ziada mwilini huongezeka eneo la tumbo kwa kiasi kikubwa.

Mtu akiwa na kitambi anapata athari kubwa ikiwamo kupungua kwa umri. Katika karne hii, hili ni mojawapo ya tatizo kubwa la kiafya duniani. Hata hivyo, tatizo la kitambi kiafya linarekebishika.

 Katika mawazo ya kizamani na hata sasa katika baadhi ya nchi mtu akiwa na kitambi anaonekana ni tajiri.

Tatizo la unene na vitambi litazidi kuongezeka ikiwa serikali, hususan wananchi wenyewe hawatachukua hatua za dharura na mipango madhubuti kulikabili.

Vitambi hupunguza maisha ya watu wenye hali hiyo ya afya, hivyo kusababisha upotevu wa rasilimali watu.

Ili kuepukana na athari hiyo watu wahakikishe wanabadili namna wanavyoishi na milo yao. Wengi wana muda mchache sana wa kutayarisha vyakula visivyo na mafuta mengi majumbani mwao, hivyo wanakula nje zaidi, yaani kwenye hoteli na migahawa na matokeo yake ni kuwa na vitambi.

Kuna wengi wanatambua athari za tatizo la unene na vitambi, lakini hawafanyi chochote kulirekebisha, hii inatokana na ukweli kwamba idadi kubwa ya watu hawajui maana halisi ya kuwa na afya njema.

 Watu wengi, hasa vijana wamekuzwa kwa kula chipsi, mikate na vyakula vya sukari na si mbogamboga na matunda.

Ukweli ni kwamba watu wengi hawafanyi mazoezi ya kutosha kama ilivyokuwa zamani hivyo, watu wenye vitambi wanaongezeka kila sehemu.

Kwa ujumla, umri wa mtu mnene mwenye kitambi huwa pungufu kwa miaka 8 had 10 ukilinganisha na mtu mwenye umbo la kawaida.

MAGONJWA

Hii inatokana na ukweli kwamba uzito wa mtu husababisha magonjwa ya moyo, aina fulani ya kisukari, magonjwa ambayo huua mamilioni ya watu duniani kote. Kifupi ni kuwa ukiwa na mafuta mengi mno utakuwa kwenye hatari ya kukumbwa na magonjwa kama ya kupanda kwa presha, magonjwa ya moyo,  kansa. Kuongeza uzito au kunenepa kunasababisha mwili ushindwe kupata sehemu ya kutosha ya kuhifadhi mafuta na hivyo kuanza kuyatunza mafuta hayo kwenye sehemu za ndani ya mwili, kuuzunguka moyo na ndipo matatizo yanapoanza.

USHAURI

Kila mtu aepuke kula vyakula vyenye mafuta mengi na kutokula chakula kupindukia na ule unaposikia njaa, kutotia mafuta mengi kwenye chakula na kutotumia sukari nyingi.

Kila mtu anatakiwa kufanya mazoezi ya kukimbia, kutembea au kuogelea angalau kwa nusu saa kila siku.

Watu wanashauriwa kuacha kutumia vyakula vya kopo na hasa vile vyenye gesi nyingi. Wale ambao ni wanene kupita kiasi waonane na daktari kwa ushauri wa kitaalamu.

Aug 10, 2016

Je, Mnajua tofauti ya mapenzi na mahaba?




Kwa mujibu wa wajuvi wa lugha, Mapenzi ni hisia za upendo kwa mwenza wako na mahaba ni vitendo vya kuyathibitisha mapenzi.

Jun 23, 2016

Utata maumbile ya wanaume!


Tafiti nyingi zinaonesha kwamba, karibu wanawake tisa kati ya kila kumi wanaridhishwa na maumbile ya sehemu za siri za waume au mabwana zao.


 Kwa hiyo, ni mmoja tu kati ya wanawake kumi ambaye haridhishwi na saizi ya maumbile ya mpenzi wake.
Hii ina maana kwamba, ni wanawake wachache  sana wasioridhishwa. Lakini, hawa wapenzi wao ni wale ambao kweli wana maumbile madogo kupindukia, ambao idadi yao ni ndogo sana.
Kinachofanya wanaume kupanga foleni kwa waganga kutaka kuongezewa ukubwa wa maumbile yao, ni kutokana na kutojiamini kwa wanume hao.

Lakini lipo tatizo lingine, je ni lipi?
Wanaume wenye tatizo hili linalofahamika kitaalamu kama  small-penis syndrome, wanakabiliwa na wasiwasi kwamba sehemu zao za siri ni ndogo, wakati wala sio ndogo, lakini wanaume hao kwa bahati mbaya  huamini hivyo.

Kama nilivyosema awali, kuna wanaume wachache sana wenye maumbile madogo kuliko kiasi, hali ambayo hufamika kitaalamu kwa jina la kubeza la micropenis. Hawa wenye wasiwasi wa kimaradhi, huaminikwamba, nao wako hivyo yaani maumbile yao ni madogo kuliko kawaida, wakati si kweli.

Wastani wa maumbile yaliyowima ni urefu kati ya inchi 5.5 hadi inchi 6.2. wale ambao wana maumbile madogo ambayo hayawezi kukidhi utashi wa mwanamke wanakuwa na maumbile ya wima ya urefu wa chini ya inchi 2.75. kumbuka nimesema maumbile wima, bila shaka mnanielewa vizuri.
Ni wanume wachache sana wenye tatizo hili, lakini karibu wanume watano kati ya kila kumi wangependa kuwa na maumbile makubwa, bila kujali maumbile yao ya sasa hivi. Hii ni dunia nzima siyo hapa nchini tu.

Hebu naomba mjipime kwanza kabla hamjaingia kwenye ujinga wa kudhani kwamba maumbile yenu ni madogo au hayawatoshelezi wake au wapenzi wenu.

Jun 14, 2016

Hafla, mitoko na ngono zisizo salama kwa wenetu



Mpaka miaka ya hivi karibuni mambo ya uchumba yalikuwa hayawezi kufanyika bila ya kuwepo wazazi na familia. Mitoko mingi na kualikana ilifanyika majumbani wakiwapo wanafamilia wote. Kujitokeza kwa usafiri na ugunduzi wa magari kumesaidia sana kuharibu utaratibu mzuri wa mitoko ya kimapenzi na uchumba kwa ujumla.

Mwanamke Unaweza kuwa mtabiri jinsi mwenzi wako atakavyokuwa baada ya miaka kumi……


[​IMG]

Ndio kwanza mmeanza uhusiano ambapo mnaelekea kufunga ndoa, wote bado ni vijana wabichi, hamna majukumu makubwa yanayohitaji fedha, hamna watoto, kwa hiyo fedha mnazopata ni kwa ajili ya kula na kusogeza maisha kidogo, huku mkipanga mipango yenu ya baadae kuhusu kufunga ndoa. Katika kipindi hiki kila mmoja anajaribu kuishi kama malaika, hataki kumkwaza mwenzake. Hata kama mwenzake amemkosea atakaa kimya na kuumia ndani kwa ndani kwa sababu ya hofu ya kuogopa kuonyesha tabia zake pale akasirikapo.

Tabia hiyo huwapa wakati mgumu wapenzi kujuana tabia, hususan kwa wanawake ambao hutamani sana kuwajua wapenzi wao jambo ambalo huwawia vigumu kutokana na sababu nilizozieleza hapo juu. Lakini zipo tabia ambazo anaweza kuwa nazo mwanaume ambazo ki ukweli hazina maana yoyote kwa wakati huo lakini zinakupa ujumbe mahsusi kwamba huko mbeleni mwanaume huyo uliye naye atakuwa mume mwema au hatakuwa mali kitu zaidi ya kuwa sawa na mzigo usiyo na mwenyewe.

Hapa chini nitaeleza baadhi ya vijitabia ambavyo vitakufanya umjue mwanaume uliye naye kama atakuwa ni mume wa namna gani:

Apr 1, 2016

UTUMIE HIVI MUDA WAKO BAADA YA SHULE

WANAFUNZI wengi wamekuwa wakitumia vibaya muda wao baada ya masomo. Wengine kwa michezo isiyo na maana, kushinda vijiweni, kutazama televisheni kupitiliza au kuwa bize na mitandao ya kijamii ambayo siku hizi imewateka vijana wengi hata ambao hawana faida nayo.
Ukweli ni kwamba wanafunzi wa aina hii, inawezekana kabisa wakawa wanafahamu au hawafahamu kuwa baada ya muda wa masomo ni muhimu kuwa na muda wa ziada wa kufanya mazoezi zaidi ili kupata uzoefu wa kujibu na kuelezea maswali.

Mar 19, 2016

Vitu ambavyo huwavutia wanaume wamwonapo mwanamke zaidi ya muonekano...!


Mwanamke, je umeshawahi kushitukizwa mtoko (dating) na mwanaume wakati wala ulikuwa huna mpango wa kutoka siku hiyo? Lakini pia umeshawahi kujikuta ukiwa unamvutia kila mwanaume unayekutana naye pamoja na kwamba hujajikwatua na urembo (Make Ups) kama ufanyavyo siku zote?

Ngoja niwamegee siri, Kuna baadhi ya vitu wanaume huvi-notice haraka sana wamuanapo mwanamke zaidi ya muonekano wa wake wa kawaida. Vitu hivi vinaweza kufunika maeneo ambayo hayakufanyiwa utanashati kwa siku hiyo, kwa mfano mwanamke anaweza akawa hajatengeneza nywele zake kwa muda mrefu au hajatengeneza kucha zale kwa muda mrefu, lakini inatokea pamoja na udhaifu huo wanaume wakawa wanamkodolea macho kwa kuvutiwa naye mpaka hata yeye mwenyewe akashangaa.

Mar 15, 2016

Je inakuwaje wanawake wasiotulia huopoa wanaume wenye muafaka...?


Kuna jambo moja huwa linawaacha wanawake wengi na maswali yasiyo na majibu na wengi huwa wanajiuliza maswali bila ya kupata majibu.

Kuna baadhi wanawake ambao hawajatulia, vijana wa mjini huwa wanawaita "utulivu ziro" yaani sio kwamba ni makahaba, hapana, lakini wanakuwa na tabia ya kutotulia na kuonekana kama wana vurugu kichwani. Kwa wanawake wengi huwa wanawaona wanawake wa aina hii kama sio wife material, yaani hawako katika kundi la wanawake wanaofaa kuolewa kutokana na tabia zao hizo za kutotulia.

[​IMG]
Lakini jambo ambalo huwa linawaacha wanawawake wengi na mwaswali ni pale wanapowaona wanawake wa aina hii wakiopoa wanaume wenye muafaka, yaani wanaume wenye sifa zinazowavutia wanawawake wengi kuolewa nao. Hapo ndipo yanapoibuka maswali mengi kwa baadhi ya wanawake wakijiuliza.

"Ni kitu gani kimemvutia huyu mwanaume kwa mwanamke yule.....!"

[​IMG]

Lakini jambo la kushangaza zaidi ni kwamba uhusiano wao unaweza kukua hadi kufikia kufunga ndoa, na usije ukadhani kwamba yule mwanamke atabadilika tabia, la hasha, anaweza kubaki na tabia yake hiyo hiyo ya kutotulia na bado akamudu kumshika huyo mwanaume barabara. Mwanaume huyo anaweza kujikuta amenasa na hawezi kuchomoka, na hata ikitokea wakitengana, haitapita muda wararudiana pamoja na uhusiano wao kutawaliwa na vurugu fulani fulani.

[​IMG]

Wapo baadhi huwa wanabadilika na kujenga uhusiano imara hata kuwashanganza watu wengi, lakini huwa ni wachache sana, narudia kusema, mara nyingi huwa ni wachache sana, lakini wengi wao pamoja na kutotulia na kuonekana kuwa na vurugu kichwani, lakini humudu kuwashika wanaume wenye muafaka na kuwaacha wanawake wenzao vinywa wazi.

Je ni jambo gani linatokea?



Ukweli wa jambo hili umegawanyika sehemu mbili:

Mosi: Wanaume wengi watulivu, wapole, yaani wale wanaoitwa "husband material" ni watu ambao huwa hawana mbinu wala guts za ku approach na kuwapata wasichana wanaofanana nao i.e watulivu, wapole na wanaoitwa "wife material"! Hii inatokana na ukweli kwamba wanaume wapole huwa pia wana aibu na ni waoga sana wa kutongoza! Upande wa pili, wanawake watulivu huwa ni waoga na wagumu sana kupatikana.. meaning unatakiwa uwe na mbinu za ziada kuweza kuwapata. Hili ni tatizo la kwanza ........................................................................................

Pili: Wanawake wengi "utulivu ziro" wanawafahamu wanaume ambao ni "husband material", na wanafahamu kwamba ni waoga, na wana aibu. Wanawake hawa hutumia ujanja wao wa mjini kujisogeza karibu na wanaume hawa (kitu ambacho wanawake wapole hawathubutu kufanya kwa kuogopa "nitaonekanaje?") na kuanzisha nao mahusiano pole pole huku wakijua kabisa kwamba wanaume hawa wakishanasa watafanya kila liwezekanalo kuhakikisha hawajinasui! ...................................... 

 Matokeo yake sasa.. utakuta wanaume wapole, watulivu, wakioa wanawake utulivu sifuri huku wanawake wapole, watulivu wakichukuliwa na wanaume utulivu sifuri ambao ndio hasa wenye mbinu na uthubutu wa kuwafata na kuwatongoza..!

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi