tag:blogger.com,1999:blog-355810992072839076.post330520564324160454..comments2023-06-18T14:45:58.364+03:00Comments on UTAMBUZI NA KUJITAMBUA: THAMANI YAKO UNAYO, HAIWEZI KUCHUKULIWA NA YEYOTE!Anonymoushttp://www.blogger.com/profile/17192821931569912610noreply@blogger.comBlogger4125tag:blogger.com,1999:blog-355810992072839076.post-64181967334631548812010-04-19T17:23:39.878+03:002010-04-19T17:23:39.878+03:00hii inanikumbusha story ya mtoto mmoja ambaye alik...hii inanikumbusha story ya mtoto mmoja ambaye alikuwa anataka kujinyonga kutokana na kuwa alikuwa hapendwi na kila mmoja, si katika familia bali pia shuleni na ktk jamii nzima.

akasikia toka redioni juu ya washauri nasaha naye akaenda kupata ushauri utakaomsaidia aharakishe ama aahirishe kwa muda alichokuwa anataka kukifanya.

Daktari wa masuala ya akili aliposikia akashindwa kujua amsaidieje. Wakati akiwa hajui anusuruje maisha ya kijana huyu mdogo ambaye alikuwa na akili sana darasani akatoa noti 2 za $100. Moja akaiweka ktk matope na kuitoa.

Kisha akamuuliza mtoto: ni ipi kati ya hizi noti mbili (bill) inaweza kununua vitu zaidi ya nyingine?

Mtoto akajibu: ZOTE ZINA THAMANI SAWA!

Dkt akamjibu kuwa wewe sasa uko ktk stage hii ya matope kwa hiyo hata iweje THAMANI YAKO IKO PALE PALE kama wengine!

Mtoto akaondoka zake akiwa na taswira mpya kuhusu yeye.

Yes: HATA IWEJE, thamani yetu iko palepale!

Asikudanganye mutu YOYOTEEE!o'Wambura Ng'wanambiti!https://www.blogger.com/profile/17146066311562834541noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-355810992072839076.post-77594413452022636622010-04-18T08:05:21.709+03:002010-04-18T08:05:21.709+03:00Kaka Kaluse, sitokosea kuungana na kaka Matondo na...Kaka Kaluse, sitokosea kuungana na kaka Matondo na da Yasinta.
Unajua mara nyingi huwa tunajipotosha kuona fulani ni mtu muhimu sana na sisi tupo alimradi tupo. Kumbe tunasahau hata sisi tuna thamani kubwa pasipo kujali hali yetu kwa wakati huo.
Ahsante sana kwa somo zuri.
Ni post inayofaa kusomwa na kila mtu.
Jumapili njema kaka.Fadhy Mtangahttps://www.blogger.com/profile/10322331153810581894noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-355810992072839076.post-28889555434443678412010-04-17T20:42:13.360+03:002010-04-17T20:42:13.360+03:00Nasema kama Pro. Matondo ni kweli habari kama hii ...Nasema kama Pro. Matondo ni kweli habari kama hii inabidi watu wengi wasome ni habari nzuri sana na inafundisha- Kwani ni kweli kuna watu ambao wanajisona haweana thamani hhata bila sababu. Kaka Kaluse ni kweli hilo gazeti la jitambue lifufueni na muandike habari kama hizi. Natumaini ujembe huu wengi watasoma.
Na halafu kaka Kaluse umenikumbusha mbali kweli hiyo picha wakati nilipokuwa mdogo baba alipokuwa anatoka kazini duh! mpaka raha, Ahsante kaka:Yasinta Ngonyanihttps://www.blogger.com/profile/09314172793959023532noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-355810992072839076.post-79919392729130804952010-04-17T19:03:31.661+03:002010-04-17T19:03:31.661+03:00Bwana Kaluse;
Nilikuwa ninatazama hapa dakika chac...Bwana Kaluse;
Nilikuwa ninatazama hapa dakika chache tu zilizopita kipindi cha Mtambuzi mmoja anayeitwa Dr. Wayne Dyer na alikuwa anaongelea jambo hili hili. Bila kutambua thamani yetu tunajiweka katika nafasi ya kupoteza muda wetu katika mambo yasiyo na faida, tukijaribu kuwafurahisha watu huku tukidhani kwamba thamani yetu inaamuliwa nao. Pia tunapoteza uwezo wa kujiamini na wakati mwingine maisha yetu yanakosa mwelekeo na mwishowe tunashindwa kufika tunakopaswa kufika.

Nilimuuliza swali hili Kamala jana. Lile gazeti lenu la Jitambue lililokuwa likichapisha makala za Munga Tehenan lingalipo? Kama limekufa pengine itabidi mfanye mkakati mlifufue. Makala kama hizi zina nguvu za kubadilisha maisha ya watu na inabidi ziwafikie wasomaji wengi kwa kadri inavyowezekana. Msichoke wala kukata tamaa!!!Masangu Matondo Nzuzullima (MMN)https://www.blogger.com/profile/17267350894732424957noreply@blogger.com