0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Feb 4, 2014

MWANAMKE: JE UMESHAWAHI KUWA NA MAHUSIANO NA MWANAUME MWENYE TABIA YA UPEKEPEKE...?


Mwanamke: Je ushawahi kuwa na mahusiano na mwanaume mwenye tabia ya upekepeke....?


Sisi binadamu tuna tabia na mienendo inayotofautiana. Mara nyingi huwa tunatambuana kwa tabia au mienendo yetu wenzetu huita personality. Miongoni mwa tabia au personality inayowachanganya wanawake ni ile ya introvert, mimi ningependa kuiita upekepeke kwa kiswahili nadhani neno hilo linaweza kufaa katika kuelezea tabia hiyo.

Mtu mwenye tabia ya upekepeke, wakati mwingine watu huweza kumdhania kama ana aibu hivi, lakini si kweli watu wenye tabia ya upekepeke hawana aibu kama inavyodhaniwa bali ni watu ambao huishi katika dunia yao kifikra, wanapenda sana kuzingatia mawazo yao ya kina na fikra zao.

Mara nyingi hawapendi kujichanganya kwenye mikusanyiko ya watu na kama inatokea kufanya hivyo basi ni kwa wale watu ambao anawafahamu kwa undani. Wanasaikolojia waliowafanyia utafiti watu wenye tabia za namna hii waligundua kwamba pale watu wenye tabia za namna hii wanapojumuika katika mikusanyiko, hupoteza nguvu zao (kumbuka kwamba sisi tunazo nguvu zinazotuzunguka lakini huwa zinatofautiana kwa mtu na mtu, ndio maana wapo wanaoweza kuona yale yatarajiwayo kwa njia ya maono). 

Baada ya kujumuika katika mkusanyiko wa watu kwa muda mrefu kidogo kwa mfano katika sherehe fulani hivi watu wenye tabia hii ya upekepeke (Introvert) huhitaji muda kuwa peke yao ili kurudisha nguvu zao walizopoteza (recharge)

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi