0715 72 92 92

SHABAN KALUSE

Kwa Matangazo na mambo mbalimbali & Wasiliana Nami

http://www.serenahotels.com/serenadaressalaam/default-en.html

Jul 4, 2013

MWANAUME ANAPOKOSA 'CHAKULA' NYUMBANI, HUWEZA KULA CHOCHOTE MTAANI...!



Kwa kawaida kadiri mwanaume anavyokosa tendo la ndoa kutoka kwa mwenzi wake ndivyo ambavyo anazidi kujishinikiza kihisia. Kama atakosa tendo kwa wiki nzima mambo huwa magumu zaidi, kwa sababu bila kujijua mwanaume hubadilika na kuwa kama simba au chui mwenye njaa aliye tayari kumvamia na kumjeruhi yeyote.

Nataka niwaambie wanawake kwamba, kama hujitahidi kuhakikisha kwamba, mumeo anamaliza kiu yake, hasa kama ana kiu sana, unachofanya ni kutengeneza mzimu ndani mwako. Mume anayekandamiza hasira za kunyimwa tendo la ndoa na mwenzi wake anakuwa kama mzimu.


Labda niwape siri moja kuhusu athari za njaa ya tendo la ndoa kwa wanandoa. Mkisikia au kusoma katika vyombo vya habari kwamba, mume amemuuwa mke wake kwa sababu ya wivu wa kimapenzi, jaribuni kuchunguza. Inawezekana kabisa, mke huyo kabla hajauawa alikuwa hampi mumewe unyumba, hivyo kumfanya mumewe akusanye maumivu ya kihisia ya kunyimwa unyumba na mkewe yaliyomfikisha mahali pa kugeuka kuwa mzimu uliommaliza mkewe. 


Tafiti nyingi zinakubaliana na jambo hili kwamba, kwa sababu ya uzalishwaji wa mbegu za kiume, homoni ya sili ya testosterone na sababu nyingine, mwanaume huhitaji kufanya tendo la kujamiiana angalau mara tatu kwa wiki ili aweze kuhisi ahueni. Labda tu pale ambapo mwanaume anaumwa, ana matatizo ya kusongeka kiakili au muda mdogo sana, ndipo ambapo anaweza kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa. Lakini hata mkewe anapokuwa na matatizo ambayo yanamfanya asiweze kushiriki tendo la ndoa na mwanaume anampenda mkewe, anaweza kabisa kuratibu hisia zake na kumudu kuvumilia. 


Lakini kama inatokana na mwanamke kutojisikia kufanya na kama mawasiliano kuhusu jambo hilo hayajawa wazi, mwanaume hugeuka kuwa mzimu kweli. Kumbuka kuna migogoro mingi sana ndani ya ndoa ambayo chanzo chake ni tendo la ndoa, ingawa wanandoa wanakuwa hawaoni. Wanaume wanahitaji tendo la ndoa zaidi kuliko wanawake na hiyo haina maana kwamba, ni wahuni au wazinzi, hapana. Kama mwanamke atajitahidi kuwa kiongozi wa jambo hili na hasa kufungua milango ya mwasiliano, yeye ndiye atakayenufaika zaidi.


Mwanamke anapaswa kukumbuka kwamba, hamu ya mwanaume kwenye tendo la ndoa ni kama mwito wa kimwili kama ilivyo njaa. Je, mtu akikosa chakula akipendacho hawezi kula chochote ili kuuwa makali ya njaa? Hiyo hufanyika sana………..! 

KUNA WANAWAKE WANAOWAFUNGASHIA WAUME ZAO NA KUWAPELEKA KWENYE NYUMBA NDOGO...!



Hebu fikiria mwanaume anatoka kazini na anapofika nyumbani tu anakutana na ‘kiama’ cha maneno na lawama au kero. Baada ya madhila ya kazi ya kutwa nzima ya kutafuta riziki kwa ajili ya familia, mwanaume hupenda kuona akirudi nyumbani anapata fursa ya kupumua na kusahau adha za kazini.

Lakini anaporejea na kukutana na adha nyingine, kimaumbile hukereka. Kimaumbile binadamu awaye yeyote anapokereka au kutishika atafanya jambo moja kati ya haya mawili. Ama atapambana au kukimbia. Ukiona Simba na kutishika kwa mfano, utaamua kupambana naye au kukimbia.


Kama mwanaume ataamua kupambana na hali hiyo, ni afadhali kwa sababu inaweza kuwa ni kubishana au kupigana (mara nyingi mwanamke kupigwa) Lakini mwanaume anapoamua njia ya pili ya kukimbia maana yake ni kutafuta mahali ambapo akitoka kazini ataachwa apumzike kabla hajaanza kuzogomwa na mahali hapo si pengine bali kutafuta nyumba ndogo itakayompa nafasi ya kupumzika baada ya madhila ya kazini.


Kuna wanawake ambao wanaamini kwamba, wakisema au kulalamikia jambo mara nyingi, yaani kila dakika, basi jambo hilo litatafutiwa ufumbuzi. Huu ni uongo na imani ya hatari sana. Wanawake wengi ni wazungumzaji sana, yaani wanapenda kulikuza jambo tena na tena na tena. Ni kama vile wanajaribu kuingiza maaarifa fulani kwenye kichwa cha mtoto asiyeelewa kirahisi.


Badala ya kuzungumza jambo kwa kifupi na upendo, hata kama ni la kukera, mwanamke ataanza hotuba na kuhubiri kusikoisha. Badala ya kuangalia upande mzuri wa jambo hilo na kuzungumzia upande huo ili taaarifa ifike vizuri zaidi, mwanamke atatafuta udhaifu na kung’ang’ania kuzungumzia upande huohuo.


Wasichojua wanawake hawa ni kwamba, miongoni mwa mambo ambayo wanaume huyachukia ni kuhubiriwa kama vile wamekuwa wasiojua kitu na wasioelewa kitu. Lakini pia kuambiwa jambo mara nyingi kama kwamba wao ni mbumbumbu huwakera sana wanaume kuliko wanawake wanavyofikiria. Tabia hiyo humfanya mwanaume amwone mkewe kama kisirani na kuanza kumkwepa au kumdharau. 


Mwanamke anaposema jambo anatakiwa kusema ni jambo gani hasa analenga, siyo kuzunguka. Anachotakiwa ni kuzungumzia jambo hilo na kutoa nafasi kwa mume kutafakari na kulitolea ufafanuzi au kutekeleza, siyo kukumbushia na ya mwaka juzi. Pia si vyema kukebehi au kumkejeli mume wakati wa kukumbushia jambo. Hii ni kwa sababu wanaume hawataki kukumbushwa ya juzi na wala hawako tayari kuvumilia kukejeliwa……….

 

MWANAMKE: AINA 10 ZA WANAUME WA KUEPUKA KUWA NA MAHUSIANO NAO HAWA HAPA...!



1. Mwanaume Kicheche:

Hakuna mwanamke anayependa kuchezewa na wanaume, labda tu kama anafanya hivyo katika juhudi zake za kujikwamua kiuchumi, lakini pale mwanamke anapokuwa katika harakati za kutafuta mwanaume ambaye kama mambo yakiwa mazuri wafunge ndoa, ni vyema akajiepusha na wanaume vicheche wanaotongoza wanawake kwa lengo la kustarehe na kumaliza matamanio yao ya ngono. wakati mwingine mwanaume mwenye tabia ya kuchezea wanawake anaweza kumfuata mwanamke ambaye ametamani mwili wake na kujifanya eti amebadilika na kuwa mtakatifu. Anaweza kujiweka katika mazingira yanayoonyesha kwamba amebadilika ili kumvuta mwanamke. Shituka mwanamke, jasiri haachi asili atakutumia kama condom na kisha kukutupilia mbali. Wanaume wenye tabia hizo ni vigumu kubadilika. Inahitaji subira ya hali ya juu kujiridhisha kama kweli amebadilika au anazuga ili apate anachokitaka.




2. Mwanaume asiye na kazi na asiyejishughulisha:

Mwaume asiye na kazi na asiyejishughulisha ni mzigo usio na mwenyewe. Mwanaume asiyejishughulisha eti kwa sababu hajapata kazi huyo hana malengo. Kukubali kuwa na uhusiano na mwnaaume wa aina hiyo ni sawa na kuishi na mtu mfu anayetembea (dead alive), labda tu kama atakupa sababu inayoingia akilini kuhusu kutokuwa kwake na kazi na kutojishughulisha kwake. Kama atakuwa ni mtu wa kulalamika tu kwamba hakuna ajira na haonyeshi dalili zozote za kuhangaika kutafuta hata vibarua ili kujikimu eti kwa sababu ni msomi na badala yake anageuka kuwa ombaomba kwa ndugu zake na marafiki zake Nawashauri wanawake muwaepuke wanaume wa aina hii kwani hawafai wanataka kulelewa. Kama amekuona unafanya kazi au una vibishara vyako vinavyokuingizia shilingi mbili tatu zinazokufanya uishi vizuri hapa mjini jua kwamba hicho ndicho kilichomvuta kwako, ukikubali umekwisha maana atakukamua hadi tone la mwisho kisha ahamie kwa mwingine, si kilichomleta kwako hakipo, sasa awe na wewe kwa lipi....



3. Mwanaume asiyejiamini:

Kukubali kuwa na mahusiano na mwanaume asiyejiamini ni sawa na kuishi na bomu ndani ya nyumba. Mwanaume asiyejihisi kuwa yuko salama na mwenye mashaka muda mwingi kuhusu uhusiano wenu, hutawaliwa na wivu wa ajabu ambao licha ya kukuletea fedheha kwa ndugu, jamaa na marafiki zako, lakini pia anaweza kukudhuru au hata kukutoa roho siku moja. Wanaume wasiojiamini mara nyingi ni watu wa kujitilia mashaka kuhusu hali zao za kipato na uwezo wao katika tendo. Kuwa na mahusiano na mwanaume asiejiamini inabidi uishi kwa akili na uchague maneno ya kuzungumza kila uwapo naye, kwani kila neno utakalotamka litatafutiwa tafsiri na kitakachofuata ni tafrani, sasa tabu yote ya nini..... Tupa kule hafai kwa mchuzi wala kwa kulumangia...




4.Mtoto wa mama:

Inawezekana mwanaume akalazimika kuishi nyumbani kwao kwa muda baada ya kumaliza masomo au amepoteza ajira na akawa bado hajapata ajira au hajapata shughuli ya maana itakayomwezesha kujitegemea, hii inakubalika. Hata hivyo kama mwanamke anakutana na mwanaume ambaye anaishi na wazazi wake na haonyeshi dalili za kutafuta kazi au shughuli yenye kipato itakayomwezesha kuondoka hapo kwao na kujitegemea, usije ukajiingiza katika uhusiano na mwanaume wa aina hiyo, itakula kwako, huyo ashakuwa kupe na tegemezi, utakuwa ni mzigo wako na atakuganda kama luba na kupoteza bahati ya kukutana na wanaume wenye mwelekeo wa maisha. 




5. Mwanaume anayependa kutukuzwa kama mfalme:

Unaweza kukutana na mwanaume aliyejipachika kibandiko ufalme ambaye anapenda sana kuhudumiwa kama mfalme. Yaani anataka afanyiwe kila kitu, na hajishughulishi kukusaidia kazi hata zile zinazotakiwa zifanywe na mwanaume, yeye kazi yake ni kukaa sebuleni na kuangalia TV au kusoma vitabu au magazeti huku akiagiza kila kitu asogezewe miguuni. Hawezi hata kunyanyuka kufuata kitu anachotaka na badala yake ni kuamrisha aletewe. Mwanaume wa aina hii ni wa kuepukwa kwani mwanamke kukubali kuwa na uhusiano na mwanaume mwenye tabia za kupenda kutukuzwa kama mfalme ni kutaka kuishi kwa msongo wa mawazo na jakamoyo na hivyo kufupisha umri wako wa kuishi hapa duniani. Kinga ni bora kuliko tiba, ukikutana na mwanaume wa aina hii chapa lapa hakufai..




6. Mwanaume mwenye utititri wa watoto kila kona:

Mwanaume kuwa na watoto nje ya ndoa si jambo la kushangaza siku hizi, lakini pale unapokutana na mvulana mwenye umri wa miaka 25 lakini ana watoto watatu kwa mama tofauti, mh! hapo sikushauri ujiingize kwenye uhusiano na mwanaume huyo. Hata hivyo si lazima awe na miaka 25 tu hata mwanaume mwenye umri mkubwa zaidi ya huo halafu ana watoto watatu au hata wanne au zaidi kutoka kwa mama tofauti ni wa kuepuka. Hivi atakupa sababu gani zilizomfanya akawa na watoto kwa mama tofauti kila kona ya mtaa mpaka umuelewe! Kuwa na mahusiano na mwanaume aina hiyo ni kukaribisha shari nyumbani kwako maana kila siku utapata wageni wanaokuja kudai hela za matumizi kutoka kwa mumeo tena wengine watakuja kishari hasa na kukuharibia siku. Mh mh! sikushauri mwanamke, sepa zako, bado nafasi unayo ya kumpata mwanaume mwingine mwadilifu.




7. Mwanaume anayejipenda mwenyewe:

Mwanaume anayejipenda mwenyewe ni kizungumkuti kingine ambacho wanawake wanapaswa kujiepusha nacho. Utakuta mwanaume anajipenda mwenyewe hakuna anachojali kuhusu mwenzi wake zaidi ya kujijali yeye mwenyewe. Wanaume wenye tabia hii ya kujipenda wenyewe, huwa wana kawaida ya kujijali wao wenyewe. Wanataka wavae nguo nzuri za thamani ili wao wapendeze na si wenzi wao. Swala la kumjali mwenzi wake halipo katika vichwa vya wanaume wa aina hii kabisa. Mwanamke sikushauri uingie katika moto huu.





8.Mwanaume bahili:

Unakutana na mwanaume mtoko wa kwanza tu anakuchagulia aina ya chakula au kinywaji kwa kuangalia bei rahisi na wakati wa kulipa anahesabia hela yake mfukoni, huyo ni janga. Utakapoingia katika uhusiano na mwanaume wa aina hii atakusumbua sana na pia katika kupanga bajeti nyumbani usishangae akihesabu finyango za nyama au vipande vya samaki jikoni. Sikushauri mwanamke, we ingia mitini hakufai huyo........




9.Mwanaume chapombe mlevi kupindukia:

Hakuna ubaya mtu kunywa pombe, hasa kama unajua kiwango chako cha unywaji, lakini kuwa na uhusiano na mwanaume mlevi anayekunywa pombe kupindukia kila siku non stop 24/7 huyo hafai. Mwanaume wa aina hii ndio wale wanaosema kunywa pombe watoto wakitembea uchi atajua mama yao. Hata siku moja hawezi kuzungumzia maendeleo kwa ustawi wa familia, kwake utakuwa ni msamiati mgumu. 




10. Mwanaume mwenye kisirani na asiyeweza kumuuwa nyoka akafa :

Mwanaume mwenye kisirani ni ngumu sana kuishi naye. Mwanaume mwenye kisirani na anayependa kuweka vitu rohoni na asiyeweza kusamehe ni janga. kuishi na mwanaume wa aina hii ni sawa na kuishi na explosive material ambayo yakipata joto tu hulipuka. Mwanaume umetoka naye mtoko wa kwanza na kwa bahati mbaya mhudumu wa mghahawa akasau kitu katika vitu mlivyoagiza akagomba kupita kiasi na kuwakusanya mameneja wote wa mghahawa akiwemo mpishi mkuu akilalamika. Na kama hiyo haitoshi mtaondoka hapo mghahawani njia nzima kambeba kichwani mhudumu yule masikini aliyeghafilika mpaka mwisho wa safari yenu na huenda akalala naye kichwani. Mwanaume huyo hafai kama gome la mgomba lisilofaa kwa dawa ya miti shamba wala kuni, labda kwa kufungia ugoro. Huyo mpishe ajiendee zake hakufai......

WANAWAKE NA UMBEA WA SALUNI...!



Kwenye Saluni nyingi za wanawake, mazungumzo mengi yanahusu maisha ya watu na hasa kuhusu mapenzi na kipato, kashfa na saikolojia zisizo rasmi kuhusu ndoa na uhusiano. Kuna mazungumzao ya kukatishana tamaa na kuumizana zaidi, kwa sababu kila mmoja anajaribu kuonyesha kwamba ana nafuu fulani.


Lakini mbaya zaidi ni kwamba, saluni za wanawake hutumiwa na wanawake hao kama maeneo ya kusemea hisia zao chungu na kutoa jumuisho kuhusu wanaume na uhusiano. Huko saluni hakuna wataalamu, bali kuna wazungumzaji ambao wanaamini wao ni wataalamu, na wengine kwa sababu ya kuzidiwa na mzigo wa matatizo hasa ya uhusiano na pengine ya kipato, huwaaamini hao wataalamu wasio rasmi. 



Huko saluni ndiko ambako wanawake wanaambiana`kwamba, mwanaume akiacha kufanya tendo la ndoa kwa wiki moja na mpenzi wake, ni lazima mwanaume huyo atakuwa na ‘nyumba ndogo.’ Ndiko ambako wanafundishana kwamba, ukipata Mganga wa nguvu unaweza kumshika mwanaume. Ndiko huko ambako hutajwa orodha ya wanawake ambao wamewashika waume zao kupitia kwa waganga. Ndiko huko ambako majina ya waganga maarufu hutajwa.


Lakini ndiko huko saluni ambako, wanawake hutaja orodha ya wanawake wenzao waliopata mali kupitia ‘mabuzi,’ ambao huwapa mitaji ya biashara inayowawezesha kusafiri hadi Uchina. Pia hutajwa majina ya wanaume wanaohonga sana. Ni saluni ambako wataalamu wasio rasmi hutoa suluhu ya matatizo ya ndoa. Ndiko ambako wataalamu hao huwaambia wanawake wenzao kwamba, ukimuonyesha mwanaume kwamba unampenda sana, atakudharau na kukuacha.


Kwa hiyo mwanamke akitoka saluni anakuwa ametoka shule anayoiamini . ambapo huacha kumwonesha mumewe kwamba, anampenda. Ni wazi shule hii ya saluni haijui kwamba, unapoonesha kutokupenda, nawe utaoneshwa kutokupendwa. Kwani unachopanda ndicho unachovuna. Wakati mwingine shule hii inajua jambo hilo, isipokuwa inataka waliopotea na kuharibikiwa wawe wengi.


Ni huko saluni ambako utasikia wanawake wakifundishana namna ya kuwadanganya wanaume zao. Hufundishana namna ya kujenga nyumba bila kunaswa na mume, kwani wanaume hawaaminiki, huwezi kuacha kujiandaa. Lakini shule hii haijui kuwa, hiyo ni sumu kubwa kuliko sumu nyingine kwenye ndoa, kutafuta mali na kujenga msingi wa kipato kwa siri.


Ni hukohuko saluni ambako wanawake huambiana uongo kuhusu wakwe, watoto wa kambo, na mawifi. Hufundishana kwamba, kumpenda mama mkwe au wifi ama mtoto wa kambo ni kutafuta muhali. Haiishia hapo huendelea kufundishana hata namna ya kuwachukia watu hao.


Mwanaume, kama ukiona mwenzi wako anakwenda saluni na akitoka huko amekuwa mtu mwingine kabisa, unapaswa kujua kwamba, huenda amepata ‘dozi’ ya wataalamu hao.


Wanawake, nawashauri jihadharini sana na maneno ya saluni. Kwani katika kila maneno mia moja, ni moja tu linalokaribia ukweli. Kumbuka, linalokaribia ukweli . siyo kuwa ni la kweli……

WARSHA NA MAKONGAMANO: YAKITUMIWA VIZURI NA WALIO SINGLE HUSAIDIA KUMPATA MWENZA

 


Imebainika kwamba, iwapo warsha na makongamano yanayofanyika mbali yakitumiwa vyema na watu walio single na wanaotafuta wenza wa kufunga nao ndoa husaidia kufanikisha jambo hilo.


Kwanza, makongamano hukutanisha wadau mbalimbali wa rika tofauti tofauti walio single na wasio single ambapo kwa walio single wanaweza kutumia nafasi hiyo kusafisha nyota na kuvuta mpenzi mpya wa maisha.


Pili, kwa kawaida makongamano na warsha hukutanisha wadau wa kada mbalimbali ambao hujadili mada zinazoendana na taaluma au utashi wa waalikwa, hivyo ule muda wa mapumziko au majadiliano yanayofanyika kwa makundi huwawezesha wadau kujuana na vile vile kuzungumza lugha inayofanana kwa kuwa wote wana utashi unaofanana


Tatu, licha ya kwamba, makongamano na warsha huwa na mijadala mbalimbali na mafunzo, lakini pia katika ratiba kunaweza kuwa na shughuli mbalimbali kama vile ziara za pamoja kuona vivutio vya mji, sherehe za vinjwaji (Cocktails Party) au Chakula maalum cha usiku ambapo wadau hupata muda muafaka wa kujuana na kuzungumza kwa ukaribu jambo ambalo linaweza kutumiwa na wadau walio single kujaribu bahati zao na hata kupeana anuani kwa ajili ya mawasiliano huko mbeleni……


Hivyo basi kwa wale wanaotafuta wenza na walio katika nafasi nzuri ya kupata mialiko ya kuhudhuria makongamano na warsha zinazofanyika nje ya miji wanayoishi wanaweza kutumia hiyo fursa kujichanganya na kutumia mbinu ya mvuto ili kumvuta mpenzi mpya wa maisha na siyo kufanya ngono kwa ajili ya kujistarehesha, kwani hilo linaweza kuwakimbiza wapenzi wapya walio na nia ya kuoa au kuolewa kuwa mbali na wewe kwa kukuona kicheche…

This Blog Designed by DonSoo, Contact 0656212326.DonSoo
Kaa Karibu na Mimi